Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Ninapitia msongo mkali wa mawazo baada ya kusimamishwa kazi kisa vyeti feki. Naomba ushauri niweze kujikwamua

Asante sana kipenzi.
Hapana, ni kwamba niliuziwa cheti cha mtu aliyemaliza form 4 nikaenda nacho kusomea ualimu ngazi ya certificate na diploma kwa kutumia jina lake.
Kipindi hiko mimi nilikuwa nimemaliza kidato cha nne miaka kama 3 iliyopita na cheti changu kilichomwa moto na msichana wetu wa kazi.
Hivo nilipanda na jina lake mpaka kufikia ngazi ya diploma (katika kujiendeleza) ndipo nikatumbuliwa hukohuko.
Mmh haya maelezo kuna kitu hakiko sawa.
 
Mmeanza ujinga sasa kutoka Form Iv direct Hadi PGDE? Tena UDSM🙄🙄
tuwekee interval ya Miaka tangu ulivyoanza kusoma mpaka ulipotoka Kazini, Na hivyo vyeti. Sababu yako ya cheti Cha form 4 kuchomwa script yake hazijakaa vizuri. Kama lengo Lilikua ni kujitambulisha kama veteran muuzaji basi umezunguka sana
 
Mmeanza ujinga sasa kutoka Form Iv direct Hadi PGDE? Tena UDSM🙄🙄
tuwekee interval ya Miaka tangu ulivyoanza kusoma mpaka ulipotoka Kazini, na hivyo vyeti
Sababu yako ya cheti Cha form 4 kuchomwa script hazijakaa vizuri. Kama lengo Lilikua ni kujitambulisha kama veteran muuzaji basi umezunguka sana
Muonee hata huruma
 
Habari wana Jf kwa ujumla.
Sina muda mrefu tangu nijiunge na jumuia hii chini ya kaka Max.

Ni hivi, napitia msongo mkali sana wa mawazo yaani nikisema ni mkali namaanisha.

First of all nilikuwa muajiriwa serikalini na likapita suala la vyeti feki hapo nilikuwa natumia cheti cha mtu na kazi ikawa ndio basi.

Sababu nilipoteza wazazi ikabidi ile akiba niliyojiwekea kipindi nafanya kazi niitumie kwa ajili ya kumsomesha mdogo wangu ambae niliachiwa na wazazi pamoja na kununua kiwanja tu. Hali ikazidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi niingie kwenye kazi ya kujiuza.

Nilichokuwa nafanya ni kumuandalia mdogo wangu sare za shule na pesa ya matumizi usiku ili hata kama nitarudi asubuhi au kama sitarudi kabisa basi apate kujiandaa na kwenda shule (shule na nyumbani ni kama km 1 tu) mwenyewe.

Nilifanya hiyo kazi kwa miaka 6, nikapata pesa na kuanza ujenzi wa nyumba yangu ya kuishi pamoja na mdogo wangu.

Shida imeanza tena, nyumba haijakamilika na pesa zote nimemaliza na mdogo wangu mwaka huu anaingia kidato cha 3.
Sitaki tena kurudi kule nilipotoka (kujiuza). Nahitaji mdogo wangu akue bila kujua nafanya nini. Pia nahitaji kumalizia nyumba

Kama kuna mtu ana uhitaji wa mtu wa kufanya kazi naomba nipewe ajira.

1. Nina diploma ya Education niliyoipata pale UDSM kabla sijatumbuliwa.

2. Nina uzoefu katika kulea watoto na pia ninajua sana upishi (nilisomea hotel management kabla sijaenda kusomea ualimu), Umri wangu ni miaka 42 na niko Morogoro.

Asanteni.
UDSM kuna diploma ya Education?
 
Back
Top Bottom