Ninaposema Mwafrika kapunjwa akili na Mungu kwa makusudi kabisa muwe mnaelewa. Rejea ajali ya ndege Bukoba 06/11/2022

Mafunzo ya jeshi yanafundisha ushirikiano na upendo miongoni mwa wanajeshi vitani,hakuna kumuacha mwenzio nyuma
Tunawategemea pia wawe msaada kwenye majanga. Maana tunaamini wanao uwezo wa ziada kutokana na mafunzo yao.
 
Watu wanalaumu tuu.
Kama wao ni Bora nini kinawazuia kumtoa huyu aliyekuwepo?
Ni kwamba tumeshakubaliana na Hali iliyopo
Waafrika hatuna akili tuseme tu ukweli. Maana hata rais angekuwa ametoka upande ule mwingine nakwambia hali ingekuwa hivi hivi .
Kuna mambo ambayo hatuyapi kipaumbele.
Siku tukiungana kupinga mambo ya kijinga kama haya bila kujali wewe ni wa chama gani ndo siku ambayo labda tutaweza kufanya viongozi wetu wakashtuka.
 
Inahitaji muda kudili na vitu Kama hivyo,siyo automatic ikitokea ajali jeshi lishajua na limefika
Tunahitaji muda gani mkuu?
Ni miaka mingapi imepita tangu itokee ajali ya MV bukoba na ile nyingine ya Zanzibar?
 

Tatizo la Waafrika ni Ubinafsi, hatupendani. Hatuna Upendo.
Sio tuu Kwa ngazi ya taifa Bali hata ngazi ya Familia.

Wewe angalia familia nyingi mahusiano ya Baba na Mama jinsi yalivyo, msingi wake Mkuu mi ubinafsi.
Nadra Sana ukute familia zenye upendo wa kweli.

Lazima tujenge upendo wa kweli ili tuwe na AKILI.
Bila upendo mtu hawezi kuwa na akili NJEMA
 
kwenye maigizo hatujambo kabisa ngoja litokee kweli uone, mara ndege inavutwa na kamba na wananchi mara wanaotaka kuokoa watu wanakatazwa yaani kuna matatizo mengi sana hasa katika mifumo ya ubongo
Ifike mahali wanajeshi wetu waonyeshe kwa vitendo zile mbwembwe zao wanazotuonyesha kwenye sherehe za kitaifa.
Wanatuaminisha wapo vizuri kumbe in reality hakuna wanaloweza.

Tuendelee tu kuwa waoga kwa kisingizio cha amani lakini ukweli ni kwamba siku tunavamiwa na jeshi la nchi nyingine tunaweza tukateketea kama kuku.
 
Tunahitaji muda gani mkuu?
Ni miaka mingapi imepita tangu itokee ajali ya MV bukoba na ile nyingine ya Zanzibar?
Namaanisha muda wa ku-react,ni lazima tukubali kwamba nchi masikini,haiwezi kuwa na rasilimali zote hizo..ni ngumu
 
Namaanisha muda wa ku-react,ni lazima tukubali kwamba nchi masikini,haiwezi kuwa na rasilimali zote hizo..ni ngumu
Umasikini wa kukosa hata rescue boat moja hapo uwanjani? Kweli mkuu?

Mbona mambo mengi makubwa tunayakamilisha kwa pesa nyingi?

Ndege tumenunua na miradi mingine mingi tumeweza. Kwanini tushindwe kuwekeza kwenye majanga?

Na hiyo SGR ikikamilika na kuanza kazi Mungu aepushe mbali isilete majanga.
 
Dah acha tu tena hapo ndege imeanguka karibu na nchi kavu tumepoteza watu 19

What if ingedondoka kati kati ya ziwa kwenye kina kirefu na kuzama kabisa tungepoteza wangapi
 
Rescue facilities siyo boti tu...na ukitaka kuweka kila sehemu ni ghali kwetu sisi,siami kwamba hakuna patrol boats Viktoria..lakini moja itasaidia nini!?
 
Na huu uzazi usio wa mpango ndio unatuharibia kabisa.
 
Rescue facilities siyo boti tu...na ukitaka kuweka kila sehemu ni ghali kwetu sisi,siami kwamba hakuna patrol boats Viktoria..lakini moja itasaidia nini!?
Nimesema moja kutoa mfano.
Unakuwaje na rescue facilities kando ya ziwa bila boat kuwepo?
Utaendaje kuokoa katikati ya maji? Au ndo tutatumia boats za wavuvi?

Tusijifanye shingo ngumu..tunahitaji rescue facilities zinazoeleweka na zinazofanya kazi inayoonekana, kusingia gharama ni siasa tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…