Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Ninataka kuchukua mkopo wa Tsh. Milioni 50 Benki ya CRDB kwa miaka 9, marejesho jumla nitalipa M90

Mkuu nikushukuru kwa elimu uliyoitoa sababu umenipa mwanga kwenye haya mambo ya mikopo.

Ila hapo mwisho umemaliza vibaya, sababu hakuna pahala popote niliposema nahitaji mkopo, kwa hiyo siyo busara kunichuria nyumba yangu kuuzwa,
am sorry Eddo, i know your house is not Dream house, haina Swimming Pool, haina Veranda na underground parking kwahiyo naombea iuzwe na dalali wa mahakama ili ujenge dream house utoke kwenye comfort zone ulipo sasa.
 
Nahitaji ufafanuzi hapa mkuu nina akiba yangu nataka kuifanyia biashara nyingine tofauti na ninayo fanya. Hebu fafanua kuhusu Tent
Akiba siwezi kukushauri cha maana, hio hata ikipotea haina hasara, fanya unachojiskia mkuu. Sisi tunashauri wanaochukua mikopo tu ili wasije wakaumbuka, nyie wengine mnajiweza, fanya unachokiona ni sahihi na unakipenda, Amin, utatoboa.
 
Hujasema unaenda kufanyia nini unaomba ushauri uchukue au usichukue , mpka unafikia maamizi ya kuchukua 50M ulitakiwa uwe ushafanya maamuzi. USHAURI Wangu USICHUKUE HUJAJIPANGA.
 
Akiba siwezi kukushauri cha maana, hio hata ikipotea haina hasara, fanya unachojiskia mkuu. Sisi tunashauri wanaochukua mikopo tu ili wasije wakaumbuka, nyie wengine mnajiweza, fanya unachokiona ni sahihi na unakipenda, Amin, utatoboa.
Duh kwahyo kama akiba yangu ndo sifai kupata ushauri!! Sawa afisa mikopo
 
Riba haramu kivip HV uanjuwa wazungu na wachina wanaendesha biashara kwamikopo ila wee maskini hujui Hili

Mikop ndio source namba moja ya uwekezaji
Sijawahi kuchukuwa mkopo wala baba yangu hajawahi kuchukua na alikuwa na biashara zake Tatu akianza akiwa na miaka 20 tu
Mimi nimefanya kazi ya kuajiriwa sambamba na biashara na sijawahi kuchukua mkopo

Leo nina miaka zaidi ya 60 na nina uwezo wa kununua hata nyumba kubwa ya 200m bila shida yoyote na ni cash
Mimi sio masikini hata familia yote

Ila ukitaka uwe na nidhamu ya hela save sana bila kutegemea mkopo, achana na mwenye mamilioni huyo huwezi kujua amechukua mkopo kwa mkataba wa aina gani na aliempa

Mimi naweza kumpa mtu mkopo wa bila riba kwa sharti la kurudisha baada ya mwaka mmoja, na ndio nafanya na ndugu zangu

Nilichukua mkopo wa mwezi mmoja wa 80m nilipopata dili la chap chap na nikatengeneza 20m kwa wiki 3
Nilimrudishia mshkaji wangu 80 yake bila senti ya ziada na kumuambia nimepata 20m profit
Hapo hatuna riba na maisha yanaenda boss

Sio sifa wala nini bali haya ndio maisha yetu kiuhalisia
Uwe na siku njema
 
Mnadanganywa makapuku, kina MO, Azam wote hukopa kwa riba
Mimi sio Kapuku mkuu na sijawahi kuchukua mkopo na niko vizuri kimaisha
Naombwa kila leo nichukue mkopo ila nimekataa na ninaendelea na maisha mazuri kuliko hao makapuku waliochukua mkopo bila akili na mwisho kwa aibu gari linapita na maspika kutangaza uuzwaji wa nyumba zao na kurudi umasikini au kuwa jambazi kabisa na kwenda kutafuta SMG
Ila hao matajiri kila mmoja ana nafsi yake
 
Mimi sio Kapuku mkuu na sijawahi kuchukua mkopo na niko vizuri kimaisha
Naomba kila leo nichukue mkopo ila nimekataa na ninaendelea na maisha mazuri kuliko hao makapuku waliochukua mkopo bila akili na mwisho kwa aibu gari linapita na maspika kutangaza uuzwaji wa nyumba zao na kurudi umasikini au kuwa jambazi kabisa na kwenda kutafuta SMG
Ila hao matajiri kila mmoja ana nafsi yake
Mkuu sio Kila anaechukua mkopo ni kapuku
 
Huyo hatakiwi kufanya biashara inayotaka proper management, maana kashakwambia security yake ni kazi, so lazima aende kazini. Hardware inataka usimame mwanzo mwisho, itamshinda tu wala halina ubishi.
Oohh Basi hyu huyu Hana la kufanya acha akope huko halmashuri tu kama alivyo ambiwa Happ
 
Back
Top Bottom