May Day
JF-Expert Member
- May 18, 2018
- 6,311
- 9,027
Hata kama hakuwepo, mimi nime refer kwa sababu nilimsikiliza akisema hayo, na wala hiyo sio hoja ya msingi hapa.Pius Msekqa alikuwepo wakati wa kudai Uhuru? Weka ushahidi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata kama hakuwepo, mimi nime refer kwa sababu nilimsikiliza akisema hayo, na wala hiyo sio hoja ya msingi hapa.Pius Msekqa alikuwepo wakati wa kudai Uhuru? Weka ushahidi.
Hata akizua we kwako sawa mradi umemsikia akisema? Hutaki kuufahamu ukweli?Hata kama hakuwepo, mimi nime refer kwa sababu nilimsikiliza akisema hayo, na wala hiyo sio hoja ya msingi hapa.
Huo ndio ukweli, muache propaganda zenu.Hata akizua we kwako sawa mradi umemsikia akisema? Hutaki kuufahamu ukweli?
Ukweli ni huu hapa, wacha kujazwa ujinga ukajazika. Ndiyo maana hamuendelei kwa kujazwa ujinga ukawajaa. Soma...Huo ndio ukweli, muache propaganda zenu.
I got you, lakini hakuna malaika wa kike,wote ni wa kiumeSamahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.
Naomba sikiliza hii, labda utatuelewa...
Alafu huu muda wa Masjid wewe bado unarandaranda humu, Mzee Said huwezi mkuta ana comment mida hii.Ukweli ni huu hapa, wacha kujazwa ujinga ukajazika. Ndiyo maana hamuendelei kwa kujazwa ujinga ukawajaa. Soma...
Mzee Pius Msekwa haifahamu historia ya TANU
MZEE PIUS MSEKWA HAIFAHAMU HISTORIA YA TANU Katika gazeti la Tazama la leo tarehe 14 Oktoba 2019 kuna makala iliyoandikwa na Pius Msekwa yenye kichwa cha habari, ‘’Mwalimu Nyerere kama nilivyomfahamu (2),’’ ambamo ameandika maneno haya yafuatayo kuhusu Mwalimu Nyerere kuwa: ‘’...alifanikiwa...www.jamiiforums.com
Siongelei malaika. Naongelea jina Angel (given name) ambalo kwa hapo Tanzania ninawafahamu wanawake wengi tu wanaitwa hivyo, sijawahi muona mwanamme wa Kitanzania akiitwa Angel labda Angelo.I got you, lakini hakuma malaika wa kike,wote ni wa kiume
Wewe unaujuwa muda wa Masjid au unakurupuka tu? Kwa kukujuza tu, duniani, hakuna muda ambao siyo wa Masjid.Alafu huu muda wa Masjid wewe bado unarandaranda humu, Mzee Said huwezi mkuta ana comment mida hii.
Samahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.
Naomba sikiliza hii, labda utatuelewa...
Savimbi Jr,Sasa dini za watu zinahusika nini na harakati za kupigania uhuru? Kwani wakoloni walikuwa wanaangalia dini ya mtu katika kudai uhuru?
Ukifuatilia hizi sarakasi zoote kuna mambo ya kujifunza kuhusu Mwalimu.
Kwamba ilihitajika busara kubwa sana kupita njia aliyopita Mwalimu, ni dhahiri kuwa hapa Mwalimu ndiye anahitaji pongezi kubwa kukaa na Wazee.
Malalamiko ya hawa Ndugu hayakuanza leo au jana, ni tangu siku hizo...ni dhahiri kwamba ilihitajika akili ya hali ya juu sana kupita alipopita Mwalimu.
Juzi nimemsikia Mzee Pius akisema Mwalimu ndiye aliyei transform TAA kuwa chama cha siasa, hii ina make a lot of sense kwangu...harakati za waanzilishi wa AA mpaka TAA hazikuwa za kisiasa na nachelea kusema zilikuwa ni za kidini zaidi.
Na ndio maana hata majaribio yao kadhaa ya kukimbilia UNO yaligonga ukuta, Mzee Said amedai hajui lolote kuhusu hili. Rejea maneno ya Mzee Bilal, ambaye Mzee Saidi anamtaja kama Baba yake, ingawa sijamsikia akikanusha maneno ya Mzee wake...basi Mzee Said aseme "msimsikilize huyo hajui anachosema"
Maandiko mengi ni kama mnaonyesha tu kwamba kila kitu kilienda kiulaini tu kwa Mwalimu na Wazee wa Dar, ila kiukweli kwa yeyote mwenye akili zake timamu wala hawezi kudhani kirahisi hivyo, na wala Mzee Said and co hawawezi kukuelezea ya upande huo.
Katika sehemu ya maelezo ya Mwalimu aliwahi kuelezea namna alivyoishi na kushirikiana na Wazee wa Dar, ingawa kina Mzee saidi mara zote huishia tu kwa kuwataja wachache kama kina Sykes, ambao pia amekiri kuwa na nasaba nao...ila Mwalimu mara nyingi anawataja Wazee zaidi ya kina Dosa, Sykes n.k, na wala kina Sykes hawakuwa Wazee kwa wakati huo.
Mwalimu amesikika akisema namna alivyolazimika kushiriki "Dua" za Wazee/Wenyeji wake, na tusidhani hili ni jambo rahisi rahisi tu haswa kwa Mtu asiyeamini/mwenye imani tofauti na hayo, na sehemu kubwa ya haya ilikuwa ni 'shirki' ....ilikuwa ni vigumu sana kwa Mwalimu kujiweka mbali na imani za Wazee wake wale, Mwalimu ameelezea hata namna alivyolazimika kwenda makaburini n.k, Wazee na imani zao sasa angefanyeje?.
Kiufupi ni kwamba mambo hayakuwa 'smooth' kama wanavyojaribu kutulisha Waandishi wa kaliba ya Mzee Said, Mwalimu alikuwa na wakati mgumu sana kupita na kufika alikofikia.
[/QUOTE
May Day,
Siwezi kukujibu yote uliyosema ila nitajikita kwa Mzee Pius Msekwa na historia ya TANU.
Mimi sina tatizo na historia rasmi kama alivyoeleza Mzee Msekwa kwani hii tunayo miaka yote na inasomeshwa katika mtaala kuanzia shule ya msingi hadi Chuo Kikuu.
Mimi ninachofanya ni kusahihisha pale ninapoona ukweli haujaelezwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na si lazima niaminike inatosha tu kwangu kueleza ukweli kama niujuavyo.
Pius Msekwa alikuwepo wakati wa TAA wa kudai Uhuru? Hata kwenye walioanzisha TANU hayumo. Weka ushahidi kama unao. Juzi watu wamemjibu porojo zake. Soma...
Mzee Pius Msekwa haifahamu historia ya TANU
MZEE PIUS MSEKWA HAIFAHAMU HISTORIA YA TANU Katika gazeti la Tazama la leo tarehe 14 Oktoba 2019 kuna makala iliyoandikwa na Pius Msekwa yenye kichwa cha habari, ‘’Mwalimu Nyerere kama nilivyomfahamu (2),’’ ambamo ameandika maneno haya yafuatayo kuhusu Mwalimu Nyerere kuwa: ‘’...alifanikiwa...www.jamiiforums.com
Tajiri...naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??
Jeki,Maustadhi mna vituko sana, fanyeni kazi, nendeni shuleni, madrasa siyo chuo.
kumbe hujawahi kuona,pole sanaSiongelei malaika. Naongelea jina Angel (given name) ambalo kwa hapo Tanzania ninawafahamu wanawake wengi tu wanaitwa hivyo, sijawahi muona mwanamme wa Kitanzania akiitwa Angel labda Angelo.
Pole sana.
Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.Tajiri...
Hebu soma hayo hapo chini:
Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.
Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.
Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.
Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.
Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.
Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ''washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.
Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake ni madras. Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.
Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.
Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.
Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.
Kati ya mwaka 1888-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.
Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza.
Hivi sasa kuna propaganda kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.
Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.
Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja Kanisa likaelekeza nguvu zake katika katika kuwatayarisha raia ambao wengi wao walikuwa Wakristo, watakaokuwa watiifu kwa Kanisa na serikali.
Ni katika mtandao huu ndiyo hii leo unaona Waislam wako nyuma na wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hujma dhidi yao.
Bahati mbaya hili ni tatizo ambalo linatisha sana serikali na hivyo kuogopa kuliweka katika agenda ya matatizo ya jamii yetu.
Adolay,Kama kuongea haya mambo sharti uwe
1. Mpigania uhuru ....TAA na TANU
2. Ulikuwepo kwenye harakati za uhuru
3. Kuwepo ndani ya TAA na TANU
4. Kufaham historia.....sijuwi ufaulu ni upi?
Basi wewe na Mzee Mohamed pia kaeni kimya.
Pole wewe nilie kudhania wa kike kwa ID yako, kumbe wa kiume.kumbe hujawahi kuona,pole sana
Tajiri,Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.
ilikuaje wakafundisha shule za kikristo na walikuwa wanajua kuandika kiarabu tu