Ninapokumbuka ya Morgan I Tsvangirai nahuzunishwa na ya Upinzani wa kina Lissu na wenzake

KooZito

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2020
Posts
397
Reaction score
1,378
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

Usiku wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe.

Alikuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake ili hatimaye wengine waje kuishi maisha ya raha na amani hata kama yeye hatokuwepo duniani. Namzungumzia Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change, MDC aliyefariki Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo.

Morgan alikuwa ni mwiba mkali mbele ya macho ya dikteta Robert Mugabe tangu akiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hadi alipoanzisha MDC kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa kifashisti ya ZANU-PF ya Mugabe iliyojaa dhulma, ufisadi, kujuana, utekaji, utesaji kwa waliomkosoa dikteta Mugabe na ushetani mwingine kama ilivyo kwa Serikali ya CCM.

Upambanaji wa Morgan kwa utawala wa ZANU-PF ya dikteta Mugabe umesheheni simulizi za kusisimua sana. Kwamba hata alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kama hatua ya kumtaka "astaafu" upambanaji bado hakukubali kusaliti wazalendo. Morgan hakuwa mwoga na kamwe hakushikwa na hofu ya kuuawa na Mugabe. Na hiyo ilimfanya asikimbie nchi yake kwenda Uropa. Alikuwa tayari kufa nchini Zimbabwe kuwapigania wananchi waliokuwa wakionewa na Serikali katili ya Mugabe.

Baada ya Mugabe kuvifungia magazeti yaliyokosoa Serikali yake, aliviamuru yaliyosalia kumtangaza Morgan kama kibaraka wa wazungu asiye na nia njema na Zimbabwe lakini bado Tsvangirai hakukata tamaa.

Sina kumbukumbu ni mara ngapi Morgan alilazwa rumande na kupigwa na Wana usalama vibaraka wa Mugabe maana picha za Morgan zikimuonesha akichuruzika damu zimetapakaa katika maktaba mbalimbali duniani.

Mugabe alijaribu hata kumhonga vyeo na pengine ofa ya vyeo na fursa za biashara lakini dunia imeandika historia kuwa alivikataa kuwapambania Wazimbabwe.

Ukweli uliokodoa macho ni kwamba mchango wa Morgan ni mkubwa sana katika kumwondoa Mugabe madarakani. Ndiyo, maana jiulize wale makamanda wa Mugabe walipata wapi ujasiri wa kumwambia "bosi" wao aondoke ofisini? Wale vijana wa "UVCCM" wa Zanu-Pf walipata wapi ujasiri wa kuunga mkono maandamano ya kumng'oa dikteta Mugabe madarakani? Ukweli ni mbegu ya ujasiri alioupanda Morgan kwa wananchi wa Zimbabwe.

Hata Rais Mnangagwa aliingiwa na woga hivyo kukimbilia ughaibuni baada ya kubaini kukamilika kwa mpango wa kumuua uliopangwa na mke wa Mugabe, Grace lakini Morgan alisalia Zimbabwe kupanda mbegu ya ujasiri na akafanikiwa.

Nikikumbuka haya ya Morgan nasononeshwa na hali ya Upinzani Tanzania. Tundu Lissu amenukuliwa akisema, "Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko kukiondoa CCM madarakani". Najiuliza ni lini Lissu amepanda mbegu ya ujasiri wa kukiondoa CCM ya Magufuli madarakani? Ni lini Lissu amepanda mbegu hiyo kwa vyombo vya usalama vinavyokilinda CCM madarakani? Kwa nini Lissu aliahidi kutupeleka barabarani akaishia kujipeleka ubalozini kwa woga na hofu ya kuuawa na vyombo vya usalama alivyodai?

Unajiuliza hivi Tanzania nani hasa ni kinara na alama ya Upinzani aliyetayari "kufa" kwa ajili ya umma mpana. Kenya wanaye Raila Odinga, Uganda wanaye Kiiza Besigye na Bobi Wine, Afrika Kusini wanaye Julius Malema nakadhalika. Tanzania tunaye nani? Mdee, Sugu, Lema, Heche, Mbowe, Zitto, Membe, Rungwe, au nani?

Kwa mbali alionekana Lissu angechukua nafasi hiyo lakini naye amejawa hofu na woga kana kwamba katika Afrika demokrasia, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, Katiba bora nakadhalika ni Mambo ya kuletwa na watawala kama bakuli la dengu mezani.

Wanajisahaulisha kuwa Mambo hayo hupiganiwa katika majukwaa ya siasa bila kujali maslahi binafsi na matumbo. Ni vita inayogharimu damu, jasho na mateso. Morgan hakufikiri wala kusubiri kuwa mageuzi yangeletwa na dikteta Mugabe. Alipambana. Hakuogopa "kushughulikiwa" kama wapinzani wetu.

Wakati Lema akitimkia Kenya na familia yake akidai nayo inaweza kuumizwa, Morgan aliwahi kuchomewa nyumba na kila kitu ndani lakini alipopata nafasi ya kuongea na media akisema, "nimepoteza kila kitu ndani ya nyumba lakini sijapoteza chochote kwa Wazimbabwe maana ukombozi uko mlangoni."

Leo Wazimbabwe wanafurahia maisha yasiyo na vituko vya Mugabe na mkewe Grace lakini jasiri Morgan ametangulia kaburini. Huo ndio Upinzani wa kweli. Kupanda mbegu ya ujasiri si lelemama. Linahitaji kujitoa mhanga si kukimbia. Tumebaki na wapinzani wa mitandaoni. Inasononesha sana!!!

Nawatakia mapumziko mema.
 
Lissu hashindani na risasi, anashindana kuikomboa nchi toka kwa watawala wasiojali utu wa Mtanzania, wasiojua kufuata sheria za nchi, hivyo kuendelea kukaa Tanzania asubiri kifo nao ungekuwa ni ujinga, kukimbia sio ujinga ukiwa vitani, nayo ni mbinu ya kivita.

Wapo wanasiasa wengi waliozikimbia nchi zao wakiwa kwenye harakati za mapambano na bado dunia inawatambua kwa uimara wao mpaka leo, hivyo Lissu sio wa kwanza kutafuta hifadhi nje kwa ajili ya usalama wake.

Labda nikuulize ewe mpenda mabadiliko, siku ya maandamano ulijitokeza barabarani au uliogopa virungu vya Mambosasa? Ni upi mchango wako kwenye kuikomboa demokrasia ya nchi yetu? kuna msemo usemao; "changes begins with you"

Nikushauri badala ya kumlaumu Lissu, anza na wewe kuwa chachu ya hayo mabadiliko unayoyataka, sio unalala nyumbani unasubiri uletewe mabadiliko ukiwa kitandani.
 
Lissu alishambuliwa kwa risasi zaidi ya kumi na sita, amejiuguza Ubelgiji miaka mitatu, amerudi kugombea urais bahati mbaya uchaguzi haukuwa huru na haki yalikuwa ni maigizo, baada ya kupata taarifa bado anawindwa na watesi wake akaamua kurudi ughaibuni akaendeleze mapambano akiwa huko...
Kwa bahati mbaya sikuwepo nchini, ningekuwa mbele kabisa. Sina woga wala hofu ya risasi kupigania demokrasia
 
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

USIKU wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe...
Hata Robert Mugabe alipigania haki na uhuru wa Zimbabwe hadi akasweka jela, Mugabe alikuja kubadirika baada ya serikali ya Uingereza kumgeuka juu ya fidia ya mashamba ya wazungu. Mambo mengine yaliochangia kifo cha mke wa mwanzo na umri wake.
 
Mtu aache kula bure na kulala bure Brussels wakati huku anajua hawezi kutoboa kwasababu Watanzania wanampenda sana JPM.

Wewe mwenyewe hauoni kuwa kwa kazi inayofanywa na awamu ya 5 MAENDELEO YA KASI huyo Lisu ni kama alikuwa anapoteza Muda tuu.
 
Siasa za Tanzania ni ngumu sana, zimejaa chuki, visasi, ubabe wa kijinga, uongo nk

Kwani Huyo Morgan nayeye alipigwa risasi 16?
 
...utawala wa kifashisti ya ZANU-PF ya Mugabe iliyojaa dhulma, ufisadi, kujuana, utekaji, utesaji kwa waliomkosoa dikteta Mugabe na ushetani mwingine kama ilivyo kwa Serikali ya CCM.
Kwa nini vyama kongwe vilivyoleta UKOMBOZi wa mwanzo vinafanana kwa matendo?!!!
 
Usimlinganisha Morgan na hawa wachumia tumbo.
Viongozi na wanachama wote wa CCM mlikuwa wafuasi wa Mugabe na kundi lake mkitetea udikiteta wake na kuufanya ndo uzalendo wa kuigwa Afrika! Mlimwita Morgan Tvangrai gaidi, kibaraka na majina lukuki ya kashfa.

Leo mnapomsifu Morgan ni Unafiki au Uzuzu mliojilimbikizia hapo Lumumba? Kama mlimwita Morgan majina ya ovyo kisa anampinga dikteta mwenzenu, tuwashangaeje mnapowaita wapinzani nchini mwenu majina ya ajabu?
 
Nime kuja kugundua kitu kuna mahusiano makubwa sana kati ya CCM na ujinga, simtukani mtu ila huo ndio ukweli tujitahidi sana kuwapa ndugu zetu somo Folded hands. madhara ya kukubali kumtegemea mtu kua kinga yako ndio hayo nilazima uwe kama zombie kila kitu unashabikia tuwasaidie wenzetu.
 
Lissu anatakiwa awatoe wapinzani huko mitandaoni na kuwaleta huku mitaani,upinzani uliyopo huku mitaani ni tofauti na mitandaoni.
 
Viongozi na wanachama wote wa CCM mlikuwa wafuasi wa Mugabe na kundi lake mkitetea udikiteta wake na kuufanya ndo uzalendo wa kuigwa Afrika! Mlimwita Morgan Tvangrai gaidi, kibaraka na majina lukuki ya kashfa. Leo mnapomsifu Morgan ni Unafiki au Uzuzu mliojilimbikizia hapo Lumumba? Kama mlimwita Morgan majina ya ovyo kisa anampinga dikteta mwenzenu, tuwashangaeje mnapowaita wapinzani nchini mwenu majina ya ajabu?

Hii mbeleko ya ukoka hata Slaa anavikwa na wanaccm siku hizi kuwa alikuwa mpinzani Bora. Anavikwa kilemba cha ukoka maana sasa hivi hawakosoi ccm.
 
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

USIKU wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe...
Wewe jamaa ukitaka kuwa credible lazima useme ukweli, na msema ukweli Ni mpenzi wa Mungu. Au nasema uongo ndugu zangu? Wakati Mnangagwa anaondoka kukimbilia Afrika Kusini Tsvangrai alikuwa hai ?
 
Nawasalimu wanabodi wa JamiiForums

Usiku wa kuamkia leo akili yangu ilinigomea kupata usingizi na hivyo kukaa macho almost the whole night. Nilikuwa nikimkumbuka mtu jasiri na mpambanaji wa kutetea haki za binadamu na ustawi wa demokrasia nchini Zimbabwe.

Alikuwa ni mtu aliyejitolea maisha yake ili hatimaye wengine waje kuishi maisha ya raha na amani hata kama yeye hatokuwepo duniani. Namzungumzia Morgan Tsvangirai wa chama cha Movement for Democratic Change, MDC aliyefariki Afrika Kusini miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa saratani ya utumbo.

Morgan alikuwa ni mwiba mkali mbele ya macho ya dikteta Robert Mugabe tangu akiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hadi alipoanzisha MDC kuendeleza mapambano dhidi ya utawala wa kifashisti ya ZANU-PF ya Mugabe iliyojaa dhulma, ufisadi, kujuana, utekaji, utesaji kwa waliomkosoa dikteta Mugabe na ushetani mwingine kama ilivyo kwa Serikali ya CCM.

Upambanaji wa Morgan kwa utawala wa ZANU-PF ya dikteta Mugabe umesheheni simulizi za kusisimua sana. Kwamba hata alipoteuliwa kuwa Waziri Mkuu kama hatua ya kumtaka "astaafu" upambanaji bado hakukubali kusaliti wazalendo. Morgan hakuwa mwoga na kamwe hakushikwa na hofu ya kuuawa na Mugabe. Na hiyo ilimfanya asikimbie nchi yake kwenda Uropa. Alikuwa tayari kufa nchini Zimbabwe kuwapigania wananchi waliokuwa wakionewa na Serikali katili ya Mugabe.

Baada ya Mugabe kuvifungia magazeti yaliyokosoa Serikali yake, aliviamuru yaliyosalia kumtangaza Morgan kama kibaraka wa wazungu asiye na nia njema na Zimbabwe lakini bado Tsvangirai hakukata tamaa.

Sina kumbukumbu ni mara ngapi Morgan alilazwa rumande na kupigwa na Wana usalama vibaraka wa Mugabe maana picha za Morgan zikimuonesha akichuruzika damu zimetapakaa katika maktaba mbalimbali duniani.

Mugabe alijaribu hata kumhonga vyeo na pengine ofa ya vyeo na fursa za biashara lakini dunia imeandika historia kuwa alivikataa kuwapambania Wazimbabwe.

Ukweli uliokodoa macho ni kwamba mchango wa Morgan ni mkubwa sana katika kumwondoa Mugabe madarakani. Ndiyo, maana jiulize wale makamanda wa Mugabe walipata wapi ujasiri wa kumwambia "bosi" wao aondoke ofisini? Wale vijana wa "UVCCM" wa Zanu-Pf walipata wapi ujasiri wa kuunga mkono maandamano ya kumng'oa dikteta Mugabe madarakani? Ukweli ni mbegu ya ujasiri alioupanda Morgan kwa wananchi wa Zimbabwe.

Hata Rais Mnangagwa aliingiwa na woga hivyo kukimbilia ughaibuni baada ya kubaini kukamilika kwa mpango wa kumuua uliopangwa na mke wa Mugabe, Grace lakini Morgan alisalia Zimbabwe kupanda mbegu ya ujasiri na akafanikiwa.

Nikikumbuka haya ya Morgan nasononeshwa na hali ya Upinzani Tanzania. Tundu Lissu amenukuliwa akisema, "Watanzania hawajawa tayari kwa mabadiliko kukiondoa CCM madarakani". Najiuliza ni lini Lissu amepanda mbegu ya ujasiri wa kukiondoa CCM ya Magufuli madarakani? Ni lini Lissu amepanda mbegu hiyo kwa vyombo vya usalama vinavyokilinda CCM madarakani? Kwa nini Lissu aliahidi kutupeleka barabarani akaishia kujipeleka ubalozini kwa woga na hofu ya kuuawa na vyombo vya usalama alivyodai?

Unajiuliza hivi Tanzania nani hasa ni kinara na alama ya Upinzani aliyetayari "kufa" kwa ajili ya umma mpana. Kenya wanaye Raila Odinga, Uganda wanaye Kiiza Besigye na Bobi Wine, Afrika Kusini wanaye Julius Malema nakadhalika. Tanzania tunaye nani? Mdee, Sugu, Lema, Heche, Mbowe, Zitto, Membe, Rungwe, au nani?

Kwa mbali alionekana Lissu angechukua nafasi hiyo lakini naye amejawa hofu na woga kana kwamba katika Afrika demokrasia, haki za binadamu, uhuru wa vyombo vya habari, uhuru wa kujieleza, Katiba bora nakadhalika ni Mambo ya kuletwa na watawala kama bakuli la dengu mezani.

Wanajisahaulisha kuwa Mambo hayo hupiganiwa katika majukwaa ya siasa bila kujali maslahi binafsi na matumbo. Ni vita inayogharimu damu, jasho na mateso. Morgan hakufikiri wala kusubiri kuwa mageuzi yangeletwa na dikteta Mugabe. Alipambana. Hakuogopa "kushughulikiwa" kama wapinzani wetu.

Wakati Lema akitimkia Kenya na familia yake akidai nayo inaweza kuumizwa, Morgan aliwahi kuchomewa nyumba na kila kitu ndani lakini alipopata nafasi ya kuongea na media akisema, "nimepoteza kila kitu ndani ya nyumba lakini sijapoteza chochote kwa Wazimbabwe maana ukombozi uko mlangoni."

Leo Wazimbabwe wanafurahia maisha yasiyo na vituko vya Mugabe na mkewe Grace lakini jasiri Morgan ametangulia kaburini. Huo ndio Upinzani wa kweli. Kupanda mbegu ya ujasiri si lelemama. Linahitaji kujitoa mhanga si kukimbia. Tumebaki na wapinzani wa mitandaoni. Inasononesha sana!!!

Nawatakia mapumziko mema.
Wewe keyboard hero mbona huwi Morgan wa Tanzania. Maneno mengi. Unasubir Lissu afe ndio uje umuandike alikua hero wako.

Kwani sisi hatupendi wewe uwe hero wetu? Tunapenda
Ukombozi gani Zimbabwe imepata hata Mugabe alivyoondolewa ushenzi tu unaendelea.

Hakuna cha chama tawala wala upinzani wote wachumia tumbo tu mamaaaaxcv zao. Familia zao ziishi vizuri tu ndio lengo. Unataka useme Lissu ni Chadema wakikamata nchi tutaishi kama peponi? Pathetic. Tena inaweza kua mbaya kuliko hata ubaya tunaouona kwa ccm.

Stop being keyboard heros that's ma main message
 
Kipindi unatafakari hili jiulize swali ni mpinzani gani ameponea tundu la kifo kwa risasi zaidi ya kumi mwilini na pia hebu nafasi ya Lissu Kazi wewe jiulize je kwa risasi zile ningekuwa mimi ningeendelea kukomaa nchini? na Zaid usikariri mambo kuna Vita ya ndani na kuna Vita ya ndani pia hao wote Mugabe, Samola n.k walikuwa nje ya nchi zao kabla ya kurudi kukomboa nchi

Back
Top Bottom