Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

  • Matajiri wote wanakopa​
  • Wenye viwanda wote wanakopa​
  • Mkopo wa muda mrefu huwa ni faida kwa mabenki​
  • Kwa mtu anayetaka kufika mbali mkopo hauepukiki​
  • Muhimu ujue huo mkopo unaenda kuwekeza kwenye nini​
  • Kama mpambanaji, nakushauri chukua huo mkopo ata ukishindwa kulipa watakata kwenye akiba yako ya kustaafu.​
  • Kwa wale pia wenye magonjwa yanayoweza kuwapeleka mbinguni muda wowote na wana nafasi ya kukopa kupitia ajira zao; nawashauri wakope mkopo wa muda mrefu kwa faida ya familia zao; bima italipa.​
Ahsante Mkuu ..huu mkopo sifanyii biashara...nataka nikauwekeze kwenye mutual fund ninufaike na compound interest
 
Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Hiyo interest ni kubwa endapo hiyo hela utaiweka katika liabilities na sio Assets

Ukikopa hela wekeza katika biashara yenye cash flow ambayo italeta returning Kwa haraka.

Unaweza kuwa middle broker unapiga simu DSM kujua sokoni wanataka mini then wewe unawaletea na sio kulima uko kutoboa kupo Ila sio uhakika 100%

Kitu kingine kitachokupa hela ni Kuwa na taarifa sahihi
 
Hapo investment moja pekee haitoshi, inabidi hio hela aigawe kwa biashara hata 3.

Ningekuwa mimi, ningenunua mashine ya kusaga na kukoboa mahindi, nikanunua na mahindi yameshuka bei saivi, nikafanya packaging ya Unga. Pumba pia ni dili sana, na hela ya wanaokuja kusaga bado inaingia.

2. Ningenunua tent za kukodisha, viti vya plastic na meza za round kwa ajili ya sherehe mbali mbali.

3. Ningenunua mashine ya kukamua alizeti, mashudu nabaki nayo mimi, hela ya kukamua pia inaingia. Na pia alizeti nanunua kwa bei nayojiwekea mimi kama kilo moja ni 600 ni 600, hakuna ubishi, atawapata tu wenye shida, haha

Hapo hio 90M inarudi kama upepo.
Nna swali mkuuu

Wewe ni motivation speaker?
 
Habar za asubuh wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Mkopo nafuu na unaoleweka nenda kauchukue benki ya Zanzibar utakuja kunishukuru. Hayo mabenki mengine wote ni matapeli wakubwa!
 
Kuna compound effect Mkuu ..Niko tayar zikae hata miaka 30
Screenshot_2023-12-06-12-45-06-468_com.android.chrome.jpg

Nimecheki hesabu hapa mkuu, Go for it Champ
 
Back
Top Bottom