Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

mbona sasa unamezea tena chadema mate? wakati ukiyafanya hayo yaliyofanya ufukuzwe hukujua hukujua hilo??? kweli hakuna chama kama chadema!! ni babu kubwa.
 
Tatizo lako wewe na hako kabinti sijui mnakaita shenzi manafikiri mkiandika sana kuhusu Slaa na Mbowe ndio mtaonewa huruma. Na mlivyokuwa wajinga mnadhani mpo katika mikono salama na mnashabikia udini, ukanda na ukabila mkidanganywa na Nape hapo. Subirini kidogo mtakapoambiwa nini ni Wamalawi au Wazambia ndipo mtajua. 2015 sio mbali kama hamuamini waulizeni Bashe na Dr. Salim. Lakini huenda huo ni utoto tu mkikua mtaacha maana hata Tambwe alipotoka CUF alikuwa na kelele kama ninyi. Mmeshindwa kujifunza kwa Lamwai, Kabouru na Ngawaiya?
 
katolewa kafara huyo isionekane CHADEMA yahusika, ila ni walewale-ngiri na nguruwe- "NCHI HAITATAWALIKA" na sasa kauli ya maaskofu wataka "ku-shift attention". Kosa lake ------ ni kutamka wazi urais wake hauna ubia na mtu baada ya kupambwa na maaskofu kuwa ni "chaguo la MUNGU". Sisi yetu macho na masikio hayatoshi bali pia twaweka rekodi kila kauli na tamko. Now we can at least join the dots and find "The church and CHADEMA" are Prototype and the same. shit!
 
katolewa kafara huyo isionekane CHADEMA yahusika, ila ni walewale-ngiri na nguruwe- "NCHI HAITATAWALIKA" na sasa kauli ya maaskofu wataka "ku-shift attention". Kosa lake ------ ni kutamka wazi urais wake hauna ubia na mtu baada ya kupambwa na maaskofu kuwa ni "chaguo la MUNGU". Sisi yetu macho na masikio hayatoshi bali pia twaweka rekodi kila kauli na tamko. Now we can at least join the dots and find "The church and CHADEMA" are Prototype and the same. shit!
Alisima Baba Riz urais wake hauna ubia ndiyo kosa lake
 
Hata mimi nilimsikia Tundu Lisu akimkana do kuwa hawamfahamu. Hichi siyo ki2 kizuri hata kidogo
 
Ujifikirie na wewe,kumbuka bado uko kwenye SIASA haya yaliyompata Ludovick kama ulivyosema huenda yakakutokea wewe

Ludovick kamwe hahitaji wakili ikiwa Rwakatale anatoka na Ludo atatoka kwani kosa halikamiliki paspo rwakatale kuwepo angalieni hapo hiyo ni sinema ya wasomi wa sheria.
 
Nina SWALI MOJA TU KWAKO; Kujiunga kwako na CCM UTAKUWA Unazungumzia Ubaya wa VIONGOZI wa CHADEMA au Utakuwa unaongelea POLICIES na MAENDELEO ya Wananchi ni KITU GANI kinachofanya Wananchi hadi leo MASIKINI ni
Kwasababu ya;
a - UFISADI
b- Uuzaji Ovyo wa Mali za Umma kama Viwanda na Majumba
c- Ubovu wa Elimu Nchini
d- Udhaifu wa Uongozi wa NCHI
 
Una mengi ya kufanya kwenye chama chako kipya kama political machine (kutumiwa kisiasa) haya ya Rwakatare yapo chini ya Dola huna haki ya kuleta simulizi zako jamvini ila una haki ya kwenda mahakamani kutoa ushahidi kama kweli una uthubutu....
 
Chris Lukosi, kwa kuwa uko hapa kama verified user, naomba nikuulize a hypothetical question...unao uhuru wa kujibu ama kutojibu.
Hivi Chadema kusambaratika leo na kutoweka kabisa katika medani ya siasa Tanzania, je kutawezesha;

  • Maisha bora kwa Watanzania kupatikana?
  • Madawa kupatikana mahospitalini?
  • Waalimu na madawati kupatikana mashuleni?
  • Ufisadi na wizi kukomeshwa serikalini?
  • Utapanyaji wa mali za asili kumalizwa nchini?
  • Utiaji saini wa mikataba mibovu kusitishwa?
  • Utawala bora unaotoa haki kuimarika?
  • Viongozi waliotanguliza rushwa kutokomezwa?
  • Matatizo lukuki yanayowakabili Watanzania kutatuliwa?
Nimeyaita haya hypothetical questions kwa sababu moja tu, najua Chadema haifi, imevuka ile threshhold ya kusambaratika...lakini hata kama hilo lingewezekana, mwamko wa mwananchi hauwezi kuzimwa hata kwa kutumia mtutu wa bunduki. Hivi sasa naamini kwa dhati kuwa Chadema ni zaidi ya viongozi wake, Chadema ni zaidi ya wabunge wake na Chadema ni zaidi ya wanachama wake moja moja...Chadema is a movement and is much more than anything else in its physical form.

You have said it all, mwanzo nilidharau kusoma uzi wa huyu jamaa anajiita Mwampamba, kwa kuona kuwa ni kupoteza muda, leo kwa kuwa nimejikuta nina 'free time' nikasema ngoja nisome mawazo ya mwenzetu...

..... bado tuna safari ndefu kama Taifa kwa sababu kuna watu 'wanajiita ni viongozi' e.g. Mwampamba lakini wana mawazo na hoja nyepesi sana bora hata watoto.
 
Mtela Mwampamba ni wewe kweli mdogo wangu au ni kivuli chako ila mwili ni wa mwingine? Huu uandishi wa kimtiririko namna hii haujapata kuonekana kwenye maandishi yako ya kabla. Kweli umepevuka!!
 
Last edited by a moderator:
Kumbe LUDO alikuwa mtu muhimu sana huko? Alikuwa anafanya special assignments za Slaa?
 
tatizo humu wana JF wanamshambulia mwampamba badala ya kutoa hoja
 
Mtela Mwampamba ni hivi, hukuwahi kumfahamu Ludovic, isipokuwa alichofanya ni kukufanya ujidhani unamfahamu, tena alihakikisha ufahamu wako unakua kwa kiwango atakacho yeye na vile atakavyo.
 
Last edited by a moderator:
Ukombozi unatakiwa uanzie kwako maana vijana mnaendekeza njaa.Ni muda wa kujitafakari mwenyewe unatumikaje na yule mwenzio mliofukuzwa CDM
 
teh teh teh.!
inaonekana imekuuma sana ulivyotimuliwa chadema!
acha UVIVU kijana, 'get a job' sio kuleta hoja lege lege humu,
i bet wewe na dada yako yule mmehusika katika ili in one way or the other, andaeni sinema nyingine hii ya lwakatare imefeli..
endeleeni na CCM ila ukae ukijua wewe na shonza ni kama bigijii tu, utamu wenu ukiisha CCM itawatupilia mbali (and i bet that will be very soon).
and that is what all cowards get!
MTAISOMAAAAA.!
hahahahahahahahhahahahahhahaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhhhh..
 
VIPI WEWE NI Mwl wa shule gani ?maana naona kila cku uko kwenye media ukipiga miayo ?
 
Naona ulikuwa na malalamiko mengi ukimshambulia Saanane na leo umeamua kutoka na Ludo.
Mfa maji haishi kutapatapa.
yaliyo CHADEMA waachie wanachadema. ulidhani umeokota lulu kumbe garasa. nenda nccr km kweli wewe ni mpiganaji uliyekusudia kuleta mabadiliko.
 
Salaam Mtela Mwampamba. Ingia Google leo. Tafuta kitu kilichojulikana kama Operation Manhattan. Hiki ndicho kilichozaa bomu lililoua watu wengi sana pale Hiroshima na Nagasaki, Japan. Bomu hili lilitengezwa katika jangwa kwenye jimbo la Nevada, kule Marekani. Ilikuwa Siri kubwa sana wakati wa kutengeza bomu lile. Wanasayansi waliohusika kufanya design ya bomu walifungiwa kama kwamba walikuwa jela. Iliitwa Operation Manhattan kuficha siri; kupoteza watu maboya.

Lakini Siri zilivuja na Urusi wakapata fomula ya kutengeza bomu lile.

Katika like kundi la Wanasayansi waliokuwa wameaminiwa sana, alikuwepo msanii mle ndani; alikuwepo fundi wa ku-act mapenzi. Na hakuwa wa kwanza kuwa na kipaji cha aina hiyo hapa duniani. Historia ya dunia imejaa wasanii wa aina hiyo. Kwa malengo ya hoja hii, napenda sasa niitumie Biblia kama kitabu cha Historia, kwa sababu mengi yaliyopo mule ndani ni Historical facts. Alikuwepo Delila aliyemsaliti mumewe Samson, na baadaye alikuja Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu. Double Agent mzuri ni lazima akuaminishe kuwa ni mwaminifu kwako. Ujue hapo sasa kwamba Double agent mzuri kama Yuda aliweza hata kumuaminisha Yesu mwenye upeo ambao ulikuwa supernatural.

Sina ushahidi wa kutosha kumuita huyu kijana mwenzako LUDO kuwa alikuwa Double Agent, lakini ushahidi wa kimazingira unaonesha kuwa kuna uwezekano mkubwa alikuwa Double Agent--kama ulivyokuwa wewe Mtela Mwampamba, Juliana Shonza, na Shitambala. Katika Taasisi zenye roho ngumu, destiny ya Double Agent huwa execution. Mumshukuru sana Mungu bado unapumua. Mwahondeye kufwa Mweeeenti...

Serikali ya Marekani ilifanya execution kwa yule Double Agent aliyevujisha Fomula ya bomu la Hiroshima. Hiyo ndiyo njia ambayo ma-Double Agenta huwa wanatakiwa kwenda. Wewe dogo umesoma BAED lakini inaelekea kuna mambo mengi sana huyajui. Chama kilifanya makosa makubwa sana kuwakabidhi makinda nyie nafasi nyeti kama zile mlizopewa pasipo kujipa muda wa kutosha kuwafahamu. Chadema ni chama chenye huruma sana. Mshukuruni Mungu.



Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION "BAED") katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na CHADEMA na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga CHADEMA. (LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history & political science).

Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa CHADEMA kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya CHADEMA, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na "mwanzilishi pekee" wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa CHADEMA mimi nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling'atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya CHADEMA kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii.

Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha, ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr. Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-

  1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr. SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
  2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr. SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya CHADEMA na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa CHADEMA.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
  3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr. Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr. Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
  4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.

Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR. SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA kwa kupanga na kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka CHADEMA, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR. SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa JamiiForums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU………. INAHUZUNISHA..!

Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na CHADEMA ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa CHADEMA wamekana kumtambua LUDOVICK, ni USALITI KIASI GANI HUU..?

Mawakili wote watano ambao ni:-

  1. MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  2. ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  3. NYARONYO KICHERE
  4. TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
  5. PETER KIBATALA


Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? Ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea CHADEMA, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.

ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.
 
Back
Top Bottom