Uchaguzi 2020 Ninakusudia kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Buyungu kupitia CCM

Uchaguzi 2020 Ninakusudia kuchukua fomu ya kugombea Ubunge Buyungu kupitia CCM

Ninakusudia kuchukua fomu ya Kugombea Ubunge. Safari hii ni Kupitia Chama Cha Mapinduzi.

Kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa Mgombea wa CCM Jimbo la Buyungu itawasaidia Wana CCM wa Wilaya ya Kakonko kuwa na Machaguo mengi.

Kuhusu Ushindi wa CCM kwa nafasi ya Urais,hapo hakuna kazi kwasababu mambo aliyoyafanya Mh Rais Magufuli yanatosha kabisa kuitetea CCM.

Hata baadhi ya Majimbo yaliyokuwa Upinzani yanaweza yakapitiwa na Mafanikio ya Mh Rais na CCM.

Nia thabiti pamoja na rekodi zangu za nyuma zinanipa ujasiri wa kurudi Buyungu.
Wanaccm wakiona ninawafaa kwa Sasa nitakuwa tayari kuyavaa majukumu hayo ya Uwakilishi.




Turn out kubwa ya vijana kuchukua form za kugombea uongozi mwaka huu sio "mwamko" inatupa ujumbe fulani. Vyama vimeacha kabisa kuwekeza kwenye kuandaa viongozi kwa kuwajenga katika misingi ya uongozi. Ile dhana ya kazi ngumu na nzuri kuwa msingi wa mafanikio imeshakufa miongoni mwa vijana na kila mmoja anataka shortcut kuelekea mafanikio na njia pekee ni SIASA. Wameshaona mifano kwenye zile nunua nunua na teuzi. Mtu anatarget kuwa nikiukosa ubunge nitasubiri uteuzi.
 
hata katibu kata ni nafasi yenye heshima, wewe ni nani hapo ulipo na una kipi cha kujivunia

Sent using Jamii Forums mobile app

Ukiwa masikini kabisa na uwezo mdogo wa kupambana, hicho cheo kitakuwa cha maana kwako. Ila mwanaume kabisa, tena kijana unayesimamisha vizuri, ni aibu kusema uko kwenye hicho cheo. Hicho cheo kinafaa wazee wasio na ndoto zozote kwenye dunia hii.
 
Mkuu nimeona comments nyingi zimekushambulia sana,pole sana mkuu,ila Mimi katika maisha yangu naamini kuwa mtu pekee anayeweza kunitakia mafanikio ni baba na mama tu,hivyo basi wanaokuvunja moyo wasikuumize kichwa

Kila la kheli mkuu

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app

Ukiona kijana anavaa kaunda suti za kitambaa cha polister kinachong'aa, na travoltar za kizee, jua huyo ni mshamba mwenye mawazo ya kizee, na njaa kali.

Cc: Elia F. Michael
 
Kiukweli kwa sasa huaminiki tena..mwa wananchi umekua kigeugeu malaya wa kisiasa..imani na wananchi haipo tena kwako..labda ubebwe na mbeleko za ukandamizi..ila hautakua chaguo la wananchi...

#MaendeleoHayanaChama.
 
Dogo umeamua kucheza bahati nasibu ya kisiasa. Kwa sasa nafasi za kuchaguliwa haiwezekani tena kwako. Uliharibu kote kote. CCM hawakutaki na upinzani haukutaki pia.

Na usipokuwa makini hata huo ukatibu kata utaupoteza soon (ikiwa Magufuli atasimamia maneno yake ya kuwatumbua wateule wake waliokuwa vimbelembele kwenda kugombea vyeo vingine).

Ushauri wangu kwako, hili liwe funzo kwako, usaliti unaweza kukupa maslahi ya muda mfupi sana lakini usaliti utakutesa maisha yako yote, utaua ndoto zako na utakufanya kudhihakiwa na vizazi vingi vitakavyofuata. Jifunze kwa Yuda Askarioti.
 
Mapeasant ndio picha zao hizo. Huyo dogo huwa anavaa kaunda suit za kitambaa cha polister zinazong'aa, yaani ni mshamba wa kiwango cha lami.
Hahahahahahaha hahahahahaha jamani
 
Huyu jamaa kuna siri kubwa nyuma ya pazia.Huyu Jamaa CCM hakuingia kwa hiari.Inaonekana hakuwa na chaguo jingine zaidi ya kujiunga CCM
 
Nimepitia comments zote, nimemhurumia mtoa mada,...... Pole kijana baki mzee kasema mtosheke na mlichonacho
Halafu hawasemi lo lote wamekazana tu kumpopoa mawe. Alishafanya kosa gani huyu dogo? Si kwa kushambuliwa huku wallaqi !!!
 
Back
Top Bottom