Ninaposema Mwafrika kapunjwa akili na Mungu kwa makusudi kabisa muwe mnaelewa. Rejea ajali ya ndege Bukoba 06/11/2022

Ninaposema Mwafrika kapunjwa akili na Mungu kwa makusudi kabisa muwe mnaelewa. Rejea ajali ya ndege Bukoba 06/11/2022

Hii ajali ukiangalia kwa upana na marefu yake. Ni ajali ya kukosa uwajibikaji. Yani tumerudi kule tumetoka. Jiulize angekuwa hai Mzee Magu.... End
Magu angefanya nini sasa ajali imeshatokea? Tuache siasa za kukatwa vichwa, maana hata yeye anahusika kwenye huu udhaifu. Alipokuwa hai alifanya nini kuboresha jeshi la ulozi?
 
Habari

Mimi nitazungumzia vitu vichache tu kati ya vingi vilivyojitokeza jana ambavyo vinaonyesha ufinyu wa akili wa viongozi wetu ambao ndio wanawakilisha uhalisia wa wananchi.

1. Ziwa Victoria pamoja na ukubwa wake na umuhimu wake kiuchumi serikali haijaweka boti angalau 4 za dharura kwaajili ya kufanya uokoaji na dharura.

2. Kuajiri kwa uchache Askari na maafisa wa jeshi la zimamoto na uokoaji pamoja na kuwapa vitendea kazi vichache . Jeshi la zimamoto na uokoaji lina watumishi wachache sana na vitendea kazi pia vichache. Hakuna KITUO CHA jeshi la zimamoto na uokoaji kando ya ziwa ili kudeal na dharura za ziwani.

3. Viongozi haraka wamekimbilia kutoa majibu ya sababu ya ajali ile ndani ya masaa machache ili kulinda ugali wao. Ni wazi Mwafrika kakosa utu na ni mbinafsi asiyekubali kuachia nafasi.

Maelfu wanavushwa na vivuko hapa Tanzania kila siku huku pembeni kuna kiboti kidogo cha uokoaji kinachoweza kuokoa watu 10-20 huku kivuko kina maelfu ya abiria. Hili nalo muende mkalitizame. Na ajabu zaidi kiboti hicho kidogo cha uokoaji kimepark pembeni hakina hata habari.
Ufanisi katika nchi hizi utafikiwa siku siasa itatenganishwa na taaluma. Mv bukoba ilitobolewa kwa maagizo ya wanasiasa, ambao hata hawakujua kwa nini ilikuwa inaelea badala ya kuzama.
 
Mimi lawama zote nawarushia CCM maana ndiyo Serikali inayoongoza nchi.
Serikali ya CCM inaona ma Toyota VX V8 ni muhimu kuliko uhai wa mwananchi.

Kiongozi wa CCM anakurupuka na matamko ya kisiasa, aache watu wa plane crash investigation wafanye kazi yao.

Hii nchi msishangae kusikia Black box imeibiwa ili tu kufanya uchunguzi wa kitaalamu usifanyike kumlinda PM na kauli yake asije akaumbuka.
Oh! Umenikumbusha kuibiwa kwa documents za mtaalamu wa Scotland yard kabla hajakabidhi uchunguzi wa moto ulioteketeza watoto Shauritanga!
 
...Na Ajali Ile ya Meli pale Mwanza Miaka Michache nyuma inaelekea haikufundisha lolote licha ya Matamshi Kadhaa ya Kisiasa yalitolewa wakati ule!!
Mwanasiasa kujifunza hana huo muda, yeye anawaza uchaguzi tu na familia yake.
 
Back
Top Bottom