Ninavutiwa Sana na Utulivu na Umakini wa Rais Samia Kiuongozi

Ninavutiwa Sana na Utulivu na Umakini wa Rais Samia Kiuongozi

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Kiukweli ninavutiwa sana na utulivu na umakini mkubwa sana wa kiuongozi alionao Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha Watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hassan. Ni kiongozi mtulivu na makini sana katika kufanya maamuzi pamoja na kuchukua hatua.

Ngoja niwaambie jambo moja ndugu zangu. Kiongozi asipokuwa makini na mtulivu kiakili anaweza kujikuta amepeleka jeshi vitani mahali palipohitajika kufanya mazungumzo tu na upande mwingine. Anaweza kujikuta ametoa kauli mahali palipohitaji kukaa kimya, kutoa maneno na amri inayoleta mpasuko na kuligawa taifa pamoja na wananchi, lakini pia kudhoofisha umoja wa kitaifa. Anaweza kutoa maneno yaliyotakiwa kubakia kama siri za taifa na usalama wa taifa.

Rais asipokuwa makini na mtulivu anaweza kujikuta anafanya makosa mengi sana kuanzia namna ya kupanga safu ya wasaidizi wake, nani akae wapi na nani akae wapi. Ni sawa na kuwa na wachezaji nyota katika kikosi chako lakini kama hujui ni nani aanze na acheze namba ipi na apangwe na nani unaweza ukajikuta hupati matokeo, kwa kuwa tu wachezaji unaowapanga hawaelewani wakiwa uwanjani, kwa kuwa unawapanga namba zisizo sahihi hivyo kuwanyima uhuru wa kucheza.

Kwa utulivu na umakini wa Rais Samia ndio maana mnaona taifa linaendelea kutamalaki kwa amani na utulivu hapa nchini, kwa kuwa yeye hata akishambuliwa kwa matusi na lugha za matusi na baadhi ya wanasiasa uchwara, unakuta yeye anaendelea na kazi ya kuwatumikia Watanzania bila kutoka hadharani kujibu kwa hasira na jazba.

Hii ni kwa kuwa Rais wetu mpendwa hutumia akili kubwa na siyo hisia na mihemuko. Hafanyi maamuzi wala kutoa kauli kwa jazba au kukurupuka. Hii ni kwa kuwa anatambua ukubwa wa nafasi yake kama mkuu wa nchi. Huwezi ukamsikia mama yetu kipenzi akiripuka hadharani huku akiwa amejaa jazba, kwa kuwa anatambua kutumia jazba, hasira, mihemuko na hisia pasipo kutumia akili kwa utulivu na umakini inaweza leta picha mbaya pale yatakapotolewa maneno kwenye kinywa chake yatakayomshushia heshima na kudhalilisha mamlaka ya urais na kiti chake.

Taifa letu linawahitaji sana viongozi wengi sana aina ya Rais Samia. Tunahitaji wawe wengi kuanzia ngazi za ukuu wa wilaya, mkoa, mawaziri, ma OCD, RPC, wakurugenzi, maafisa utumishi na wengine wengi. Tunahitaji viongozi wale watoa amri wawe watu makini na wenye utulivu wa akili na moyo. Siyo watu wa kukurupuka, mihemuko, sifa za kitoto, majivuno na ubabe ubabe wa kijinga na ulevi wa madaraka.

Ukiwa na kiongozi asiye na utulivu na umakini halafu akawa na mamlaka mkononi mwake ataonea na kuumiza sana watu, atawatoa wengi machozi na kuwafanya wengine wengi wajute kuzaliwa hapa nchini. Tunahitaji kiongozi ambaye moyo wake umejaa hofu ya Mungu na ni mcha Mungu kama ilivyo kwa Rais Samia.

Kazi iendelee, mama ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa. Mama anatosha kuendelea kuliongoza taifa letu kwa muhula wa pili.
 

Attachments

  • FB_IMG_1612420221935.jpg
    FB_IMG_1612420221935.jpg
    22.2 KB · Views: 2
Mabadiliko tuliyoyaona ya rais Samia ni kama ifuatavyo
1.kupanda Kwa nishati.mfano petroli Kwa Sasa ni 3500/Lita tofauti na miaka mitatu nyuma ilikuwa1500/Lita.
2.wafanyabiashara wa malori kutoka congo kwenda bandari ya Dar wamehamia Mombasa baada ya kuuzwa Kwa dp world tofauti na miaka kadhaa nyuma wateja wa congo walimiminika Dar na kutupatia Kodi nyingi.
3rushwa imekithiri nchini kuliko kipindi chochote toka tupate uhuru.kwa Sasa rushwa inaombwa waziwazi
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kiukweli ninavutiwa sana na utulivu na Umakini Mkubwa sana wa kiuongozi alionao Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan. Ni kiongozi mtulivu na makini sana katika kufanya maamuzi pamoja na kuchukua hatua.

Ngoja niwaambie jambo moja ndugu zangu. Kiongozi asipokuwa makini na Mtulivu kiakili anaweza kujikuta amepeleka Jeshi vitani mahali palipohitajika kufanya mazungumzo tu na upande mwingine,anaweza kujikuta ametoa kauli mahali palipohitaji kukaa kimya,ametoa maneno na amri inayoleta mpasuko na kuligawa Taifa pamoja na wananchi,lakini pia kudhoofisha umoja wa kitaifa.ametoa maneno yaliyotakiwa kubakia kama Siri za Taifa na usalama wa Taifa.

Rais asipokuwa makini na Mtulivu anaweza kujikuta anafanya makosa mengi sana kuanzia namna ya kupanga safu ya wasaidizi wake,nani akae wapi na nani akae wapi .ni sawa unawachezaji nyota katika kikosi chako lakini kama hujuwi ni nani aanze na acheze namba ipi na apangwe na nani unaweza ukajikuta hupati matokeo ,kwa kuwa tu wachezaji unaowapanga hawaelewani wakiwa uwanjani kimbuni ,kwa kuwa unawapanga namba zisizo sahihi.hivyo kuwanyima uhuru wa kucheza.

Kwa utulivu na Umakini wa Rais Samia ndio maana mnaona Taifa linaendelea kutamalaki kwa amani na utulivu hapa Nchini,kwa kuwa yeye hata akishambuliwa kwa matusi na lugha za matusi na baadhi ya wanasiasa uchwara unakuta yeye anaendelea na kazi ya kuwatumikia watanzania bila kutoka hadharani kujibu kwa hasira na jazba.

Hii ni kwa kuwa Rais wetu mpendwa hutumia akili kubwa na siyo hisia na mihemuko.Hafanyi maamuzi wala kutoa kauli kwa jazba au kukurupuka.hii ni kwa kuwa anatambua ukubwa wa nafasi yake kama mkuu wa nchi.huwezi ukamsikia mama yetu kipenzi akiripuka hadharani huku akiwa amejaa jazba.kwa kuwa anatambua kutumia jazba ,hasira,mihemuko na hisia pasipo kutumia akili kwa utulivu na Umakini inaweza leta picha mbaya pale yatakapotolewa maneno kwenye kinywa chake yatakayomshushia heshima na kudhalilisha mamlaka ya Urais na kiti chake.

Taifa letu linawahitaji sana viongozi wengi sana aina ya Rais Samia.tunahitaji wawe wengi kuanzia ngazi za ukuu wa wilaya,mkoa,mawaziri,ma Ocd,RPC,wakurugenzi,maafisa utumishi na wengine wengi. Tunahitaji viongozi wale watoa amri wawe watu makini na wenye utulivu wa akili na moyo. Siyo watu wa kukurupuka,mihemuko,sifa za kitoto ,majivuno na ubabe ubabe wa kijinga na ulevi wa madaraka.

Ukiwa na kiongozi asiye na utulivu na Umakini halafu akawa na mamlaka mkononi mwake ataonea na kuumiza sana watu,atawatoa wengi machozi na kuwafanya wengine wengi wajute kuzaliwa hapa nchini .tunahitaji kiongozi ambaye moyo wake umejaa hofu ya Mungu na ni mcha Mungu kama ilivyo kwa Rais Samia.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa.Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
Wewe mwenzetu unakutana na Rais wetu wapi mpaka uujue umakini wake!!?

Watanzania tulio wengi tunajua anaishi Angani tu na inapotokea ametua ardhini basi atakuwa USA, Ulaya, Asia na Mlimani City!!

Wewe mwenzetu unamuona wapi na huo umakini!? Au na wewe mwenzetu ni Msanii na Leo upo hapo Korea?
 
Back
Top Bottom