Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

Ahsante sana dada kwa ushauri nashukuru.

Napambana sana na kutokujitenga ila dah kuna wakati na mazingira mengine unaona kabisa unakuwa shida na kujikuta automatically upo mwenyewe yaani. (Hapa simu ndio huwa mkombozi wangu)

Ninajikuta tu kwenye baadhi ya matukio au mialiko nalazimika kwenda ili kukamilisha ratiba basi, nionekane nipo nimeudhuria basi lakini kiuhalisia natoka na kitu kidogo sana au empty at all.

Ubaya wa hii hali haionekani moja kwa moja kwa nje kama vile vipofu au ulemavu wa viuongo vya nje (ni mpaka umsumbue sana mtu kimawasiliano na kumfanya arudierudie mno ndio anaweza kugundua) sasa mpaka agundua unakuta mtu aisha jaa hasira sana na kukuchukulia vibaya.

Matokeo yake unakuta ukilazimisha sana kujichanganya na watu hasa wasiokufahamu unaambulia kujichukia na kujaa mastress tu, hata kuwachukia watu kabisa, unakuta sehemu kama class au meetings au kwenye masherehe, church nk unashangaa wenzako wanacheka tu, we utaishia kutabasamu baada ya wao kumaliza kicheko au kuonekana upo siriasi kumbe hakuna kitu, au kuchelewa baadhi ya vitendo vilivyo amrishwa kwa kutumia sauti ( nilikula sana mabanzi na matusi jkt😀😎)

So dada sometime kujitenga na baadhi ya matukio au kuwa mbali nayo hasa napogundua sina watu naoweza kuwa nao karibu huko tunaofahamihana inakuwa na unafuu mkubwa na kunipunguzia stress na kujilaumu juu ya hali ya masikio.

Unakuta upo kwenye harusi labda au umealikwa kwenye sendoff za watu huko au party na masherehe bahati mbaya najikuta mwenyewe tu nimetulia tuliii kama maji ya mtungi, mtu mwingine katika hali hiyo atakuona ni kama unamatatizo dunia nzima labda so atajongea mpige stori mbili tatu utamuangaisha hadi atakuacha mwenyewe😀😀.

so kuepuka yote hayo unaona ni mara mia kuignore baadhi mambo na kujitenga nayo kwani badala ya kukusaidia unajikuta yanakuongezea maumivu tu.

Kaka siwezi kukueleza nadhani unafahamu changamoto zenu especially sisi wahanga mi madhira mno duniani mi binafsi najikubali na matatizo yangu haya nilikuwa chairman chuoni tena muongeaji hata kweny presentation sema siku nyingine naomba sifanyi presentation nilikuwa na stress husasani piga hesabu nikta kuwasilian na mama siwezi kwa simu na meseji mama hajasoma hata darasa moja baba mae ni mzee sana kuchat macho ynamuuma naumia sana ndo ivyo natumia mtu karibu nae hswa kuna kipnd mama nilimtumia pesa kupitia kwa mtu anayejua kuchati akala pesa kama laki 3 yeye ananimbia niko na mama yako anasema asante
 
Aisee...unaweza meza mtu jamani...!
 
Aisee pole sana mkuu, naelewa
 
Diagnosis Treatment:

It is important to seek treatment early. Treatment for this condition usually requires an outpatient surgical procedure known as canalplasty. One of our skilled surgeons will use a binocular microscope to remove the exostotic growth. Generally a through-the-ear-canal (endaural) approach is used and a chisel-type technique.

If the bony growths extend close to the ear drum, the surgery may be done from behind the ear through an incision. You will go home the same day as the procedure, and the recovery period is at least one month. If ear plugs are not worn after the ear canals have healed, surfer's ear can return over the course of several years.

The best way to prevent surfer's ear is to wear ear plugs while surfing. Other methods of prevention include wearing a hood or special headband that covers and seals the ears. Wearing ear plugs and a hood or headband together adds even more protection.
 
Tupe tafsiri mkuu hili janga limetukumba wengi sana hasa graduators
 
Habari za humu ndugu zangu.
Poleni kwa majukumu.

Changmoto inayonirudisha nyuma sana:
Ninachangamoto ya usikivu mdogo(Hard hearing, Hearing loss), kushidwa kuelewa kinachozungumzwa kwa kiasi fulani (Word deafness) hasa kwa sauti za besi sana sometime ninaweza nisikuelewe maneno utamkayo, watu wanaoongea kwa spidi sana au harakaharaka sana mara nyingi naweza nisielewe, au nikaelewa maneno ya mwanzo unapoanza kuongea, utakapoweka vituo na mwishoni tu unapomalizia, Sometime kuelewa utakachosema ni mpaka nikuface nitazame lips za mzungumzaji ndio ninaweza kuelewa maneno yote, Sehemu zenye kelele nyingi kama sokoni nk au tukiwa tunaongea huku kukiwa na sauti za labda tv, radio au sauti zingine zaidi (Background noises) tunaweza tusielewane kabisa (kukusikia nitakusikia vizuri tu ila sehemu kubwa ya speech sitakuelewa),

kwa mfano ninaweza kuwa kanisani ambapo kuna vipaza sauti vingi tu na sauti ni kubwa sana ila nikikaa ndani nisielewe kitu na sehemu kubwa ya speech nikaipoteza lakini nikitoka na kukaa nje ya kanisa nikaelewa kila kitu na kila neno vizuri kabisa, Pia watu ambao wanaongea sauti ya chini sana mara nyingi siwasikii kabisa mfano mtu akiwa anaongea huku anatafuna labda chakula nk kumsikia nitamsikia vizuri tu ila kwa sehemu kubwa naweza nisimwelewe. (Auditory verbal agnosis)

Wakuu ni ngumu sana kwa wenye changamoto za masikio (Hard hearing) kuelezea hali zao mpaka kueleweka vyema kwa yanayowasibu (hasa kama hujawahi kuishi na mtu mwenye usikivu mdogo, Hearing loss) Hivyo nimejaribu kuelezea vyema hali yangu ya masikio na mazingira yanayonipa shida kumudu usikivu, natumaini kwa kiasi icho nilichojaribu kujielezea walau unaweza nielewa kidogo nini hasa ninachopitia.

Historia fupi ya hii changamoto:
ni takribani miaka 10 sasa tangu mwaka 2011 nimekuwa nikiishi na hali hii mpaka leo navoandika ivi sijafanikiwa kupata utatuzi wa changamoto yangu hii ya usikivu hafifu, changamoto hii ilianza kidogokidogo, nilianza kuitambua hasa na kujihisi usikivu unashuka nilipomaliza masomo yangu ya O-level mwaka 2011. (kiukweli mpaka sasa sijui chanzao cha changamoto hii wala sababu ya usikivu kushuka)

ikanibidi niendelee na masomo ya A-level na hali hii mpaka namaliza, Zaidi kuanzia Elimu ya degree ilinibidi niisome kwa nguvu nyingi na kupambana sana, Kiukweli Tangu level hii nimekuwa nikisoma kwa macho (kutazama) zaidi kuliko masikio (kusikiliza), kujifundisha na kujisomea mwenyewe vitabu ndio umekuwa msaada kwangu.

Tangu nilipogundua changamoto hii, nilianza kutafuta tiba kupitia clinics za masikio, hospitali ya aga ghan mara mbili, nikaenda muhimbili kote huko mwisho wa siku niliishia kupewa mashine za masikio (Analogy Hearing aids) bahati mbaya hazikunisaidia chochote hata nilipo jaribu kuzibadilisha sikufanikiwa kupata hata nafuu.

Mwaka 2018 nilienda bugando na kuishia kupata dozi ya vidonge vya "Neurobin" ambavyo nilitumia kwa muda wa miezi sita bila mafanikio yeyote baada ya dozi kuisha nikaambiwa nitafute Hearing machines, Mwaka 2019 mwishoni nilifanikiwa kupata mashine za kisasa kabisa zilizoboreshwa zenye latest technology (Digital Hearing AIds) kwa millioni 14 lakini bahati mbaya sana nazo hazijanipatia nafuu yeyote japo ni imara na nzuri zaidi ya zile za mwanzo za analogy.

Adha nazokutananazo:
Upweke uliopitiliza na kulazimika kuwa mwenyewe mwenyewe muda mwingi hasa ninapokuwa nje ya watu wanaoelewa hali yangu.
kushindwa kumanage conversations, kushindwa kumudu vizuri majadiliano hasa ya watu zaidi ya wawili,
ukimya uliopitiliza, nalazimika kujikuta mkimya sana hasa ninapokuwa na watu wasionifahamu, mfano kwenye vyombo vya usafiri, mikutanoni nk. kuficha hali hii rafiki yangu mkubwa kwenye mazingira kama haya amekuwa ni simu.
kujifanya na kuonekana kama ninazarau, najivuna au sina heshima imekuwa ni sehemu ya maisha yangu hasa kwa watu wasionifahamu.
Mahusiano na kujenga urafiki kwa kiasi kikubwa imekuwa ni tatizo sana kwangu.
kulazimika kutumia nguvu nyingi sana katika baadhi ya mazingira ili kusikia na kuelewa ninachoambiwa

Hivyo Wapendwa kwa yeyote anayewezakuwa anaefahamu tiba yeyote ya changamoto hii ya hearing loss, au hata kulipunguza kwa kuongeza usikivu na kunipunguzia adha nazokutananazo naomba anisaidie.

PIa hata msaada wa kimawazo na ushauri wa jinsi au mbinu yeyote ya kupambana na hali hii hasa kwa kupunguza changamoto na adha mbalimbali nazokutananazo nilizozieleza hapo juu nitashukuru sana.

View attachment 1799771
Mkuu pole kwa maradhi yako ya usikivu mdogo (Hearing loss) Nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole Mkuu.
 
Hiyo Hali Ni Kama yangu na nimekwisha kata tamaa.
Mkuu pole kwa maradhi yako ya usikivu mdogo (Hearing loss) Nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibia upate kupona maradhi yako uguwa pole Mkuu. Usikate Tamaa tiba zipo n aunatmia na kupona kabisa maradhi yako.
 
Hi inanihusu kwa asilimia Mia,
 
Duuu huu uzi mtamu ingawa unasikitisha Sasa hapa naona kila hasikii vizuri

Anyway mi mwenye muhanga pia
 
Nishajikubali ndugu yangu, na ndio hasa kinachonipa amani na nguvu ya kupambana na mambo mengine kwa furaha, ila sasa kuyakatia tamaa ndio nashindwa aisee.

NimekuPM inbox unisaidie zaidi kuhusu lugha za alama mkuu.
Mngeelekezana hapahapa kwa faida ya wengi
 
Tatizo linawakumba wengi sana na mbaya zaidi halina Tiba ya kueleweka Hearing aids zipo za model mbalimbali jaribu ICC model pia Cochlea implant ndio suluhisho lakini garama zake ni MIL 39 TZS [emoji34]
Mh! Hiyo mipesa yote hiyo loh!
 
Back
Top Bottom