Ninaomba msaada wa kimawazo au ushauri wa kutatua changamoto ya usikivu mdogo (Hearing loss) au kupunguza adha zake

Pole kwa yote unayopitia.

Kuna mambo ya muhimu kuzingatia.
Tatizo la usikivu ni suala mtambuka, linahusisha wanataaluma wengi, kuanzia bingwa wa masikio/ENT, Audilogist na pia daktari bingwa wa mishipa ya fahamu.

Matatizo haya yanahusisha aina na kiasi chake.

1: Aina hutegemea na sehemu gani ya sikio inahusika.

2: Kiasi hutegemea na madhara husika

Tiba halisi hutegemea na hayo yote hapo juu na wakati mwingine tiba huusisha kuwekewa visaidizi au watu kueleza hali ya ufanisi wa tiba kutokumsaidia mhusika.

Pia, tiba hutegemea uwepo wa teknolojia mbalimbali kuwepo eneo husika.

NB: Ni vyema kuhakikisha tunapata maana ya kile ambacho:

1: Mtaalamu wa afya ameking'amua nini kama tatizo unapokuwa nae. Muda husika unakuwa umelipiwa na ni haki yako kupata taarifa sahihi na elimu sahihi.

2: Nini mtaalamu wa afya anaweza kufanya ili kutatua tatizo.

3: Nini kinaweza kufanyika zaidi ikiwa utaalamu na teknolojia vikiwepo sehemu husika/alternative.
 
POLE SANA NDUGU,
MIMI NAPITIA CHANGAMOTO KAMA YAKO, TENA MIMI KUELEWA MPAKA NOONGEE NA MTU FACE TO FACE, NIKIMUANGALIA MDOMONI NA KUHUSIANISHA KILE NACHOKISIKIA, NIMETUMIA ANALOGY HEA6MACHINE ILA HAIJANISAIDIA CHOCHOTE, KIUKWELI NI CHANGAMOTO KUBWA SANA, MIMI NDO NIMEMALIZA CHUO MWAKA JANA, NAWAZA NTAAJILIWA NA NANI? NYUMBANI MAISHA MAGUMU NA MLANGO WA KUTOKEA SIHUONI KABISA,, NDUGU TANGU WW KAMA UMEFIKIA KIWANGO FLANI CHA MAISHA SHUKURU TU, WALA USIJIHISI UPO PEKE YAKO, TUPO WENGI NYUMA YAKO TUNAPITIA HII CHANGAMOTO. AMINI MUNGU ATAKUFIKISHA PALE ALIPOKUPANGIA.
OMBI LANGU KWAKO: KAMA INAWEZEKANA NAOMBA NIJARIBIE HIZO DIGITAL HEARING ULZONAZO MAANA DAKTAR KANIAMBIA NDO LAST OPTION KWANGU. NAOMBA UNISAIDIE NDUGU YANGU NIJARIBIE NIPIME KAMA VITAWEZA KUNISAIDIA ALAFU MAMBO MENGINE YATAFATA MKUU.
PIA KAMA UNAUWEZO NAKUSHAURI NENDA KAFANYIWE COCHLER IMPLANT NDO SURUHISHO KWAKO.
NAKUTAKIA MAJUKUMU MEMA
BY ALLEN WAKALA ALBOGAST
FROM: BUKOBA
 
Ahsante sana, kwa kiasi kikubwa ndio mambo ninayopambana nayo hayo, na kiasi kikubwa yanaonesha matokeo chanya, japo nalazimika kuishi kwenye ulimwengu mwingine kabisa kivyangu vyangu yaani.
Pole sana mkuu, MUNGU atufanyie wepes, mm Nipo MWAKA Wa 4 hivi, naisho kivyanguvyangu tu
 
Jikubali mkuu.
Bora wewe hard hearing, wenzio ni viziwi kabisa but tumejikubali tulivyo maana Allah ana makusudio yake kutufanya hivi.
Karibu katika jamii ya viziwi ujifunze lugha ya alama hutojisikia mpweke maana haupo peke yako.
AMEN BROπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏπŸ™πŸΏ SAME HERE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…