Ninapotaka kununua ardhi kutoka kwa mtu ni vitu gani vya msingi kuzingatia?

Ninapotaka kununua ardhi kutoka kwa mtu ni vitu gani vya msingi kuzingatia?

Kwa mkoa wa Dar es Salaam
1. Iwe imepimwa na ujue plot number na block number/name
2. Iwe ina hati ya wizara ya ardhi (Rais).
3. Isiwe na migogoro wowote uliosajiliwa.
4. Mmiliki awe Tayari kukupa nakala ya kitambulisho cha taifa/passport.
 
Wakuu naomba msaada nimepata eneo nahitaji kununua ila Kwa mtu.

Naomba vitu vya kuzingatia kuokota pesa
Kama kina Hati basi akupe ukafanye verification kwenye ofisi ya Kamishna wa Ardhi ujiridhishe kama ni chake kweli pia kisije kikawa kina dhamana Benki. Pia fanya verification kwenye Serikali za Mitaa na hizo verifications fanya kwa maandishi siyo kwa mdomo tu.
 
Wakuu naomba msaada nimepata eneo nahitaji kununua ila Kwa mtu.

Naomba vitu vya kuzingatia kuokoa pesa
Hapa ni baadhi ya mambo ya kuzingatia:

1. Uhalali wa Hati Miliki: Hakikisha kwamba mtu anayekuuzia ardhi ana hati miliki halali ya ardhi hiyo. Ni muhimu kupata nakala ya hati hiyo na kuangalia kama inavyokubaliana na kanuni za serikali. Pia, unaweza kwenda katika ofisi ya ardhi ya mkoa ili kuthibitisha uhalali wake.

2. Historia ya Umiliki: Fanya uchunguzi wa kina kuhusu historia ya ardhi hiyo. Wakati mwingine ardhi inaweza kuwa na migogoro ya umiliki. Zungumza na majirani au watu wa eneo hilo ili kupata taarifa za awali kuhusu umiliki wa ardhi hiyo.

3. Migogoro ya Ardhi: Hakikisha ardhi hiyo haina mgogoro wa kisheria au wa kijamii. Tumia muda kuchunguza kama kuna kesi za ardhi mahakamani zinazohusisha ardhi unayotarajia kununua.

4. Mamlaka za Serikali za Mitaa: Wasiliana na ofisi ya serikali za mitaa au kijiji ili kuhakikisha kuwa ardhi hiyo inauzwa kihalali na hakuna tatizo lolote na mamlaka za eneo husika.

5. Mipaka ya Ardhi: Hakikisha mipaka ya ardhi imewekwa wazi na kupimwa na mtaalamu wa ardhi (surveyor) ili kuzuia migogoro ya baadaye kuhusu mipaka.

6. Mkataba wa Mauzo: Fanya makubaliano ya maandishi yanayohusisha mwanasheria ili kuhakikisha kuwa unapata kinga kisheria kwa makubaliano yenu. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa kuna rekodi sahihi za mauzo.

7. Ulipaji wa Kodi: Thibitisha kama ardhi hiyo imekamilisha malipo yote ya kodi ya ardhi, ikiwa ni pamoja na kodi za zamani kama zipo. Hii itakusaidia kuepuka madeni ambayo unaweza kurithi.

8. Matumizi ya Ardhi: Chunguza matumizi yaliyopangwa ya ardhi hiyo. Ardhi za kilimo, makazi, na biashara zinaweza kuwa na matumizi tofauti yaliyowekwa na serikali. Hakikisha ardhi hiyo inalingana na matumizi yako yaliyokusudiwa.

Ushauri wa kisheria na kufanya utafiti wa kina kuhusu ardhi itakayohusishwa kutakusaidia kufanya maamuzi salama.

Na mambo mengine ya msingi wataongezea watu hapa.
 
Wakuu naomba msaada nimepata eneo nahitaji kununua ila Kwa mtu.

Naomba vitu vya kuzingatia kuokoa pesa
Angalia vizuri km kuna uwepo wa kaburi kaburi haliuzwi wenye kaburi lao watakuja kukuletea mgogoro kwamba hio ardhi yenye kaburi ilikua haiuzwi kwa hio umepigwa
 
Niko morogoro
Kobello
Unachotakiwa kujua ni aina ya umiliki.
Nenda kwenye eneo na surveyor akapate coordinates za Hilo eneo.

Akishamaliza kupima, kabla ya kuondoka muombe akutumie coordinates hapo hapo kwenye simu yako. Zitakuw kama excel file.

Ataangalia kama eneo lipo kwenye Town Plan Drawing (TP Drawing). Na kama lina approved Survey Plan.
Ukiwa vyote vipo basi zingatia post uliyo-quote.

Kama havipo, uangalie mfumi wa Serikali za mitaa kama ni Manispaa, miji mdogo au wilaya ili ujue tarafibu za umiliki na uuzaji.
Kama ni chini ya Manispaa na hamna mchoro Wala upimaji, achana nalo Hilo eneo, halifai.
 
Je taratibu zipi hufuatwa katika kubadilisha hati
Na huchukua MDA gani Hadi kukamilisha hatua hiyo
 
Unachotakiwa kujua ni aina ya umiliki.
Nenda kwenye eneo na surveyor akapate coordinates za Hilo eneo.

Akishamaliza kupima, kabla ya kuondoka muombe akutumie coordinates hapo hapo kwenye simu yako. Zitakuw kama excel file.

Ataangalia kama eneo lipo kwenye Town Plan Drawing (TP Drawing). Na kama lina approved Survey Plan.
Ukiwa vyote vipo basi zingatia post uliyo-quote.

Kama havipo, uangalie mfumi wa Serikali za mitaa kama ni Manispaa, miji mdogo au wilaya ili ujue tarafibu za umiliki na uuzaji.
Kama ni chini ya Manispaa na hamna mchoro Wala upimaji, achana nalo Hilo eneo, halifai.
Kuna maeneo huku nimepata taarifa kuwa yalipimwa na kugawiwa wananchi miaka mitano iliyopita na Kwa walivyodai maeneo yapo chini ya uongozi wa eneo ni maeneo mapya Kwa maana hiyo.
Ndiyo maana nimekuja hapa Kwa great thinkers kuchukuwa taarifa za MSINGI kabla sijaamua.
Na tumeafikiana tuuziane jumapili
Hii ni sahihi kweli kiofisi za serikali?
 
Pitia majirani kwa utaratibu kabisa waulize...vp hilo eneo lina shida gani....katika majirani wote lazima mbea atakuepo tu na litamtoka neno...
Kama wakikwambia hakuna shida nunua...
 
1,Angalia ubora wa kiwanja

2,Chunguza kama kina migogoro

3, fahamu ukomo wa kiwanja

4, chunguza kama kina nyaraka zote sahihi ikiwemo hati nk

5, mthibitishe anayetaka kukuuzia kiwanja kama ni chake kwa majirani wa eneo hilo na mjumbe wa eneo hilo.

6, wakati mnakabidhiana kiwanja uwe na mashahidi wa kutosha wakiwemo majirani na wajumbe wa maeneo hayo kama mashaidi

7, Wakati mnakabidhiana jitahidi uende ana cameraman kwaajili ya kuchukua video za matukio yote na kuchukua sura za wote waliikuwepo wasije waka kugeuka baadae.

9, hao mashahidi wapooze hata kwa ten ten, hao wajumbe na majirani kwa kuwakusanya kwenye shughuli yako.

10, hapo sasa kiwanja kinakuwa halali kwako
 
Back
Top Bottom