Hata kama mimi ni MCCM damu damu ukweli moyoni ni binadamu bado. Tunachomfanya TAL hakika ninamwomba Mungu ama yeye mwenyewe TAL akija bahatika akaingia madarakani au MwanaCCM mwingine yeyote akimpokea mama asije akakifanya.
Asitokee mwanaCCM au TAL akaamua tu kumwanzishia tuhuma mtangulizi wake na mpaka kuamua kumpeleka mahabusu na kumfikisha mahakamani kama tunavyomfanya TAL.
Hii inatokea sana kwa wenzetu, kuwaweka watangulizi wao ndani kwa makosa hasa yanayohusikana na ubadhirifu wa mali za umma, ambayo ni rahisi viongozi kuyatenda - makosa yasiyo na dhamana au hata yenye dhamana.
Lisitokee hapa Tanzania jamani!