Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Huu ni uongo.

Kwanza, kinachomata haswa ni index number ya kidato cha nne. Cheti huwa ni nyongeza tu baadae, hapa nazungumzia katika mchakato wa kuomba vyuo, nk.

Lakini pia, ukichoma cheti ama kukipoteza kwa bahati mbaya, utaratibu upo very clear. Omba loss report, andika barua kwenda NECTA, watakutengenezea cheti kingine.

Kudai ulitumia cheti cha mtu kwa sababu chako ulichoma ni upuuzi usio na mantiki.
Mleta uzi ni tapeli.
 
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.
Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu.

Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.
Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.
Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza).
Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini.
Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.
1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu)
Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.
Asanteni.

Hakuna justification yeyote ya mwanamke kujiuza
 
Huu ni uongo.

Kwanza, kinachomata haswa ni index number ya kidato cha nne. Cheti huwa ni nyongeza tu baadae, hapa nazungumzia katika mchakato wa kuomba vyuo, nk.

Lakini pia, ukichoma cheti ama kukipoteza kwa bahati mbaya, utaratibu upo very clear. Omba loss report, andika barua kwenda NECTA, watakutengenezea cheti kingine.

Kudai ulitumia cheti cha mtu kwa sababu chako ulichoma ni upuuzi usio na mantiki.
Ningeweza kuweka hata ushahidi wa hiki ninachosema hapa hadharani, ila kwa kuwa umeshasema mimi ni mpuuzi naona haina haja.
Ila jua tu kuwa nilisomea ualimu kwa kutumia cheti cha form 4 cha mtu na ndio hikohiko nikapanda nacho.
Silazimishi ukubaliane nami ila mimi ndio ninaejua ukweli.
 
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.
Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu.

Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.
Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.
Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza).
Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini.
Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.
1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu)
Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.
Asanteni.

Naweza saidia mdogo wa kusoma kupitia ufadhili fulani, fanya hivi:

1. Sema Shule anayosoma.
2. Kidato na darasa.

Usiseme jina mimi nitamsaidia kupitia Shule!

Hayo mambo ya kujenga sijui mnayakimbiliaga ya nini; hayana maana kabisa Kama una struggle!

Asante!
 
Kwa nini uliacha kujiuza?

Je, ulipata hela za kutosha au ni vipi?

Kwa uamuzi wako wa kuweka kila kitu hapa, ukisema uliwahi kujiuza NA SASA HUTAKI TENA KUJIUZA, umeamua kutafuta kazi.

Huoni kama waajiri wako wanaweza kukusumbua?(Maana past yako inajulikana)

Je huoni kama watu watakutafuta wakiwa na lengo Lao la kificho, wakijaribu kukushawishi kwa hiyo kazi?

Dada, ulikua unajiuza, na kwa bandiko lako hili, muda si mrefu utarudi katika kujiuza hata kama hupendi. Maana hakuna namna, hakuna mwanaume atakutafuta akusaidie kazi tu peke yake behind atakua na interest zake na hiyo ni kwa sababu umewapa past yako.
Sidhani na wala sifikirii kurudi huko.
Niliacha baada ya kuona natumika ndivyo sivyo
 
Huu ni uongo.

Kwanza, kinachomata haswa ni index number ya kidato cha nne. Cheti huwa ni nyongeza tu baadae, hapa nazungumzia katika mchakato wa kuomba vyuo, nk.

Lakini pia, ukichoma cheti ama kukipoteza kwa bahati mbaya, utaratibu upo very clear. Omba loss report, andika barua kwenda NECTA, watakutengenezea cheti kingine.

Kudai ulitumia cheti cha mtu kwa sababu chako ulichoma ni upuuzi usio na mantiki.
hata na mm baada ya kusoma hayo maelezo yake kuhusu chet, nimepata ukakasi.
 
Pole sana dadq,
Huna mtoto?

At 42 jitahidi usipate depression, kuanzia 35-55 usipoangalia depression itakumaliza sababu ni umri wa kusahihisha makosa, ikitokea ukakosea zaidi unaangukia kwenye depression.

Tafuta kazi halali, hata ndogo ya kuingiza kipato ufanye. Ukirudi kwenye kujiuza na umri huo ni hatari kwako.
Asante sana.
Ndio maana nimekiri kuwa sihitaji kurudi tena huko.
Sikubahatika kupata mtoto wala kuolewa.
 
Pole sana dada ALLAH akunusuru.

Hebu anza kufanya yafuatayo

1. Jifunze kutengeneza keki, utaweza kusupply kwenye birthdays, harusi, etc

2. Biashara ya chakula inalipa, tafuta sehemu nzuri yenye watu wengi uanze kupika.

3. Kusanya kuku wa kienyeji huko Morogoro uwe unawaleta Dar kuwauza. Baadae unaweza kuwa unakusanya mbuzi huko mikoa ya jirani na dar unawalera dar unauza

4. Njoo Dar tafuta soko moja utafute meza uwe unauza viazi vya chips etc. Kwa siku unawezankuuza hata gunia

5. Anza kutengeneza vitafunio kama vile maandazi etc, uwe unasambaza ktk maduka kadhaa wanakuuzia

Mtangulize Mungu mbele atakusaidia Insha Allah.
 
Back
Top Bottom