Ninaomba mchanganuo wa biashara rahisi... Wanangu hawajalipiwa karo na maisha hayaendi. Nina 500,000 tu ndugu zangu, nifanye nini?

Toka ARUSHA huko NENDA dar katafute maisha..Unapokua huna hela na unaona mkoa uliopo Hauna Furrsa ONDOKA kwa MUDA sio kwamba unaikimbia familia yako ila MAISHA ndio yanayokufanya hivyo. so utafanya kazi utawajali familia yako na kkwa kua umejiajiri una uwezo wa Kila WIKI kurudi ARUSHA kusalimia familia yyako kama kweli ukifika huko dar UTAPAMBANA ipasavyo.

Mwanaume unatakiwa uwe kama mwanajeshi ukishaamua kuwa mfanyabiashara/mkulima unaweza ondoka kwenda kazini ukakaa miezi kadhaaa kisha ukarudi MUHIMU tu uwe UNAJITAMBUA
 
Hahah ila wahindi kwa fursa
Sio watu wa mchezo kabisa
Hatari sana kina Kanjibai..wanajua pesa haoooo Asilimia 70 ya wanaouza maji,juice,soda take away wale wanaotembeza Wanapewa na Wahindii..tena Haina cha mdhamana wala nini ni wewe tuuu na utayari wako Fika pale OMBA mzigo unapewa..
 
Mkuu hii kazi ushaifanyaga?
 
Mi ni mchangiaji tu,, nilikua namsaidia mwenye mada..

Nadhani atakua kasoma
Sent using Unknown device
 
Su Sure Mkuu,UBISHOO NA UVIVU NI NYUMBA YA NJAA!
 
Hatari sana kina Kanjibai..wanajua pesa haoooo Asilimia 70 ya wanaouza maji,juice,soda take away wale wanaotembeza Wanapewa na Wahindii..tena Haina cha mdhamana wala nini ni wewe tuuu na utayari wako Fika pale OMBA mzigo unapewa..
Hahahah mradi upeleke hesabu yake!
 
Safi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Upo smart sana braza, nimekukubali kwa wazo dogo lakini very viable

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maji ya kandoro si yalipigwa marufuku mkuu? Au kibishibishi tunasonga?
 
Maji ya kandoro si yalipigwa marufuku mkuu? Au kibishibishi tunasonga?
hiyo hata siijui mkuu, ndo kwanza naiskia kwako Hata ivyo kibish tu zinaenda bwana maana wakikataza kandoro wawakataze na mama ntilie kama wanaweza.
 
Kwenye laki tano hiyohiyo anunue viti, meza, cret za bia na maji yake, cret za soda na maji yake, glass, leseni, kodi ya nyumba, kodi ya serikali/TRA, friji na vikorokoro vyote?

Mkuu acha utani na hii biashara ya kuuza vinywaji

auze bia, sio viti wala friji
 
hiyo hata siijui mkuu, ndo kwanza naiskia kwako Hata ivyo kibish tu zinaenda bwana maana wakikataza kandoro wawakataze na mama ntilie kama wanaweza.
Sawa mkuu, Ni idea nzuri natamani ningekuwa dar. Huku nilipo hiyo idea haitalipa kivile
 
Tafuta eneo lenye makazi ya watu au mkusanyiko wa watu fanya biashara ya kuuza kahawa na kashata mida ya jioni/asubuhi,fungua hata vibanda vitatu maeneo tofauti tofauti...uwawekee na radio, wasikilize Dw,BBC n.k
kahawa na kashata atatumia kiasi gani cha pesa kutengeneza na atauza kwa kipimo kipi na bei ipi ili apate faida?
 
kahawa na kashata atatumia kiasi gani cha pesa kutengeneza na atauza kwa kipimo kipi na bei ipi ili apate faida?
Kuna watu wanaishi kutokana na hizi biashara,ndio maana vijiwe vipo na haviitaji mtaji mkubwa cha muhimu ni uthubutu na kupata eneo lenye msongamano wa watu.
 
Kuna watu wanaishi kutokana na hizi biashara,ndio maana vijiwe vipo na haviitaji mtaji mkubwa cha muhimu ni uthubutu na kupata eneo lenye msongamano wa watu.
sawa sijakataa Equation x nachotaka hapa ungetufafanulia atleast na mchanganuo wa mahitaji ili mtu ajue anaanzia wapi,
 
sawa sijakataa Equation x nachotaka hapa ungetufafanulia atleast na mchanganuo wa mahitaji ili mtu ajue anaanzia wapi,
Kwa haraka haraka nitaweka hivi:-
  1. Ufuta 1kg@5000
  2. karanga 1debe@20,000
  3. sukari 5kg@2500
  4. kahawa 10pkt@ 1000
  5. Benchi za mbao 4@15000 (ukiweka viti vya plastic wateja hawataki)
  6. Tangawizi 1000
  7. Maji ndoo 500
  8. Birika 20000
  9. Chupa ya chai 2@15000
  10. Mkaa 1debe@10000
Tumia nguvu zako kutengeneza na kucheka na wateja
 
Wengi wanapenda mawazo ya biashara ya kufungua yard ya magari kwa laki 2,bila kujua ili ufike pakubwa lazima uanzie chini kama changamoto ni mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…