Ninapotaka kununua ardhi kutoka kwa mtu ni vitu gani vya msingi kuzingatia?

1,Angalia ubora wa kiwanja

2,Chunguza kama kina migogoro

3, fahamu ukomo wa kiwanja

4, chunguza kama kina nyaraka zote sahihi ikiwemo hati nk

5, mthibitishe anayetaka kukuuzia kiwanja kama ni chake kwa majirani wa eneo hilo na mjumbe wa eneo hilo.

6, wakati mnakabidhiana kiwanja uwe na mashahidi wa kutosha wakiwemo majirani na wajumbe wa maeneo hayo kama mashaidi

7, Wakati mnakabidhiana jitahidi uende ana cameraman kwaajili ya kuchukua video za matukio yote na kuchukua sura za wote waliikuwepo wasije waka kugeuka baadae.

9, hao mashahidi wapooze hata kwa ten ten, hao wajumbe na majirani kwa kuwakusanya kwenye shughuli yako.

10, hapo sasa kiwanja kinakuwa halali kwako
Ur a Genius Indeed.
 
Kuna maeneo huku nimepata taarifa kuwa yalipimwa na kugawiwa wananchi miaka mitano iliyopita na Kwa walivyodai maeneo yapo chini ya uongozi wa eneo ni maeneo mapya Kwa maana hiyo.
Ndiyo maana nimekuja hapa Kwa great thinkers kuchukuwa taarifa za MSINGI kabla sijaamua.
Na tumeafikiana tuuziane jumapili
Hii ni sahihi kweli kiofisi za serikali?
Kama eneo lilipimwa na kugawiwa watu, basi lazima uione hati na ufuatilie kama nilivyokwambia hapo juu.
1. Plot na block number.
2. Perform search, not incumbered.
3. Linganisha ID na muuzaji.

Labda neno kupima sijui unalitumiaje ila usinunue ardhi isiyopimwa ambayo IPO chini ya Manispaa.
 
Wakuu naomba msaada nimepata eneo nahitaji kununua ila Kwa mtu.

Naomba vitu vya kuzingatia kuokoa pesa
Hakikisha:
1. hakuna mgogoro wa kifamilia juu ya eneo hilo
2. kwamba muuzaji ni mmiliki halali
3. serkali ya mtaa inahusishwa
4. mauzo yawe wazi na watu wajue
5. unapata nyaraka za mauzo
6. eneo sio la serkali au taasisi
7. sio bonde la mafuriko au mkondo wa maji
8. halitaliwa na mipango miji
10. hakuna mgogoro juu ya eneo hilo
11. eneo halijauzwa kwa mwingine
12. muuzaji unamfahamu na makazi yake ya kudumu
13. mamlaka inamjua
14. sio makaburini
15. panafaa kwa kusudio lako?
16. mwisho uwe umeomba mashauri ya Mungu
 
🤝
 
Na ukinunua ardhi je anayempa dalali chochote kitu ni muuzaji au mnunuaji
 
Kwa mkoa wa Dar es salaam
1. Iwe imepimwa na ujus plot number na block number/name
2. Iwe ina hati ya wizara ya ardhi (Rais).
3. Isiwe na migogoro wowote uliosajiliwa.
4. Mmiliki awe Tayari kukupa nakala ya kitambulisho cha taifa/passport.
Ukiweka vigezo hivi utaishia kuwa baba mpangaji.

Hapo kwenye mgogoro ninakuunga mkonoo.
 
Wewe umenunua kiwanja wapi?
Ukitaka nikuuzie kiwanja kigamboni Kibada, mwasonga au Buyuni nicheki inbox, nina viwanja karibia 41 size ndogo ni sqm 864 na kikubwa ni sqm 10,000 navyote residential na housing Estate na kimoja kwa Public Building.
Hati ya Wizar na kodi zimelipwa.
Nakuonyesha kitambulisho Cha NIDA changu kabisa na tunafanya mauziano Manispaa ya Kigamboni.
Nitakuwepo bongo kuanzia Januari 15, 2025.
Kuwa muelewa, usiwe mbishi na usiwe mtu wa madharau.

Dar es salaam nzima ni Planning Area tangu 1993, under GN No 231 of 1992 kwa hiyo hakuna kisheria customary au deemed right of ownership kama sheria itafuata mkondo wake.
Na sehemu ambayo ina TP hairuhusiwi customary ownership of Land mpaka kiwanja kipimwe na upate hati ndiyo uuze kwa sababu ardhi yote ipo chini ya manispaa za Mkoa wa Dar es salaam.

sasa wewe sikiliza porojo tu za mtandaoni na ukanunue kiwanja kupitia mwenyekiti wa mtaa, baadae watoto wako waanze kumuomba mama Samia aingilie kati. Aingilie kat nini????
 
Kumbe upo nje ya nchi?

Umeandika kama vile kila mtu ananunua kiwanja Dar es Salaam.

Umeandika kama vile wewe peke yako ndiye muuzaji na mnunuzi wa viwanja Dar.

Pia kwa fikra zako ni kwamba mimi sijawahi kununua ardhi.

Una fikra kwamba ardhi yote ya DSM imepimwa na kurasimishwa.

Umeandika as if Dar bado ina maeneo mengi ya wazi ambayo hayajengwa.

Ni kwamba hauna taarifa kwamba watu sasa wanahamia Mkoa wa Pwani haswa Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Kisarawe, na Mkuranga.

Update taarifa zako, zipo nje ya muda kwa sababu upo nje nchi.
 
Wewe kama umenunua ardhi Dar es salaam, jua kwamba hukufuata sheria.
Pili,kwa sababu tu umenunua shati dukani kariakoo bila kupewa risiti, basi usidhani ndivyo mashati yote yananunuliwa bila kupata risiti.
Kwa hiyo mtu akiuliza ili ninunue shati kariakoo dukani inabidi nizingatie nini, basi mwambie azingatie kupewa risiti.
Mtu akiniuliza unanunuaje ardhi lazima nitenganishe Planning Areas (declared) na other areas apart from general land.
Mifumo ya kununua ipo tofauti kisheria na ushauri niliompa hautamletea matatizo kisheria hata ikitokea mtu mkubwa anataka kumpora hiyo ardhi.

Dhuluma inaweza kuanzishwa na wewe kutofuata sheria, siyo tu kwa sababu hutaki bali hufahamu. So, acha maneno ya kejeli na jifunze au nifunze kwa kutumia lugha nzuri na nyepesi isiyo na kashfa. na usi - assume kuwa unanijua sana, hata ndugu zangu wa damu hawanijui kivile.
 
Hayo maneno umeyaanza mwenyewe.

Kila mtu ana aina yake ya kumiliki ardhi. Usikariri Land Law!
 
Hamna kitu kama hicho, hayo ni mambo ya kijima halafu mnashamgaa kwanini mji hauna mpangilio.
Baraza linaangaliana na choo cha jirani na pembeni genge.
 
Ndiyo maisha ya Afrika.
 
Ni rahisi sana kujua chaka
Kabla hata ya kuumiza kichwa kufuatilia hati na umiliki wizarani
Kwanza usinunue kiwanja, jirani wa kwanza ni kilometer kadhaa, hapo unauziwa hifadhi ya taifa
Kama umeona na unakipenda, wewe sema sawa kesho nitakupigia au tutakutana tuanze mchakato
Kesho wewe damka, nenda kwenye maeneo ya kiwanja, tafuta majirani wake, na upige nao stori, mara nyingi majirani huwa wana namba za mmiliki wa kweli . au wanajua moja mbili tatu
 
Back
Top Bottom