Mimi mwenyewe nilimshangaa Waziri Mkuu kuanza kutoa majibu ya ajali ya ndege wakati watu hawajaokolewa. Anasema kwanini ndege imeanguka kama vile ilikuwa inapata, hakujua kama mbele ya kichwa cha ndege kimekatika. Police, Zimamoto na jeshi wamekaa pembeni wanashangaa, baada ya kufanya kazi zao za Kutoa Usalama na uokozi baada ya kuwajibika, wamewaachia wavuvi wanaojua kuvua samaki wafanye kazi za kiuokozi.
Sasa hivi walinda Usalama karibia wote wanachojua ni kufika eneo la ajali na kukaa pembeni huku wakipiga picha na kutumiana, halafu wanawaachia wananchi ndio wafanye kila kitu. Na hili tatizo ni la awamu zote za uongozi wa nchi hii.