Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
KAMA HIYO UNAKOTAKA KU-INVEST BIASHARA INALIPA KWA UHAKKA, CHUKUA. KAMA NI MAMBO YA KILIMO KISICHOTABIRIKA NA MVUA, USITHUBUTU!
 
Mpaka unasema hivo basi wewe hujawahi kufanya biashara, kwahyo sina cha kukushauri mkuu. Endelea tu kuukumbatia umaskini. Mtakuja kujifunzia biashara ukubwani, mkishastahafu, mzizike hela zenu mlizozisotea miaka 60, haha.
Naongelea kuchukua mkopo, huwezi kubahatisha kwa hela ya mkopo lazima uwe na calculated risks. Kuna jamaa aliingia all in kuchimba madini ikakwangua millions tena za watu sio zake!! karudi kuanza upya na madeni juu.

Always jilipue kwa ile pesa ambayo upo tayari kuipoteza. Zaidi ya hapo anza kidogo huku unaongeza mtaji taratibu.
 
Angeweka aina ya Investment anayotaka kufanya tungeweza kumshauri zaidi.

Asije ndani ya miaka 3 investment imekufa na bado ana miaka 6 ya kukatwa ataona kazi chungu.

All in all uamuzi ni wake, ila kwa uzoefu wangu watumishi wengi Mikopo wanayochukua huwa inafeli.
Hapo investment moja pekee haitoshi, inabidi hio hela aigawe kwa biashara hata 3.

Ningekuwa mimi, ningenunua mashine ya kusaga na kukoboa mahindi, nikanunua na mahindi yameshuka bei saivi, nikafanya packaging ya Unga. Pumba pia ni dili sana, na hela ya wanaokuja kusaga bado inaingia.

2. Ningenunua tent za kukodisha, viti vya plastic na meza za round kwa ajili ya sherehe mbali mbali.

3. Ningenunua mashine ya kukamua alizeti, mashudu nabaki nayo mimi, hela ya kukamua pia inaingia. Na pia alizeti nanunua kwa bei nayojiwekea mimi kama kilo moja ni 600 ni 600, hakuna ubishi, atawapata tu wenye shida, haha

Hapo hio 90M inarudi kama upepo.
 
Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Take your time to think of the investment that is not that much risky and of which has low competition..... sijui kama ipo lkn fikiria kwanza kwa undani...kwahesabu za karibu ni kuwa kila mwezi rejesho ni 833,333.00 Tsh hii siyo hela ndogo.......think twice una invest biashara gani itakuzalishia 833,333.00 kwa mwezi rejesho na faida yako juu ya hiyo rejesho
 
Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Chukua kagombee ubunge CCM, UKIPATA UKAWA WAZIRI ZINARUDI NDANI YA MWAKA, UKIKOSA UKAKUWA MGANGA WA KIENYEJI AU KUFUNGUA KANISA, ZITARUDI FASTA
 
Usiogope wewe chukua hela ila usifanye biashara za kubahatisha bila research ya kutosha,usisahau kuiombea sana kwa Mungu kazi yako (kanisani/Msikitini). Kama sio mtu wa ibada tafuta mganga konki😊 maana ukikaa kizembe utapukutishwa bila kujua .
 
Unadhani ni wajinga kihivyo wakukopeshe pesa bila ya kuifanyia tathmini nyumba yako? Ukiona unakopeshwa 500m jua kuwa nyumba yako ina thamani ya zaidi ya 500m endapo itauzwa
Kinachotazamwa kwenye mkopo siyo nyumba tu.

Kuna vigezo vingi, wenyewe wanakusomesha.
Benki wanataka kukopesha, ndiyo kazi yao. Bila kukopesha watafilisika.
 
,usisahau kuiombea sana kwa Mungu kazi yako (kanisani/Msikitini).
hapo hamna kitu, unaleta ujinga wa dini kwenye science!!!!!....hakuna cha kuomba, hapa ni science tu! Ukipanda juu ya mti ukajiachia ,utaanguka utakufa, hakuna sala wala swala ala Mungu atakunusuru...you will face the wrath of gravity....utakufa instantly...biashara itakufa instantly...
 
Back
Top Bottom