Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwalimu mtu wa watu (6)

Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwalimu mtu wa watu (6)

Sasa kama wewe hauna dini kwanini ushabikie wenye dini zao?

Walikuingilia wewe kwa kutokuwa na dini? Walikuuliza lolote lililokukwaza?

Marehemeu Nyerere alikuwa na dini au huelewi hilo? Na waliomakaribisha Dar walikuwa na dini au nalo huelewi pia?

Wewe pilipili iko shamba inakuwashia nini?
Sasa dini za watu zinahusika nini na harakati za kupigania uhuru? Kwani wakoloni walikuwa wanaangalia dini ya mtu katika kudai uhuru?
 
Mwinyi na Kikwete walikuwepp katika harakati za kudai Uhuru?

Waislam wanadai kuwa CCM kimekuwa chama cha kanisa kikifanya maamuzi kwa maslahi ya Ukristo.

Je CCM ilikuwepo wakati wakupigania uhuru?

Waislam wameshapambana na askari mara kadhaa na damu imemwagika.

Hawa waliopambana na askari baada ya uhuru na kumwaga damu umeelewa?

Je hapa Mzee Mohamed Said anaonglea wapigania uhuru? Kama unavotaka kupotosha?
👇👇

Waislam wanadai kuwa CCM kimekuwa chama cha kanisa kikifanya maamuzi kwa maslahi ya Ukristo.
Waislam wameshapambana na askari mara kadhaa na damu imemwagika
.
 
Kumbe wenyewe kwa wenyewe mnafanyiana fitna!?
Umeongelea kuhusu Zanzibar, wasome Wazanzibari wameandika nini kuhusu Malima...

Barua ya Marehemu Malima yafichuwa aliyotendewa na JK
Zanzibar Daima
Zanzibar Daima
2 years ago
1495384127513.jpg

Visa na vitimbi vilivyozuka

vilivyozuka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 vinashabihiana sana na kile kilichotokea miaka 20 nyuma wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi wa kwanza tangu kurejeshwa tena kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inafichuwa barua iliyoandikwa na Marehemu Profesa Kighoma Ali Malima wakati huo.

Miongoni mwa mambo yanayoshabihiana mno ni ushiriki wa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye mwaka 1995 alikuwa mmoja wa waliowania tiketi ya CCM kugombea urais wa nchi, na ambaye pia alikuwa mrithi wa Profesa Malima kwenye nafasi ya uwaziri wa fedha.

Profesa Malima alijivua nyadhifa zake zote kwenye baraza la mawaziri la Rais Ali Hassan Mwinyi, kwa kile anachokieleza kwenye barua yake ya kuomba kujiuzulu kuwa ni kukiukwa kwa maadili ya utawala na misingi ya uwajibikaji wa pamoja kulikofanywa na Kikwete.

Inafahamika kuwa Profesa Malima, aliyekuja kufariki dunia jijini London, Uingereza, miezi michache baada ya kujiondoa serikalini na kutangaza kuwania urais kupitia chama kipya cha kisiasa, aliwahi kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM na nje yake, kutokana na kujipambanua kwake kama msomi na msemaji wa ngome kuu ya CCM – jamii ya Kiislamu.

Mbele ya Profesa Malima, kwa hivyo, wagombea akina Kikwete wasingelikuwa na pa kupenyea, lakini kile kinachoonekana kama hujuma dhidi yake iliyoongozwa na wenziwe, ilimporomoa na mapema na hivyo kuiporomosha ndoto yake ya kuwa rais wa Tanzania kupitia CCM.

Ingawa wengine wanasema kuwa lawama za kuporomoka kwa Profesa Malima zinamuangukia pia Rais Mwinyi, mzawa mwenziwe wa Mkuranga, kutokana na udhaifu mkubwa aliouonesha kiuongozi, lakini njama za kundi la vijana wa wakati huo zina nafasi kubwa sana.

Historia ilijirejea tena kwa Kikwete, miaka 20 baadaye, sasa akiwa rais wa nchi, amiri jeshi mkuu na mwenyekiti wa chama tawala, pale aliposimamia mkutano uliowang’oa wagombea kadhaa mashuhuri ndani ya CCM, akiwemo aliyewahi kuwa swahibu wake wa chanda na pete, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.

Chanzo: Barua ya Marehemu Malima yafichuwa aliyotendewa na JK
 
Zanzibar huifahamu dada. Ni heri uongee unayoyafahamu.
Nisiifahamu kwa lipi, halafu ni kaka, jibu hoja za huo ubaguzi mnaoulilia ni upi maana huwa mnanafasi lkn hatuoni mabadiliko ya hayo mnayolilia kupitia viongozi wa kiislamu mnaowapata au malalamiko yenu ni ya mtu mmoja siyo ya ujumla na mbona viongozi wenu wa Bakwata hawayasemi kama ni ya kweli maana wao huomba kujengewa misikiti
 
Maustadhi mna vituko sana, fanyeni kazi, nendeni shuleni, madrasa siyo chuo.
Ndugu yangu unatufundisha tulichowafundisha. Ajabu kubwa sana.

Unataka kutufundisha kuhusu kusoma? Unaelewa kuwa neno la kwanza lililoshuka katika Qur'an ni "SOMA"?

Labda utuulize nini kimetusibu mpaka leo hii tunaonekana sisi hatusomi.
 
Watu wa dini zote hapa nchini wanaishi kwa uhuru na amani yote .....wana haki zote bila kubagua nani ni dini gani...

Sasa haya maporojo ya dini moja kuonesha kubagulia yanatokana na nin,,?
Unless anaebaguliwa alete ushahidi hapa!? Alibaguliwa/ au kuonewa na nani, kivipi, na wapi?
 
Ndugu yangu unatufundisha tulichowafundisha. Ajabu kubwa sana.

Unataka kutufundisha kuhusu kusoma? Unaelewa kuwa neno la kwanza lililoshuka katika Qur'an ni "SOMA"?

Labda utuulize nini kimetusibu mpaka leo hii tunaonekana sisi hatusomi.
naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??
 
Nisiifahamu kwa lipi, halafu ni kaka, jibu hoja za huo ubaguzi mnaoulilia ni upi maana huwa mnanafasi lkn hatuoni mabadiliko ya hayo mnayolilia kupitia viongozi wa kiislamu mnaowapata au malalamiko yenu ni ya mtu mmoja siyo ya ujumla na mbona viongozi wenu wa Bakwata hawayasemi kama ni ya kweli maana wao huomba kujengewa misikiti
Samahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.

Naomba sikiliza hii, labda utatuelewa...
naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??
 
Huyu mzee hana faida kwa hii Nchi,mimi nimeishi visiwani
Lakini chuki aliyonayo huyu mleta mada kwa wakristo ni mbaya sana Kuliko hata watu wa visiwani ambao wakristo ni digt moja

Acha chuki dhidi ya Nyerere na wakristo
Wafunze vijana wako na wafuasi wako upendo wacha chuki
 
Hivi waislamu mmebaguliwa wapi mbona lawama nyingi sana maana kuanzia awamu ya nne mpk hii mna viongozi wakubwa kwenye uongozi wa juu, awamu ya nne 3 Rais, makamu wa Rais walikuwa waislamu achia mbali wengine na huko Zanzibar wakristo walikuwa na waziri Mkuu tu lkn hatukusikia malalamiko ya wakristo. Awamu hii ambayo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wote ni waislamu lkn bado mnalia sasa shida nini

Mnataka nchi yote viongozi muwe nyie ndiyo nyoyo zenu zifurahi mbona huko Zanzibar viongozi karibia wote ni waislamu japo wakristo wapo lkn hatusikii wakilalamikia hilo na mnawaminya kweli lkn wametulia lkn huku kila siku malalamiko mnabaguliwa acheni zenu sote ni wamoja tuishi kwa amani
Halafu hapo bado wao ndio wachache Tz, nashangaa Waislam ndio wangekuwa na idadi kama ya Wakristo Tz na Wakristo ndio wawe kwachache kama Waislam walivyo sasa hivi. Sijui ingekuwaje
 
Ukifuatilia hizi sarakasi zoote kuna mambo ya kujifunza kuhusu Mwalimu.

Kwamba ilihitajika busara kubwa sana kupita njia aliyopita Mwalimu, ni dhahiri kuwa hapa Mwalimu ndiye anahitaji pongezi kubwa kukaa na Wazee.

Malalamiko ya hawa Ndugu hayakuanza leo au jana, ni tangu siku hizo...ni dhahiri kwamba ilihitajika akili ya hali ya juu sana kupita alipopita Mwalimu.

Juzi nimemsikia Mzee Pius akisema Mwalimu ndiye aliyei transform TAA kuwa chama cha siasa, hii ina make a lot of sense kwangu...harakati za waanzilishi wa AA mpaka TAA hazikuwa za kisiasa na nachelea kusema zilikuwa ni za kidini zaidi.

Na ndio maana hata majaribio yao kadhaa ya kukimbilia UNO yaligonga ukuta, Mzee Said amedai hajui lolote kuhusu hili. Rejea maneno ya Mzee Bilal, ambaye Mzee Saidi anamtaja kama Baba yake, ingawa sijamsikia akikanusha maneno ya Mzee wake...basi Mzee Said aseme "msimsikilize huyo hajui anachosema"

Maandiko mengi ni kama mnaonyesha tu kwamba kila kitu kilienda kiulaini tu kwa Mwalimu na Wazee wa Dar, ila kiukweli kwa yeyote mwenye akili zake timamu wala hawezi kudhani kirahisi hivyo, na wala Mzee Said and co hawawezi kukuelezea ya upande huo.

Katika sehemu ya maelezo ya Mwalimu aliwahi kuelezea namna alivyoishi na kushirikiana na Wazee wa Dar, ingawa kina Mzee saidi mara zote huishia tu kwa kuwataja wachache kama kina Sykes, ambao pia amekiri kuwa na nasaba nao...ila Mwalimu mara nyingi anawataja Wazee zaidi ya kina Dosa, Sykes n.k, na wala kina Sykes hawakuwa Wazee kwa wakati huo.

Mwalimu amesikika akisema namna alivyolazimika kushiriki "Dua" za Wazee/Wenyeji wake, na tusidhani hili ni jambo rahisi rahisi tu haswa kwa Mtu asiyeamini/mwenye imani tofauti na hayo, na sehemu kubwa ya haya ilikuwa ni 'shirki' ....ilikuwa ni vigumu sana kwa Mwalimu kujiweka mbali na imani za Wazee wake wale, Mwalimu ameelezea hata namna alivyolazimika kwenda makaburini n.k, Wazee na imani zao sasa angefanyeje?.

Kiufupi ni kwamba mambo hayakuwa 'smooth' kama wanavyojaribu kutulisha Waandishi wa kaliba ya Mzee Said, Mwalimu alikuwa na wakati mgumu sana kupita na kufika alikofikia.
 
Halafu hapo bado wao ndio wachache Tz, nashangaa Waislam ndio wangekuwa na idadi kama ya Wakristo Tz na Wakristo ndio wawe kwachache kama Waislam walivyo sasa hivi. Sijui ingekuwaje
Ooh. Weka ushahidi wa uliyoyaandika.
 
Ukifuatilia hizi sarakasi zoote kuna mambo ya kujifunza kuhusu Mwalimu.

Kwamba ilihitajika busara kubwa sana kupita njia aliyopita Mwalimu, ni dhahiri kuwa hapa Mwalimu ndiye anahitaji pongezi kubwa kukaa na Wazee.

Malalamiko ya hawa Ndugu hayakuanza leo au jana, ni tangu siku hizo...ni dhahiri kwamba ilihitajika akili ya hali ya juu sana kupita alipopita Mwalimu.

Juzi nimemsikia Mzee Pius akisema Mwalimu ndiye aliyei transform TAA kuwa chama cha siasa, hii ina make a lot of sense kwangu...harakati za waanzilishi wa AA mpaka TAA hazikuwa za kisiasa na nachelea kusema zilikuwa ni za kidini zaidi.

Na ndio maana hata majaribio yao kadhaa ya kukimbilia UNO yaligonga ukuta, Mzee Said amedai hajui lolote kuhusu hili. Rejea maneno ya Mzee Bilal, ambaye Mzee Saidi anamtaja kama Baba yake, ingawa sijamsikia akikanusha maneno ya Mzee wake...basi Mzee Said aseme "msimsikilize huyo hajui anachosema"

Maandiko mengi ni kama mnaonyesha tu kwamba kila kitu kilienda kiulaini tu kwa Mwalimu na Wazee wa Dar, ila kiukweli kwa yeyote mwenye akili zake timamu wala hawezi kudhani kirahisi hivyo, na wala Mzee Said and co hawawezi kukuelezea ya upande huo.

Katika sehemu ya maelezo ya Mwalimu aliwahi kuelezea namna alivyoishi na kushirikiana na Wazee wa Dar, ingawa kina Mzee saidi mara zote huishia tu kwa kuwataja wachache kama kina Sykes, ambao pia amekiri kuwa na nasaba nao...ila Mwalimu mara nyingi anawataja Wazee zaidi ya kina Dosa, Sykes n.k, kina Sykes hawakuwa Wazee kwa wakati huo.

Mwalimu amesikika akisema namna alivyolazimika kushiriki "Dua" za Wazee/Wenyeji wake, tusidhani hili ni jambo rahisi rahisi tu haswa kwa Mtu asiyeamini/mwenye imani tofauti na hayo, na sehemu kubwa ya haya ilikuwa ni 'shirki' ....ilikuwa ni vigumu sana kujiweka mbali na imani za Wazee, Mwalimu ameelezea namna walivyoenda makaburini n.k.

Kiufupi ni kwamba mambo hayakuwa 'smooth' kama wanavyojaribu kutulisha Waandishi wa kaliba ya Mzee Said, Mwalimu alikuwa na wakati mgumu sana kupita na kufika alikofikia.

Pius Msekwa alikuwepo wakati wa TAA wa kudai Uhuru? Hata kwenye walioanzisha TANU hayumo. Weka ushahidi kama unao. Juzi watu wamemjibu porojo zake. Soma...

Back
Top Bottom