Ninamtafuta Baba yangu anaitwa Gervas Kalilo. Alikuwa anaishi Kahama Mtaa wa Uhindini miaka ya 1990

Ninamtafuta Baba yangu anaitwa Gervas Kalilo. Alikuwa anaishi Kahama Mtaa wa Uhindini miaka ya 1990

Pierina Vicka

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2017
Posts
241
Reaction score
516
Wana-JamiiForums, habari za majukumu

Naja mbele yenu nikiomba msaada wa hali na mali wa kupata dondoo yoyote itakayoniwezesha kumpata baba yangu mzazi ambaye sijawahi kumwona tangu nizaliwe. Naitwa Pendo Gervas Kalilo, na kwa sasa sipo nchini Tanzania lakini kiu yangu kubwa ni kumfahamu baba yangu mzazi au ndugu zake.

Historia kwa ufupi:
Marehemu mama yangu alikuwa anaitwa Khadija Omary Kabona. Mwishoni mwa miaka ya 1990, mama alikuwa anafanya kazi za ndani kule Kahama, Mtaa wa Uhindini kwa bosi mmoja wa asili ya Asia (Mhindi). Ndipo hapo alipokutana na baba yangu, Gervas Kalilo, na mimi nikazaliwa. Mwaka 1993

Kufuatia kifo cha mama yangu mnamo mwaka 1999, nilibaki na kulelewa na bibi yangu kule Masumbwe, Wilaya ya Mbogwe, Mkoani Geita. Kutokana na mazingira hayo, sina kabisa mawasiliano au dondoo zozote za upande wa baba yangu.

Ombi Langu kwa Wana-JF (Hasa wa Kahama na Geita):
  • Kama wewe ni mwenyeji wa zamani wa Mtaa wa Uhindini, Kahama na unamkumbuka bosi yeyote wa Kihindi aliyekuwa anaishi hapo miaka ya 90 na alikuwa na wafanyakazi wa ndani.
  • Kama unamfahamu au kuwahi kusikia mtu anayeitwa Gervas Kalilo (huenda hili ni jina lake kamili au Kalilo ni jina la ukoo wake).
  • Kama unafahamu familia yoyote ya akina "Kalilo" inayopatikana maeneo ya kanda ya ziwa (Shinyanga, Geita, Mwanza).

Tafadhali naomba unisaidie dondoo yoyote, hata iwe ndogo kiasi gani inaweza kuwa ufunguo wa kunikutanisha na baba yangu mzazi.

Mawasiliano:
Unaweza kunitumia ujumbe wa faragha hapa (PM) au kuwasiliana na mwakilishi wangu aliyeko Tanzania kwa namba: 0689 848090.

Nawasilisha, na mnasaba wa kipekee naomba msaada wenu wa kusambaza ujumbe huu. Mungu awabariki.
 
Kwanza pole na hongera kwa wakati mmoja. 1993-2026 means you are 33+20=50yrs and above ndio miaka mzazi wako na umeamua kumtafuta. Kama kweli unamtafuta kwa amani, hata kama hutompata ubarikiwe sana na kwa niaba ya babako nakuombea upate baraka kushoto kulia upate watoto wengi wazibe hiyo mianya yote. Mungu akuonyeshe njia ufanikishe jambo lako la kumtafuta mzee.
Lakini kama ni utani nakuombea asubuhi uamke umejikojolea mwili mzima hadi machoni.
 
Aisee kwanza nashukru kwa Dua zako njema kwangu🙏 pili nipo serious sio utani kama unavyofikiria tatu ninamtafuta kwa nia njema kabisa ya aman na lengo kubwa nikutaka kumfahamu tu na kujua asili yangu hiyo tu itatosha na nitapata aman sana kwa kadiri ya iman yangu ipo siku nitampata na itakua siku njema sana kwangu🙏
 
Ngoja nimuulize rafiki yangu Kelvin Navin wa Primary (Muhindi) wa mtaa huo huo kama ana hints japokuwa ni kitamboo.
Aisee muulize kelvin kama anawajua wale vijana watatu wanene wa kisomali walikulia mitaa hio miaka ya 80 mpaka 90
 
Back
Top Bottom