Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

Na Mimi nataka
 
Duu jamani Hadi huruma
 
Hebu kwenda na kingereza chako huko lione andika Swahili tu
 
I have the same problem. Yani your experience ni yangu 100%

Me ilianza since 2008 mpaka sasa, ni tinnitus. Nime zunguka sana hospital zote kama KCM, MUHIMBILI na nmeenda sana pale hear well clinic upanga nkapewa hearing aids lakini wapi. Tumenunua aina tofauti tofauti tumepoteza mamilioni bure tu.

nimeenda mpaka ujerumani na finland ila wapii, in the end nkaona tunapoteza pesa bure. HAKUNA TIBA YA UHAKIKA MPAKA SASA

Nnachokushauri jifunze kuishi na tatizo lichukulie normal tu kama wenye shida zingine kama macho, kuwa disminder, me ata ukichukia kisa sijakuskia nakuona mjinga tu and that’s not my problem, wewe uliemind ndo una shida. Hili tatzo nmejifunza linachochewa na emotiona pia, ukiwa very stressed inakua much worse.. so jitahidi uwe happy always, jiamini, be smart, make money and enjoy life. Don’t be ashamed with ur problem, kama mtu sielewani nae namwambia kabisa i have hearing problem so ongea namna hii nkuskie.

Find money, status and be smart itakusaidia kama defensive mechanism, mimi watu nawaambia kabisa nitafute kwa text, ukipiga simu sipokei. and YES i hate so much mtu akipiga simu yani nakasirika kabisa and people know that.

Yangu ni hayo mkuu.
 
Umeua mkuu hili Ni baya Sana ukiwa emotional tagged and stressed Ni watu wenye tatzo huwa tunakuwa na hasira Sana....


Umetoa ushauri mzuri sana hili tatzo wajomba halihusiani kabsa na masikio...Ni nervous impulse damage. ..kusinyaa kwa mishipa ya fahamu ya kichwa ....

Mm Sasa napokea simu na naongea na watu fresh sehemu ikiwa tulivu..sihitaji aids mashine Tena..

Relax na kulikubali tatizo tutafute pesa and a like...nalog off...
 

pamojaaa sana kiongozi wangu
 
Jiamini kwamba bado wewe ni wa kipekee,jikubali..chukulia kama ni changamoto ya kawaida tu kama zingine

Sasa unajinyima raha kwa mawazo ya tatizo la kiungo kimoja tu cha mwili

Kuna wakati utafika viungo vyote vya mwili ," vitazimika".

So ...why bother..! [emoji57][emoji57]

Kuwa positive..uzuri hali hii haikulazi kitandani,unaweza fanya shughuli zako vizuri tuu.
Wenye saratani nao watasemaje sasa?
 
USHAURI
Wale wenzangu na Mimi wenye case hii ya usikivu hafifu tuwe makini tusijeumizwa na madaktari humu halafu kupona usipone...

Mganga au Daktari aliyetayari kukutibu asikupige pesa kwanza yaani akutibu kwa makubaliano ya mwisho wa matibabu ndipo kufanyika malipo...

Maana tunafuatwa pm na wengi ..Wengine tumeumiza pesa ndefu Bila mafanikio..

Nalog off
 
Ushauri mzuri Sana huu
 
Polea sana mkuu kumbe tuko wengi hivi na si hapa tu bali kidunia hilo tatizo nadhani kinajulikana na dawa yake hamna kwahiyo tujikubali tu ukizingatia tunapambana sana kwa kutumia nguvu za ziada

Anyway hili tatizo kitaalamu linaitwa "Tinnitus" na categories zake kadha wa kadha

Aisee πŸ€”πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Pole, sana ndugu yangu umejitahid sana kuelezea hali unayopitia ni changamoto sana aisee, lakini Amini siku moja utakuwa sawa tu umepambana sana naomba usiache kusali na kushukuru Mungu anaweza kutenda pale ambapo tunaina tumeshindwa..... Naomba tuwasiliane ndugu yangu
 
Broth Nina tatizo hiloo kama hutojali nicheki tsup 0673739405 tuyaje ge
 
Kakabroh nicheki tsup 0673739405 Nina shida kama yako

 
Pole sana ila yote uliyoyaeleza namimi kwa upande wangu ndio hali niliyonayo mpaka keo hii ila kwa upande wangu kuna muda yanazibuka ghafla nakua ninauwezo wa kusikia kwa ufasaha kabisa yani ni kama tatizo linaisha kabisa ila baada ya kama ya saa ghafla hali inarudi tena ya masikio kupunguza uwezo wa kusikia.

Ila nikiingiza vijiti vya pamba za masikioni nikazisukuma kidogo nasikia vizuri kabisa kwa ufasaha ila nikivitoa tu vile vijiti vya pamba nakua na usikivu hafifu kwakweli hali hii imeshamichosha ila nimeamua kukubaliana na hali japo kuna muda hua inanikosesha mishe zangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…