Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

Habari za humu ndugu zangu.
Poleni kwa majukumu.

Changmoto inayonirudisha nyuma sana:
Ninachangamoto ya usikivu mdogo(Hard hearing, Hearing loss), kushidwa kuelewa kinachozungumzwa kwa kiasi fulani (Word deafness) hasa kwa sauti za besi sana sometime ninaweza nisikuelewe maneno utamkayo, watu wanaoongea kwa spidi sana au harakaharaka sana mara nyingi naweza nisielewe, au nikaelewa maneno ya mwanzo unapoanza kuongea, utakapoweka vituo na mwishoni tu unapomalizia, Sometime kuelewa utakachosema ni mpaka nikuface nitazame lips za mzungumzaji ndio ninaweza kuelewa maneno yote, Sehemu zenye kelele nyingi kama sokoni nk au tukiwa tunaongea huku kukiwa na sauti za labda tv, radio au sauti zingine zaidi (Background noises) tunaweza tusielewane kabisa (kukusikia nitakusikia vizuri tu ila sehemu kubwa ya speech sitakuelewa),

kwa mfano ninaweza kuwa kanisani ambapo kuna vipaza sauti vingi tu na sauti ni kubwa sana ila nikikaa ndani nisielewe kitu na sehemu kubwa ya speech nikaipoteza lakini nikitoka na kukaa nje ya kanisa nikaelewa kila kitu na kila neno vizuri kabisa, Pia watu ambao wanaongea sauti ya chini sana mara nyingi siwasikii kabisa mfano mtu akiwa anaongea huku anatafuna labda chakula nk kumsikia nitamsikia vizuri tu ila kwa sehemu kubwa naweza nisimwelewe. (Auditory verbal agnosis)

Wakuu ni ngumu sana kwa wenye changamoto za masikio (Hard hearing) kuelezea hali zao mpaka kueleweka vyema kwa yanayowasibu (hasa kama hujawahi kuishi na mtu mwenye usikivu mdogo, Hearing loss) Hivyo nimejaribu kuelezea vyema hali yangu ya masikio na mazingira yanayonipa shida kumudu usikivu, natumaini kwa kiasi icho nilichojaribu kujielezea walau unaweza nielewa kidogo nini hasa ninachopitia.

Historia fupi ya hii changamoto:
ni takribani miaka 10 sasa tangu mwaka 2011 nimekuwa nikiishi na hali hii mpaka leo navoandika ivi sijafanikiwa kupata utatuzi wa changamoto yangu hii ya usikivu hafifu, changamoto hii ilianza kidogokidogo, nilianza kuitambua hasa na kujihisi usikivu unashuka nilipomaliza masomo yangu ya O-level mwaka 2011. (kiukweli mpaka sasa sijui chanzao cha changamoto hii wala sababu ya usikivu kushuka)

ikanibidi niendelee na masomo ya A-level na hali hii mpaka namaliza, Zaidi kuanzia Elimu ya degree ilinibidi niisome kwa nguvu nyingi na kupambana sana, Kiukweli Tangu level hii nimekuwa nikisoma kwa macho (kutazama) zaidi kuliko masikio (kusikiliza), kujifundisha na kujisomea mwenyewe vitabu ndio umekuwa msaada kwangu.

Tangu nilipogundua changamoto hii, nilianza kutafuta tiba kupitia clinics za masikio, hospitali ya aga ghan mara mbili, nikaenda muhimbili kote huko mwisho wa siku niliishia kupewa mashine za masikio (Analogy Hearing aids) bahati mbaya hazikunisaidia chochote hata nilipo jaribu kuzibadilisha sikufanikiwa kupata hata nafuu.

Mwaka 2018 nilienda bugando na kuishia kupata dozi ya vidonge vya "Neurobin" ambavyo nilitumia kwa muda wa miezi sita bila mafanikio yeyote baada ya dozi kuisha nikaambiwa nitafute Hearing machines, Mwaka 2019 mwishoni nilifanikiwa kupata mashine za kisasa kabisa zilizoboreshwa zenye latest technology (Digital Hearing AIds) kwa millioni 14 lakini bahati mbaya sana nazo hazijanipatia nafuu yeyote japo ni imara na nzuri zaidi ya zile za mwanzo za analogy.

Hivyo Wapendwa kwa yeyote anayewezakuwa anaefahamu tiba yeyote ya changamoto hii ya hearing loss, au hata kulipunguza kwa kuongeza usikivu na kunipunguzia adha nazokutananazo naomba anisaidie.

PIa hata msaada wa kimawazo na ushauri wa jinsi au mbinu yeyote ya kupambana na hali hii hasa kwa kupunguza changamoto na adha mbalimbali nazokutananazo nilizozieleza hapo juu nitashukuru sana.

View attachment 1799771
Pole kwa yote unayopitia.

Kuna mambo ya muhimu kuzingatia.
Tatizo la usikivu ni suala mtambuka, linahusisha wanataaluma wengi, kuanzia bingwa wa masikio/ENT, Audilogist na pia daktari bingwa wa mishipa ya fahamu.

Matatizo haya yanahusisha aina na kiasi chake.

1: Aina hutegemea na sehemu gani ya sikio inahusika.

2: Kiasi hutegemea na madhara husika

Tiba halisi hutegemea na hayo yote hapo juu na wakati mwingine tiba huusisha kuwekewa visaidizi au watu kueleza hali ya ufanisi wa tiba kutokumsaidia mhusika.

Pia, tiba hutegemea uwepo wa teknolojia mbalimbali kuwepo eneo husika.

NB: Ni vyema kuhakikisha tunapata maana ya kile ambacho:

1: Mtaalamu wa afya ameking'amua nini kama tatizo unapokuwa nae. Muda husika unakuwa umelipiwa na ni haki yako kupata taarifa sahihi na elimu sahihi.

2: Nini mtaalamu wa afya anaweza kufanya ili kutatua tatizo.

3: Nini kinaweza kufanyika zaidi ikiwa utaalamu na teknolojia vikiwepo sehemu husika/alternative.
 
Habari za humu ndugu zangu.
Poleni kwa majukumu.

Changamoto inayonirudisha nyuma sana:
Ninachangamoto ya usikivu mdogo(Hard hearing, Hearing loss), kushindwa kuelewa kinachozungumzwa kwa kiasi fulani (Word deafness) hasa kwa sauti za besi sana sometime ninaweza nisikuelewe maneno utamkayo, watu wanaoongea kwa spidi sana au harakaharaka sana mara nyingi naweza nisielewe, au nikaelewa maneno ya mwanzo unapoanza kuongea, utakapoweka vituo na mwishoni tu unapomalizia, Sometime kuelewa utakachosema ni mpaka nikuface nitazame lips za mzungumzaji ndio ninaweza kuelewa maneno yote, Sehemu zenye kelele nyingi kama sokoni nk au tukiwa tunaongea huku kukiwa na sauti za labda tv, radio au sauti zingine zaidi (Background noises) tunaweza tusielewane kabisa (kukusikia nitakusikia vizuri tu ila sehemu kubwa ya speech sitakuelewa),

Kwa mfano ninaweza kuwa kanisani ambapo kuna vipaza sauti vingi tu na sauti ni kubwa sana ila nikikaa ndani nisielewe kitu na sehemu kubwa ya speech nikaipoteza lakini nikitoka na kukaa nje ya kanisa nikaelewa kila kitu na kila neno vizuri kabisa. Pia watu ambao wanaongea sauti ya chini sana mara nyingi siwasikii kabisa mfano mtu akiwa anaongea huku anatafuna labda chakula nk kumsikia nitamsikia vizuri tu ila kwa sehemu kubwa naweza nisimwelewe. (Auditory verbal agnosis)

Wakuu ni ngumu sana kwa wenye changamoto za masikio (Hard hearing) kuelezea hali zao mpaka kueleweka vyema kwa yanayowasibu (hasa kama hujawahi kuishi na mtu mwenye usikivu mdogo, Hearing loss) Hivyo nimejaribu kuelezea vyema hali yangu ya masikio na mazingira yanayonipa shida kumudu usikivu, natumaini kwa kiasi icho nilichojaribu kujielezea walau unaweza nielewa kidogo nini hasa ninachopitia.

Historia fupi ya hii changamoto:
ni takribani miaka 10 sasa tangu mwaka 2011 nimekuwa nikiishi na hali hii mpaka leo navoandika ivi sijafanikiwa kupata utatuzi wa changamoto yangu hii ya usikivu hafifu, changamoto hii ilianza kidogokidogo, nilianza kuitambua hasa na kujihisi usikivu unashuka nilipomaliza masomo yangu ya O-level mwaka 2011. (kiukweli mpaka sasa sijui chanzao cha changamoto hii wala sababu ya usikivu kushuka)

ikanibidi niendelee na masomo ya A-level na hali hii mpaka namaliza, Zaidi kuanzia Elimu ya degree ilinibidi niisome kwa nguvu nyingi na kupambana sana, Kiukweli Tangu level hii nimekuwa nikisoma kwa macho (kutazama) zaidi kuliko masikio (kusikiliza), kujifundisha na kujisomea mwenyewe vitabu ndio umekuwa msaada kwangu.

Tangu nilipogundua changamoto hii, nilianza kutafuta tiba kupitia clinics za masikio, hospitali ya aga ghan mara mbili, nikaenda muhimbili kote huko mwisho wa siku niliishia kupewa mashine za masikio (Analogy Hearing aids) bahati mbaya hazikunisaidia chochote hata nilipo jaribu kuzibadilisha sikufanikiwa kupata hata nafuu.

Mwaka 2018 nilienda bugando na kuishia kupata dozi ya vidonge vya "Neurobin" ambavyo nilitumia kwa muda wa miezi sita bila mafanikio yeyote baada ya dozi kuisha nikaambiwa nitafute Hearing machines, Mwaka 2019 mwishoni nilifanikiwa kupata mashine za kisasa kabisa zilizoboreshwa zenye latest technology (Digital Hearing AIds) kwa millioni 14 lakini bahati mbaya sana nazo hazijanipatia nafuu yeyote japo ni imara na nzuri zaidi ya zile za mwanzo za analogy.

Hivyo Wapendwa kwa yeyote anayewezakuwa anayefahamu tiba yeyote ya changamoto hii ya hearing loss, au hata kulipunguza kwa kuongeza usikivu na kunipunguzia adha nazokutananazo naomba anisaidie.

PIa hata msaada wa kimawazo na ushauri wa jinsi au mbinu yeyote ya kupambana na hali hii hasa kwa kupunguza changamoto na adha mbalimbali nazokutananazo nilizozieleza hapo juu nitashukuru sana.

View attachment 1799771
POLE SANA NDUGU,
MIMI NAPITIA CHANGAMOTO KAMA YAKO, TENA MIMI KUELEWA MPAKA NOONGEE NA MTU FACE TO FACE, NIKIMUANGALIA MDOMONI NA KUHUSIANISHA KILE NACHOKISIKIA, NIMETUMIA ANALOGY HEA6MACHINE ILA HAIJANISAIDIA CHOCHOTE, KIUKWELI NI CHANGAMOTO KUBWA SANA, MIMI NDO NIMEMALIZA CHUO MWAKA JANA, NAWAZA NTAAJILIWA NA NANI? NYUMBANI MAISHA MAGUMU NA MLANGO WA KUTOKEA SIHUONI KABISA,, NDUGU TANGU WW KAMA UMEFIKIA KIWANGO FLANI CHA MAISHA SHUKURU TU, WALA USIJIHISI UPO PEKE YAKO, TUPO WENGI NYUMA YAKO TUNAPITIA HII CHANGAMOTO. AMINI MUNGU ATAKUFIKISHA PALE ALIPOKUPANGIA.
OMBI LANGU KWAKO: KAMA INAWEZEKANA NAOMBA NIJARIBIE HIZO DIGITAL HEARING ULZONAZO MAANA DAKTAR KANIAMBIA NDO LAST OPTION KWANGU. NAOMBA UNISAIDIE NDUGU YANGU NIJARIBIE NIPIME KAMA VITAWEZA KUNISAIDIA ALAFU MAMBO MENGINE YATAFATA MKUU.
PIA KAMA UNAUWEZO NAKUSHAURI NENDA KAFANYIWE COCHLER IMPLANT NDO SURUHISHO KWAKO.
NAKUTAKIA MAJUKUMU MEMA
BY ALLEN WAKALA ALBOGAST
FROM: BUKOBA
 
Ahsante sana, kwa kiasi kikubwa ndio mambo ninayopambana nayo hayo, na kiasi kikubwa yanaonesha matokeo chanya, japo nalazimika kuishi kwenye ulimwengu mwingine kabisa kivyangu vyangu yaani.
Pole sana mkuu, MUNGU atufanyie wepes, mm Nipo MWAKA Wa 4 hivi, naisho kivyanguvyangu tu
 
Jikubali mkuu.
Bora wewe hard hearing, wenzio ni viziwi kabisa but tumejikubali tulivyo maana Allah ana makusudio yake kutufanya hivi.
Karibu katika jamii ya viziwi ujifunze lugha ya alama hutojisikia mpweke maana haupo peke yako.
AMEN BRO🙏🏿🙏🏿🙏🏿 SAME HERE
 
Back
Top Bottom