Ninatoa dollar $1000 kwa atakaenifanikishia Visa hii

Mmmh
Wakukague vizuri aisee
 
Wewe umeongea Kama mwanaume!
 
Mkuu LaRosa we unahitaji mwaliko tu?? Ukipewa mwaliko labda wa Sweden unapo mahali pa kufikia au ndio inabidi mtu aliekualika ndio akupokee??

Lakini pia kipindi hiki cha Pandemic visa zimekuwa shida sana hata kwa nchi ambazo hawana lockdown kama Sweden, wanahitaji sababu za msingi sana ndio wakuruhusu kwenda, watu ambao wanaenda bila usumbufu ni wale wenye residence permit.
 
Asante kwa response yako nzuri. Kuna jamaa ananifanyia mchakato na tumefikia pazuri tu.
Nakupenda Jimena [emoji257]
 
Nimeshindwa kuelewa kwa nini kashindwa kuelewa maelezo uliyompa ambayo kwa mtu mwenye akili akiyatafakari ni majibu yenye mantik
Hakika watu kama hawa ukiwasaidia ndio wanaweza kukutumbukiza kwenye matatizo makubwa na ukabaki na majuto.
 
Mkuu nenda kwa mganga mpe dola 50 tu, unaenda mpaka ulaya ata bila kulipa nauli,
 

We mkuu ndo unataka kuja huku ulaya au kwenda huko USA kwa lugha kama hizi. Kwanini watz hatupendi kuambiwa Ukweli. Huyu mkuu kaeleza Ukweli Wake tena hadharani, kosa lake nini, unakuja na hukumu baseless namna hiyo. Je ulitaka akudanganye.

Kama una hela why utake kuhonga dollar 1000. eti una mambo ya kufanya. Ulaya utafanya biashara na unasema Bank huna zaidi ya 6000. umemkosea sana huyu mkuu.
 
Kwa hali ilivyo sasa ni vema kutimiza masharti upate visa halali na halisi
Kwa miaka ya nyuma shortcuts ziliwezekana , maana technology haikutumika sana , siku hizi bank statements unaweza ukaombwa ukiwa safarini mana wanajua hazina mlolongo.
Kwa maana hii hata ukiuziwa bank statements na ukapata visa , huko mbele inaweza kuwa kitanzi kitakachokufanya uwe deported.
 

Mkuu moja ya kitu kirahisi kufoji ni BS. Hiyo hata ukipewa saa1 utoe utaipata kama unajua nini cha kufanya. Ikumbukwe si ubalozi au uhamiaji wa nchi yeyote ile duniani utaenda ku-verify uhalali wa BS yako na bank yako bila idhini yako au mahakama kuamuru hivyo. You just have to play your cards right.

Kila mtu akifuata hivyo vigezo wanavyotaka sijui 20K USD, kazi, assests etc. nje wataenda mafogo tu, mbongo gani wa kawaida anavyo hivyo vigezo? Watoto wa mbwa tunapita mlango wa nyuma, hii haitaisha leo wala kesho.
 
Kwani una tatizo gani hadi utumie agenti, visa za Uarubuni na Asia ndio labda unaweza tumia agenti lakini hizi za Ulaya/Marekani unatakiwa mwenyewe uende front, ukapigwe maswali na kama wameridhika unaambiwa njoo keshokutwa uchukue viza kiulaini . Nina wasiwasi utakuwa na matatizo ya kutaka kuzamia au ulifanya uharifu fulani. Ukiwa mkweli kwenye maombi ya visa huwezi kukosa hata siku moja hata iwe kwa Biden,lakini ukiwa muongo na ukitaka kutumia ujanjaujanja utakwama tu.
 
Mimi sijawahi kuulizwa BS wala kukosa viza toka nianze kwenda majuu, maswali mengine yanakuja kutokana na muonekano wako na jinsi unavyojiamini kujibu maswali ya watoa viza. Kingine muhimu ni kuonyesha kuwa utarudi baada ya siku zako za viza kuisha.
 
Ubalozi wa Australia nairobi wanapiga simu hadi bank husika , iloshawahi nitokea
Halafu Bs unafoji vipi wakati unaweza kubanwa wakati wowote uoneshe salio? Siku hizi Watu wanatembea na ATM cards ambazo zina link moja kwa moja na account yako,
Forgery kwenye makaratasi ya kuombea viza inawezekana ila ukiwa safarini inaweza kukukost anytime. Na ukawa deported.
 
Elfu moja inaweza kuwa haitoshi kwa mtu mwenye akili timamu kuuza credibility yake kwa ajili misheni zako.
 

Mkuu with all due respect ulichowasilisha is the most ridiculous thing I've ever read. You mean to say hao uhamiaji wanataka pesa iwe kwenye account yako full time ili tu wao kujiridhisha? Pesa yako haina shughuli zingine? Sitaki kuamini kuna uhamiaji wa nchi fulani ni mazwazwa kiasi hicho.

Inakubalika kutumia sponsor, sasa vp kama umetumia BS ya sponsor maana wengi tu wanaenda kwa kuwa sponsored? Bado watasema onyesha salio anytime huko mbeleni? Unatoaje latest BS ya sponsor on the spot? This doesn't make any sense at all.

Secondly, ubalozi kupiga simu na bank kutoa taarifa za mteja is wrong at all levels. Banks are committed to privacy. Kawaida banks hutoa taarifa kwa serikali tena kwa idhini ya mahakama au kibongo bongo kwa serikali kutumia mabavu ila sio kwa ubalozi au third party kiholela. Kama KE banks zipo loose hivyo basi KE is worse than TZ maana hilo swala bongo halipo kabisa na si bongo tu bali hata nchi zingine, natilia mashaka sana. Mambo ya mabalozi kupiga simu sijui kuingia online na kuangalia bank acc yako ni story za kijiweni na wengi wanaziamini sana.

Nakubaliana na wewe kwamba forgery can be costly ndo maana nimesema lazima mtu ajue anachofanya, take calculated risks na awe willing kukubali matokeo should things backfire. Kutoboa duniani lazima uwe risk taker ukisubiri kila kitu kiende kimenyooka utasubiri sana. Wengine tumecheza sana on the blurry zone so I know what I'm talking about.
 
kaka ifike hatua watanzania tuwe kama wanaijeria tusaidiane kutimiza malengo ndo msingi wa ubinaadamu na ili waafrika tuendelee
 
Mexico tena wakati wameshajenga ukuta?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…