Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

quote_icon.png
By Crashwise
Yaani hii ngoma kama polisi wetu wangekuwa makini wangeshapata ukweli kitambo sana kwanza mwampamba hajàndika mwenyewe hiyo thread na bado wanajaribu kuwaunganisha viongozi wetu wa kitaifa hasa dr slaa, najua lengo lenu ni kukichafua chama kama siyo kumzuia dr asigombee lakini mme shindwa mapema sana..watanzania wanajua kupembua mambo kuliko mnavyodhania..
ona na huyu ali'post tarehe 12 January.
quote_icon.png
By TUNTEMEKE
kwa bomu linalokuja naona utakata tamaa kabisa,Kwa sbabu bomu hilo linaianika chadema na michezo yao yote michafu inayofanyika kwa usiri mkubwa na kuwaaminisha watanzania kwamba ni serikali kumbe ni wao.

Yaani,nakuombea uwe hai ushuhudie mwaka huu watu wanavyoumbuka.Asante mungu kwa kufanikisha hatua zote kilichobaki ni kuweka kwa tv muone

ona na huyu ali'post tarehe 12 January.

Zumbemkuu!!!!.. Nakupa tano kwa hili!!!!
 
mm naona Chadema inawapa tabu kwakuwa moto wake mkali inshu ya undugu ipo ccm na sio chadema kwakuwa ccm hawawez kujitetea kwamba wanafanya hivyo ili kujenga chma kwan tiyari kile ni chma kikongwe lakn CDM nadhan wako hivyo kwakuwa tunaambiwa mitume kama Mohammad,na mwanzilish wa Ukristo Yesu walianza kuungwa mkono na watu wao wa karibu then imani ikasambaa kwa wote.Lakn ss hv ccm kipindi cha uanzilish kimekwisha ni muda wa kuwapa na wengine wakaongoze kwan wanachama ss ni wengi .Hv utailaumu CDM wakat ndo kwanz wajipanga ,suala la undugu ccm ni kubwa mno mm ckudhani km J.Nkamia angewabeza waa
ndish wa habari lakin labda niache hilo niseme ukweli au jambo ambalo lilinikuta mwenyewe mnamo mwaka 2005 nikiwa nimechguliwa kusomeshwa na halmashauri kwakuwa ni yatima diwani wa ccm kipindi kile alistisha ada yangu kwakuwa mama hana khanga wala kofia ya ccm badala yake akampa mtoto wa ndugu yake ambaye hat hvyo aliacha masomo kwa kuwa na ujauzito.Jambo hili lilinihuma sana mpaka sasa sihitaji chma chochote cha siasa
 
pole aise,pole sana
 
Mwampamba unatumika kama Ludovic au mko kitengo kimoja na Ludovic hadi hivisasa Chini ya Savimbi Mwigulu Nchema lamek Madelu. Unajua kwanini.
Vipi umtetee mtu unaeonesha wazi alikugombanisha au kukuchonganisha wewe na Viongo wa Chadema na kutoa taarifa kwa viongozi chadema zilizomfukuzisha babaako uanachama chadema.

Je wewe sasa upo kitengo cha mtandao cha Mwigulu?

Samahani sababu sikujui ivi we ni mwanamke au mwanaume

je kama unakiri kuwa Ludo ulimleta wewe chadema lakini alikusaliti je kwanini ushangae mtu huyu kuusaliti tena uongozi wa chadema kwa ahadi hewa kutoka kwa Mwigulu nchemba.

Mwampamba usikubali kutumika ka condom kunakazi nyingi za kufanya vizuri tu nje ya siasa
 
Video hii inajibu dhana ya usaliti wa Ludovick

Kwamba huyu Ludovick akiwa ndani ya Chadema amefanya kazi za Mwigulu, za kurekodi video iliyokusudiwa kuangamiza chama.

Huyu ndiye anapaswa atetewe na Chadema, na asipotetewa amesalitiwa!!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION “BAED”) katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na CHADEMA na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga CHADEMA. (LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history & political science).

Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa CHADEMA kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya CHADEMA, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na “mwanzilishi pekee” wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa CHADEMA mimi nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling’atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang’ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya CHADEMA kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii.

Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha, ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr. Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-

  1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr. SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
  2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr. SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya CHADEMA na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa CHADEMA.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
  3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr. Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr. Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
  4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.

Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR. SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA kwa kupanga na kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka CHADEMA, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR. SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa JamiiForums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU………. INAHUZUNISHA..!

Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na CHADEMA ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa CHADEMA wamekana kumtambua LUDOVICK, ni USALITI KIASI GANI HUU..?

Mawakili wote watano ambao ni:-

  1. MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  2. ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  3. NYARONYO KICHERE
  4. TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
  5. PETER KIBATALA

Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? Ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea CHADEMA, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.

ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.

Na wewe ufikirie mwisho wako huko kuliko sasa, ungebaki neutral bila chama Kidogo ningekuelewa, kumbuka vita ya ukombozi c lelemama kama unavyofikiri lazima kwenye mapambano hawakosekani watu kama nyie
 
Kabla ya yote ningependa kuanza na maneno yafuatayo ya Utangulizi wa hiki ninachotaka kukisema hapa kama ifuatavyo:

USALITI;
Usaliti ni neno pana sana...,
Lina madhara mengi sana...,
Hujuma hukwamisha mambo mengi sana...,
Tamaa huzaa usaliti...,
Usaliti huleta maumivu kwa waliokuamini...!

Baada ya Utangulizi huo naomba sasa nieleze vipi ninavyomfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA nikishabihisha ufahamu wangu huo kwake na matukio yanayoendelea hivi sasa.

Katika mfululizo wa matukio yanayoendelea hapa nchini hasa yanayogusa medani za siasa za ndani ya nchi pamoja na jamii kwa ujumla wake, katika yote lipo tukio moja ambalo ni kubwa na lenye sura ya kuogofya. Kwa kuwa tukio lenyewe lipo katika mchakato wa kimahamakama sitalizungumza bali nitazungumza nje ya Wigo wa kesi hiyo ili nisiingilie hatua za kimahakama na nisivunje sheria za nchi.

Nitakachokisema hapa ni namna tu ambavyo nimewahi kumfahamu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA ambae ni mmoja wa washukiwa wa matukio ya kigaidi.

Nilikutana na LUDOVICK pindi nilipokuwa Mwanafunzi wa Shahada ya kwanza ya Ualimu (BACHELOR OF ARTS WITH EDUCATION "BAED") katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Campus ya DUCE mwaka 2008-9 nikiwa mwanafunzi wa Mwaka wa pili, LUDO akiwa mwaka wa kwanza.

Nikiwa ni miongoni mwa vijana wana mkakati na wapinaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nikiendesha shughuli mbalimbali za kukijenga na kukiimarisha Chama hiko katika maeneo ya Vyuo Vikuu, nikiwa nina wajibu na majukumu ya kuwashawishi vijana kujiunga na CHADEMA na kuwajengea imani na matumaini ya kupata Maisha mzuri na Ajira katika taasisi mbalimbali za kijamii zilizo affiliated na Chama hiko, ndipo nilipokutana na LUDO na kuzungumza nae kisha kuungana pamoja kuijenga CHADEMA. (LUDO akiwa mwaka wa Kwanza akifanya BAED-history & political science).

Harakati zetu ziliendelea kwa mafanikio ambapo tulikuwa tukipanga na kufanikisha mikakati mbalimbali ya kuandaa matukio na mijadala ambayo tulialika vongozi wakuu wa CHADEMA kuja kuzungumza issues mbalimbali za kitaifa na kichama. Katikati ya Mwaka 2009 nilipata wazo la kuanzisha Jumuiya ya wanafunzi chini ya CHADEMA, ambapo CHASO ilizaliwa, nikiwa ni muasisi na "mwanzilishi pekee" wa Jumuiya hiyo ya CHADEMA STUDENTS ORGANISATION (CHASO), Ilianza kazi rasmi ya kuwaweka pamoja wanafunzi wanachama wa CHADEMA mimi nikiwa ni MWENYEKITI wa kwanza wa jumuiya hiyo.

Tulipata mafanikio makubwa kwani tuliweza kuwashawishi wanafunzi wengi kujiunga na Chadema, haya tuliyafanya PAMOJA. Hata ilipofika mwaka 2010 niling'atuka kama Mwenyekiti na kuiacha jumuiya hiyo katika mikono salama ya LUDOVICK, ambapo aliendelea nayo jumuiya mpaka Mwaka 2011, alipokuwa Mwaka wa Mwisho naye alikabidhi Uenyekiti kwa Peter John shughuli ambayo ilifanyika katika Ukumbi wa TTC Chang'ombe na mgeni rasmi alikuwa ni Dr. Slaa ambapo aliambatana na Dr. Azaveli Lwaitama-mhadhiri wa UDSM.

Baada ya kuhitimu chuo, LUDO alikuja Makao Makuu ya CHADEMA kama Volunteer ambapo alijumuika tena na volunteer wengine (mimi nikiwemo tangu mwaka 2008) ambapo LUDO alipewa kazi ya kupambana ndani ya mitandao ya kijamii.

Ilipofika Mwanzoni mwa Mwaka 2012, LUDO alikuwa amepangiwa TABORA kama Mwalimu wa Sekondari ambapo LUDO alikwenda kuanza maisha mapya ya kufundisha, ambapo Mwezi mmoja tu baadae Dr. Slaa alimuita arudi Makao Makuu na kumuweka katika Idara ya Ulinzi na Usalama, Chini ya WILFRED LWAKATARE.

Nitaeleza kwa ufupi kwanini Dr. Slaa alimpa LUDO kazi hiyo:-

  1. LUDOVICK alisoma shule ya seminary na pia alisoma masomo ya Uchungaji kwa miaka minne, hivyo alikuwa ni mtiifu sana kwa Dr. SLAA na pia aliamini amesoma kwa undani mafunzo ya kutunza siri na uaminifu.
  2. Pia LUDO alikuwa akiwa ni mtu anayepeleka taarifa kwa Dr. SLAA kuhusu viongozi wengine ndani ya CHADEMA na pia alikuwa akitumika katika mitandao ya kijamii kuwashughulikia viongozi wengine wa CHADEMA.(Pindi alipokuwa kitengo cha mitandao ya Kijamii)
  3. Credit nyingine aliyoipata kwa Dr. Slaa ni pale alipopeleka majina ya wagombea wa BAVICHA ambao wamekataa kutumika na Dr. Slaa (Mimi nikiwemo) na kupelekea majina yetu kuenguliwa, Uchaguzi wa BAVICHA uliofanyika pale ukumbi wa P.T.A Sabasaba.
  4. Lakini pia LUDO aliaminika pia na LWAKATARE kwa kuwa walitoka Mkoa mmoja wa Kagera.

Hivyo, Mwaka 2012 LUDO alikuwa miongoni mwa frontline Undercover katika chaguzi mbalimbali, ambapo alitumikia pia kama afisa usalama wa Viongozi wa Juu wa Chama, ambapo aliongozana na DR. SLAA kama mlinzi wake kuelekea kwenye Uchaguzi wa JIMBO la UZINI kule ZANZIBAR.

Aliendelea na nafasi yake hiyo katika Kurugenzi ya Ulinzi na Usalama ya CHADEMA kwa kupanga na kufanikisha mikakati mbalimbali, ambapo nilikutana nae Big Brother mwanzoni mwa Mwaka huu, alikuwa anatoka PACIFIC HOTEL akaniambia kuwa ametoka MBOZI MAGHARIBI ambako alikwenda kuchunguza kama DAVID SILINDE anakubalika jimboni kwake, na hata ilipotokea sakata lililopelekea Mimi na SHONZA na wengineo kuondoka CHADEMA, LUDOVICK ndiye mtu aliyetumwa kwenda MBEYA akiwa na maagizo kutoka kwa DR. SLAA ya kumfukuza UANACHAMA baba yangu Mzazi (MZEE MWAMPAMBA ambae nae alikuwa ni mwanachama wa CHADEMA) na ndiye aliyekuja hapa JamiiForums (JF) kuweka post yenye barua za kufukuzwa kwa Mzee Mwampamba.

PAMOJA NA HAYA YOTE NA MENGINE AMBAYO AMEIFANYIA CHADEMA AMBAYO MIMI SIYAJUI, VIONGOZI WA CHADEMA WANAKANA KUMFAHAMU………. INAHUZUNISHA..!

Nimeshtushwa sana na Taarifa nilizoziona kwenye vyombo vya habari, juu ya Dr SLAA kukana kuwa hamfahamu wala hajawahi kumsikia na kufanya nae kazi yeyote NDUGU yangu LUDOVICK JOSEPH RWEZAURA.

Lakini si hilo tu bali pia Mawakili ambao wamewekwa na CHADEMA ambao idadi yao ni watano, wakiwemo (katika mawakili hao) viongozi waandamizi wa CHADEMA wamekana kumtambua LUDOVICK, ni USALITI KIASI GANI HUU..?

Mawakili wote watano ambao ni:-

  1. MABERE MARANDO-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  2. ABDALLAH SAFARI-MJUMBE WA KAMATI KUU CHADEMA
  3. NYARONYO KICHERE
  4. TUNDU LISSU-MNADHIMU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI
  5. PETER KIBATALA

Kwanini wasigawanywe hawa au wote katika hawa hawamtetei LUDO..? Ama kama si hawa kwanini hawatafutwi mawakili wengine kwa ajili ya LUDO na badala yake akaachwa anaangamia pamoja na kujitolea kote kuijenga na kuitetea CHADEMA, pamoja na utiifu wote wa kuwalinda na kutunza siri za viongozi na siri za Chama hicho.

ANGALIZO:
Napenda pia kukumbusha kuwa katika umasikini mbaya ni kufikiri chini ya kiwango au utumwa mbaya ni kuruhusu wengine wafikiri kwa ajili yako nawe uwe mfuata mkumbo na upepo wa mawazo yao.

Naomba vijana wenzangu mfikiri kwa kina juu ya haya yaliyompata LUDOVICK na mjifikirie hatma yenu ndani ya chama na maisha katika ujumla wake.[/QUOT

Mtela Mwampamba unaifahamu kurugenzi ya ulinzi na usalama ya chadema kweli? Bila shaka huifahamu. Kurugenzi hii imewahi kuongozwa na marehemu Eugen Gaspar Magaga ambaye baadaye alisaliti na kuhamia CCM kama ulivyo fanya wewe na huyo unayemtetea.Matendo aina hii(ya usaliti) hutokea duniani kote .Kwa wanaojua shughuli hizi kazi inayofuatia huwa ni kudhibiti Madhara yanayotokana na usaliti au matendo ya wasaliti. Bila shaka tunafanya vema katika kudhibiti hujuma zenu.Tuliweza kwa Dr Aman Warlid Kaburu hakika na ninyi tunawamudu.

Ni dhahiri sasa wafu wanawazika wafu wenzao,endeleeni kuzikana!!!!!!!
​
 
Mtela Mwampamba umeonyesha udhaifu mkubwa ambao hata hao CCM hawata kuamini, kila chama kin strategy zake za kujiendesha. Na kama CDm kisipo kuwa na strategy zozote za kujilinda na kutunza siri zake, leo kisingekuwa na hadhi yoyote katika jamii. CCM ni mamafia, ukiendesha chama cha kupambana na CCm kama hakina mbinu za kujilinda na kujitanua, CCM watakifanyia kitu mbaya mpaka kinasambaratika kama vilivyo sambaratika NCCR, CUF na UDP.

CDM wako sahihi kwa sababu ina viongozi makini na wanao ifahamu vizuri CCM amabyo wanapambana nayo. CDM ina wachukua vijana kama ninyi akina Mtela, Ludo nk ili iwapike na kuwafunza namna ya kuendesha mapambano dhidi ya wadhalimu LAKINI mnaokuwa DHAIFU na kupeleka siri CCM, nayo inawatumia kukihujumu chama chenu kwa vijipesa vichafu nanyi mnakubali.

Mtu kama wewe ni wakuogopwa kama ukoma kwani unaongea matope ili kudhihilisha UDHAIFU WAKO katika kutunza siri za taasisi yako. Kama uliamua kuhama , wewe nenda kaanze upya, achana na mambo ya CDM. Ukiendelea hivyo hata hao waliokutuma HAWATAKUAMINI, watakutumia kama kondomu, ukimaliza kazi hiyo wanakugeukia na KUKUFUTILIA mbali unapotea milele, hiyo ndiyo kanuni za intelijensia zinavyokwenda. Endelea kuonyesha udhaifu wako baadaye utaona watakavyokufanya.
 
haya mambo ni makubwa na ni ya giza..kwa akili ya haraka haraka unaweza usiamini macho yako lakini ndio uharamia wa siasa za leo
 
Mtela Mwampamba umeonyesha udhaifu mkubwa ambao hata hao CCM hawata kuamini, kila chama kin strategy zake za kujiendesha. Na kama CDm kisipo kuwa na strategy zozote za kujilinda na kutunza siri zake, leo kisingekuwa na hadhi yoyote katika jamii. CCM ni mamafia, ukiendesha chama cha kupambana na CCm kama hakina mbinu za kujilinda na kujitanua, CCM watakifanyia kitu mbaya mpaka kinasambaratika kama vilivyo sambaratika NCCR, CUF na UDP.

CDM wako sahihi kwa sababu ina viongozi makini na wanao ifahamu vizuri CCM amabyo wanapambana nayo. CDM ina wachukua vijana kama ninyi akina Mtela, Ludo nk ili iwapike na kuwafunza namna ya kuendesha mapambano dhidi ya wadhalimu LAKINI mnaokuwa DHAIFU na kupeleka siri CCM, nayo inawatumia kukihujumu chama chenu kwa vijipesa vichafu nanyi mnakubali.

Mtu kama wewe ni wakuogopwa kama ukoma kwani unaongea matope ili kudhihilisha UDHAIFU WAKO katika kutunza siri za taasisi yako. Kama uliamua kuhama , wewe nenda kaanze upya, achana na mambo ya CDM. Ukiendelea hivyo hata hao waliokutuma HAWATAKUAMINI, watakutumia kama kondomu, ukimaliza kazi hiyo wanakugeukia na KUKUFUTILIA mbali unapotea milele, hiyo ndiyo kanuni za intelijensia zinavyokwenda. Endelea kuonyesha udhaifu wako baadaye utaona watakavyokufanya.

nimekudharau sana, umetoa povu jingi lakini halina maana..ungejiuliza kwann mtela amemuelezea ludovick anavyomfaham kuliko kumshambulia yeye binafsi...siasa maji taka hii
 
Dah kumbe mkuki ni kwa nguruwe tu, Naona comments nyingi hapa hazitaki kabisa kutoa boriti lililopo kwenye macho yao, taarifa hii naiamini kabisa kutokana na kua chili source ya habari hii ni valid and sound mind
 
Wanasiasa wote wenzao ni wale wanaowatunzia maslahi yao. na urafiki unamalizika pale huduma kwao hahitajiki. Luddo ni muhanga au pengine liliotendwa lazima liepukwe lisije likaonyesha ukweli.
 
ludovick ni chadema na chadema ni ludovick, huo ndio ukweli
 
Back
Top Bottom