Naona kwenye uzi huu watu wengi wanazungumzia kwenda ughaibuni lakini maelezo machache sana ndo ya uhakika.
Kwa ufupi viza kwa sasa nchi yeyote ya maana si rahisi,na hii corona imezidisha ugumu ukitilia maanae status yaTz na corona haijulikani. Kwanza sahau kabisa kutumia viti feki kuombea visa,utakosa.
Visa za kutembea au za uanafunzi,bado ngumu sababu wanajua wengi wazamiaji,has nchi za Usa na canada, ulaya hasa uk wana masharti ya ovyo na wanataka kozi utalayoenda kuisoma haipatikani bongo pia uwe umelipia kiwango flani cha fee.Ili upate urahisi,kozi iwe undergraduate au graduate (degree ya 1na masters),ieleweke international student uk anaweza kulipa ada ya kuanzia £10,000 kwa mwaka mpaka £38,000 kwa mwaka kutegemea na course na chuo ulochagua.
Visa ya kutembea pia bahati nasibu,unaweza ukapata barua ya mwaliko,cheti cha nyumba,pesa bank na mwenyeji bado wakakunyima.
Njia ya uhakika zaidi,ambayo inahitaji uvumilivu ni moja tu,Ndoa.
Ukipata mwanamke au mwanamme anaeishi usa,canada,uk australia,germany,france you name it,kama anafanya kazi ya halali,analipa kodi,ana sehemu ya kuishi na ana mkataba nayo akaamua kuoa au kuolewa na wewe ulie bongo,wewe wa bongo hutakiwi kufanya mambo mengi,yote anamaliza yeye.hii mdo njia nyepesi kuliko zote unazosona hapa,sababu ukipata viza ya ndoa ukifika unapoenda unaweza kufanya kazi moja kwa moja tena ki harali kabisa.ukasoma ukitaka na unaweza kurudi kwenu mda unaotaka.
Wabongo wengi wapo izo nchi na uraia wao na wana uhitaji wa wake na wengine waume,tatizo hatuaminiani,lakini ukimpata atakaekuamini utashangaa utakavyopanda ndege ki uraini.
I speak from experience na wala sijimwambafai.