Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Wew bana,
Hio 16% ni kwa mwaka mmoja tu, endapo angechukua mkopo wa mwaka mmoja ndio hesabu ingekuja hio unayowaza wew,
Ila kwa kuwa ni miaka 9 hapo hesabu nyingi zinaingia katikati mambo ya reducing balance na ndugu zake ndo wataleta hio riba ya juu,
Japo kimahesabu ilibidi ije 72M sijui yeye kafanyaje kupata hio 90M
Mimi nakwambia kitu ninachokijua na practical issue si kubumba, sawa.
 
Hapana mkopo unatakiwa uuweke kwenye biashara inayoendelea tayari yaani uongeze liquidity, huduma, bidhaa n.k ila sio kwa uwekezaji mpya. Ni risky sana kufanya kitu kama hicho maana mpaka uwekezaji uanze kukulipa riba inapanda tuu utajikuta 50% ya faida latika miaka hii 9 inaishia kwa riba na hapo ni kama biashara itakua ina exist in 9 years!!
Chukua ushauri huu.
 
Take your time to think of the investment that is not that much risky and of which has low competition..... sijui kama ipo lkn fikiria kwanza kwa undani...kwahesabu za karibu ni kuwa kila mwezi rejesho ni 833,333.00 Tsh hii siyo hela ndogo.......think twice una invest biashara gani itakuzalishia 833,333.00 kwa mwezi rejesho na faida yako juu ya hiyo rejesho
Hyu akifungua hdw anapata hyo pesa na analipa kbsa huo mkopo tatizo Ni mkopo wa Muda mrefu
 
Habari za asubuhi wadau.

Nishaonana na Afisa mikopo tukapiga hesabu kabisa, nikichukua Tsh. Milioni 50 kwa miaka 9 riba ni 16% na nitatakiwa kurejesha Tsh. Milioni 90.

Naombeni mnishauri kwenye hili wadau, niache au nichukue mkopo huu?
Chukua, alafu tafuta demu mmoja mkaliiii, kamle tiGo
 
Wakati tunasoma hesabu wew ulikuwa unaweka vioo chini ya sket za wadada 😂😂😂😂😂😂😂

Btw, hio uliofanya wew ni kwa mwaka mmoja, kwa kuwa ni miaka 9 inabidi utumie ile formula ya kutafuta interest ambayo ni
I= PRT/100

P kianzio au Mkopo
R Riba
T Muda ambapo katika kesi yetu ni miaka 9
Kama hajui kumeki sabjecti bado kichwa lazima kiwake moto
 
Kopa weka kwenye real asset angalau hautolia.
Mfano ukichukua hio m 50 ukaifukia kwenye ardhi saveyed area.
Baada ya miaka 9 itazaa m 200 so toa M 90 utabakia na m 110 faida
 
Chukua mwanangu, alafu toa 10M katengeneze Tent za kukodisha 5, kwa mwaka jiwekee kurudisha mkopo kwa kiasi cha 10M ndani ya biashara zako tu. Tent pekee kwenye hio 10 zinakupa 5M, hio 5M nyingine angalia 40M utaiwekeza wapi.
Nahitaji ufafanuzi hapa mkuu nina akiba yangu nataka kuifanyia biashara nyingine tofauti na ninayo fanya. Hebu fafanua kuhusu Tent
 
Eddo nakupongeza na nlitaka niache watu wanaofikiri wanajua wabaki na ujinga wao.
Fomu za mikopo ya benki huwa zina clause ambazo zina maandishi madogo sana, huko kuna interest na compaunding interest.
Usijidanganye kuwa mkopo wa 50 M utalipa only 16%.
Kuna underlying charges nyingi sana mpaka legal fee, processing fee, insurance unaweka wewe na hapo afisa mikopo anataka laki 5.
Sikukatisheni tamaa ila huku mahakamani kila siku nyumba zenu zinauzwa hamkomi.
Ukitaka kukopa kapate ushauri wa wanasheria.
Mkuu nikushukuru kwa elimu uliyoitoa sababu umenipa mwanga kwenye haya mambo ya mikopo.

Ila hapo mwisho umemaliza vibaya, sababu hakuna pahala popote niliposema nahitaji mkopo, kwa hiyo siyo busara kunichuria nyumba yangu kuuzwa,
 
Back
Top Bottom