Hapo investment moja pekee haitoshi, inabidi hio hela aigawe kwa biashara hata 3.
Ningekuwa mimi, ningenunua mashine ya kusaga na kukoboa mahindi, nikanunua na mahindi yameshuka bei saivi, nikafanya packaging ya Unga. Pumba pia ni dili sana, na hela ya wanaokuja kusaga bado inaingia.
2. Ningenunua tent za kukodisha, viti vya plastic na meza za round kwa ajili ya sherehe mbali mbali.
3. Ningenunua mashine ya kukamua alizeti, mashudu nabaki nayo mimi, hela ya kukamua pia inaingia. Na pia alizeti nanunua kwa bei nayojiwekea mimi kama kilo moja ni 600 ni 600, hakuna ubishi, atawapata tu wenye shida, haha
Hapo hio 90M inarudi kama upepo.