Savimbi Jr
JF-Expert Member
- Sep 23, 2011
- 6,818
- 9,183
Sasa dini za watu zinahusika nini na harakati za kupigania uhuru? Kwani wakoloni walikuwa wanaangalia dini ya mtu katika kudai uhuru?Sasa kama wewe hauna dini kwanini ushabikie wenye dini zao?
Walikuingilia wewe kwa kutokuwa na dini? Walikuuliza lolote lililokukwaza?
Marehemeu Nyerere alikuwa na dini au huelewi hilo? Na waliomakaribisha Dar walikuwa na dini au nalo huelewi pia?
Wewe pilipili iko shamba inakuwashia nini?
Mwinyi na Kikwete walikuwepp katika harakati za kudai Uhuru?
Waislam wanadai kuwa CCM kimekuwa chama cha kanisa kikifanya maamuzi kwa maslahi ya Ukristo.
Waislam wameshapambana na askari mara kadhaa na damu imemwagika.
Waislam wanadai kuwa CCM kimekuwa chama cha kanisa kikifanya maamuzi kwa maslahi ya Ukristo.
Waislam wameshapambana na askari mara kadhaa na damu imemwagika.
Ni mtu wa dini sana lakini cha kushangaza ameliwa "BACK" na mwijaku.Hahah daah nasikia 'juzuu' imemkaa kichwani vibaya sana.
Umeongelea kuhusu Zanzibar, wasome Wazanzibari wameandika nini kuhusu Malima...
Barua ya Marehemu Malima yafichuwa aliyotendewa na JK
Zanzibar Daima
2 years ago
Visa na vitimbi vilivyozuka
vilivyozuka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015 vinashabihiana sana na kile kilichotokea miaka 20 nyuma wakati wa kuelekea kwenye uchaguzi wa kwanza tangu kurejeshwa tena kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inafichuwa barua iliyoandikwa na Marehemu Profesa Kighoma Ali Malima wakati huo.
Miongoni mwa mambo yanayoshabihiana mno ni ushiriki wa Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye mwaka 1995 alikuwa mmoja wa waliowania tiketi ya CCM kugombea urais wa nchi, na ambaye pia alikuwa mrithi wa Profesa Malima kwenye nafasi ya uwaziri wa fedha.
Profesa Malima alijivua nyadhifa zake zote kwenye baraza la mawaziri la Rais Ali Hassan Mwinyi, kwa kile anachokieleza kwenye barua yake ya kuomba kujiuzulu kuwa ni kukiukwa kwa maadili ya utawala na misingi ya uwajibikaji wa pamoja kulikofanywa na Kikwete.
Inafahamika kuwa Profesa Malima, aliyekuja kufariki dunia jijini London, Uingereza, miezi michache baada ya kujiondoa serikalini na kutangaza kuwania urais kupitia chama kipya cha kisiasa, aliwahi kuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa ndani ya CCM na nje yake, kutokana na kujipambanua kwake kama msomi na msemaji wa ngome kuu ya CCM – jamii ya Kiislamu.
Mbele ya Profesa Malima, kwa hivyo, wagombea akina Kikwete wasingelikuwa na pa kupenyea, lakini kile kinachoonekana kama hujuma dhidi yake iliyoongozwa na wenziwe, ilimporomoa na mapema na hivyo kuiporomosha ndoto yake ya kuwa rais wa Tanzania kupitia CCM.
Ingawa wengine wanasema kuwa lawama za kuporomoka kwa Profesa Malima zinamuangukia pia Rais Mwinyi, mzawa mwenziwe wa Mkuranga, kutokana na udhaifu mkubwa aliouonesha kiuongozi, lakini njama za kundi la vijana wa wakati huo zina nafasi kubwa sana.
Historia ilijirejea tena kwa Kikwete, miaka 20 baadaye, sasa akiwa rais wa nchi, amiri jeshi mkuu na mwenyekiti wa chama tawala, pale aliposimamia mkutano uliowang’oa wagombea kadhaa mashuhuri ndani ya CCM, akiwemo aliyewahi kuwa swahibu wake wa chanda na pete, Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa.
Chanzo: Barua ya Marehemu Malima yafichuwa aliyotendewa na JK
Na uno amelikata fresh kabisaa.Ni mtu wa dini sana lakini cha kushangaza ameliwa "BACK" na mwijaku.
Nisiifahamu kwa lipi, halafu ni kaka, jibu hoja za huo ubaguzi mnaoulilia ni upi maana huwa mnanafasi lkn hatuoni mabadiliko ya hayo mnayolilia kupitia viongozi wa kiislamu mnaowapata au malalamiko yenu ni ya mtu mmoja siyo ya ujumla na mbona viongozi wenu wa Bakwata hawayasemi kama ni ya kweli maana wao huomba kujengewa misikitiZanzibar huifahamu dada. Ni heri uongee unayoyafahamu.
Maustadhi mna vituko sana, fanyeni kazi, nendeni shuleni, madrasa siyo chuo.Unaonesha hata mada hujaisoma. Unasikitisha sana.
Ndugu yangu unatufundisha tulichowafundisha. Ajabu kubwa sana.Maustadhi mna vituko sana, fanyeni kazi, nendeni shuleni, madrasa siyo chuo.
ahaaa!!! nilikuwa sijajua, kumbe ni mwalimu wa madrasa?? hapo sio sawa kabisaMwalimu wa madrasa si MENINA?
naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??Ndugu yangu unatufundisha tulichowafundisha. Ajabu kubwa sana.
Unataka kutufundisha kuhusu kusoma? Unaelewa kuwa neno la kwanza lililoshuka katika Qur'an ni "SOMA"?
Labda utuulize nini kimetusibu mpaka leo hii tunaonekana sisi hatusomi.
tuelezee wewe ambaye unaifahamu vizuriZanzibar huifahamu dada. Ni heri uongee unayoyafahamu.
Samahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.Nisiifahamu kwa lipi, halafu ni kaka, jibu hoja za huo ubaguzi mnaoulilia ni upi maana huwa mnanafasi lkn hatuoni mabadiliko ya hayo mnayolilia kupitia viongozi wa kiislamu mnaowapata au malalamiko yenu ni ya mtu mmoja siyo ya ujumla na mbona viongozi wenu wa Bakwata hawayasemi kama ni ya kweli maana wao huomba kujengewa misikiti
naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??
Samahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.
Naomba sikiliza hii, labda utatuelewa...
Halafu hapo bado wao ndio wachache Tz, nashangaa Waislam ndio wangekuwa na idadi kama ya Wakristo Tz na Wakristo ndio wawe kwachache kama Waislam walivyo sasa hivi. Sijui ingekuwajeHivi waislamu mmebaguliwa wapi mbona lawama nyingi sana maana kuanzia awamu ya nne mpk hii mna viongozi wakubwa kwenye uongozi wa juu, awamu ya nne 3 Rais, makamu wa Rais walikuwa waislamu achia mbali wengine na huko Zanzibar wakristo walikuwa na waziri Mkuu tu lkn hatukusikia malalamiko ya wakristo. Awamu hii ambayo Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wote ni waislamu lkn bado mnalia sasa shida nini
Mnataka nchi yote viongozi muwe nyie ndiyo nyoyo zenu zifurahi mbona huko Zanzibar viongozi karibia wote ni waislamu japo wakristo wapo lkn hatusikii wakilalamikia hilo na mnawaminya kweli lkn wametulia lkn huku kila siku malalamiko mnabaguliwa acheni zenu sote ni wamoja tuishi kwa amani
tuelezee wewe ambaye unaifahamu vizuri
Ooh. Weka ushahidi wa uliyoyaandika.Halafu hapo bado wao ndio wachache Tz, nashangaa Waislam ndio wangekuwa na idadi kama ya Wakristo Tz na Wakristo ndio wawe kwachache kama Waislam walivyo sasa hivi. Sijui ingekuwaje
Pius Msekwa alikuwepo wakati wa TAA wa kudai Uhuru? Hata kwenye walioanzisha TANU hayumo. Weka ushahidi kama unao. Juzi watu wamemjibu porojo zake. Soma...Ukifuatilia hizi sarakasi zoote kuna mambo ya kujifunza kuhusu Mwalimu.
Kwamba ilihitajika busara kubwa sana kupita njia aliyopita Mwalimu, ni dhahiri kuwa hapa Mwalimu ndiye anahitaji pongezi kubwa kukaa na Wazee.
Malalamiko ya hawa Ndugu hayakuanza leo au jana, ni tangu siku hizo...ni dhahiri kwamba ilihitajika akili ya hali ya juu sana kupita alipopita Mwalimu.
Juzi nimemsikia Mzee Pius akisema Mwalimu ndiye aliyei transform TAA kuwa chama cha siasa, hii ina make a lot of sense kwangu...harakati za waanzilishi wa AA mpaka TAA hazikuwa za kisiasa na nachelea kusema zilikuwa ni za kidini zaidi.
Na ndio maana hata majaribio yao kadhaa ya kukimbilia UNO yaligonga ukuta, Mzee Said amedai hajui lolote kuhusu hili. Rejea maneno ya Mzee Bilal, ambaye Mzee Saidi anamtaja kama Baba yake, ingawa sijamsikia akikanusha maneno ya Mzee wake...basi Mzee Said aseme "msimsikilize huyo hajui anachosema"
Maandiko mengi ni kama mnaonyesha tu kwamba kila kitu kilienda kiulaini tu kwa Mwalimu na Wazee wa Dar, ila kiukweli kwa yeyote mwenye akili zake timamu wala hawezi kudhani kirahisi hivyo, na wala Mzee Said and co hawawezi kukuelezea ya upande huo.
Katika sehemu ya maelezo ya Mwalimu aliwahi kuelezea namna alivyoishi na kushirikiana na Wazee wa Dar, ingawa kina Mzee saidi mara zote huishia tu kwa kuwataja wachache kama kina Sykes, ambao pia amekiri kuwa na nasaba nao...ila Mwalimu mara nyingi anawataja Wazee zaidi ya kina Dosa, Sykes n.k, kina Sykes hawakuwa Wazee kwa wakati huo.
Mwalimu amesikika akisema namna alivyolazimika kushiriki "Dua" za Wazee/Wenyeji wake, tusidhani hili ni jambo rahisi rahisi tu haswa kwa Mtu asiyeamini/mwenye imani tofauti na hayo, na sehemu kubwa ya haya ilikuwa ni 'shirki' ....ilikuwa ni vigumu sana kujiweka mbali na imani za Wazee, Mwalimu ameelezea namna walivyoenda makaburini n.k.
Kiufupi ni kwamba mambo hayakuwa 'smooth' kama wanavyojaribu kutulisha Waandishi wa kaliba ya Mzee Said, Mwalimu alikuwa na wakati mgumu sana kupita na kufika alikofikia.