Ninavyomkumbuka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, mwalimu mtu wa watu (6)

Pius Msekqa alikuwepo wakati wa kudai Uhuru? Weka ushahidi.
Hata kama hakuwepo, mimi nime refer kwa sababu nilimsikiliza akisema hayo, na wala hiyo sio hoja ya msingi hapa.
 
Hata kama hakuwepo, mimi nime refer kwa sababu nilimsikiliza akisema hayo, na wala hiyo sio hoja ya msingi hapa.
Hata akizua we kwako sawa mradi umemsikia akisema? Hutaki kuufahamu ukweli?
 
Kama kawaida, rejea zinatumika pale unapoona zinaendana na nia zako ila pale unapoona zinakinzana au kukupa ushahidi usiokutosheleza bhasi inakuja simulizi ya yaliyofanyika au uliyopata kuyasikia ukiwa mtoto au kijana mdogo NYUMBANI, SEBULENI, KIBARAZANI au POPOTE PALE kwa wahusika. Hujawahi kwenda kinyume na hapo

Nyerere angekuwa muislamu na kwa hicho kichwa cha habari, bhasi ungeandika kurasa tatu bila kuchoka na kwa ushahidi ila kwa kuwa ni mkristo bhasi imekuja simulizi ambayo hatuna hata hakika nayo ikifuatiwa na malalamiko tupu.
 
Huo ndio ukweli, muache propaganda zenu.
Ukweli ni huu hapa, wacha kujazwa ujinga ukajazika. Ndiyo maana hamuendelei kwa kujazwa ujinga ukawajaa. Soma...
 
Alafu huu muda wa Masjid wewe bado unarandaranda humu, Mzee Said huwezi mkuta ana comment mida hii.
 
I got you, lakini hakuma malaika wa kike,wote ni wa kiume
Siongelei malaika. Naongelea jina Angel (given name) ambalo kwa hapo Tanzania ninawafahamu wanawake wengi tu wanaitwa hivyo, sijawahi muona mwanamme wa Kitanzania akiitwa Angel labda Angelo.
Pole sana.
 
Alafu huu muda wa Masjid wewe bado unarandaranda humu, Mzee Said huwezi mkuta ana comment mida hii.
Wewe unaujuwa muda wa Masjid au unakurupuka tu? Kwa kukujuza tu, duniani, hakuna muda ambao siyo wa Masjid.
 
Samahani sana nilipoona ID ina "angels" nikachukulia ni wa kike. Nisameh sana.

Naomba sikiliza hii, labda utatuelewa...

Kwahiyo na wewe unashabikia walei wachinjwe kama alivyoshauri Late Ilunga?
 
Sasa dini za watu zinahusika nini na harakati za kupigania uhuru? Kwani wakoloni walikuwa wanaangalia dini ya mtu katika kudai uhuru?
Savimbi Jr,
Inabidi kuelewa uhusiano uliokuwapo baina ya wakoloni na wamishionari ili kujua kwa nini historia ya kudai uhuru ilichukua mkondo iliochukua.

Ukijua historia hii utaelewa kwa nini katika harakati za kudai uhuru Waislam walikuwa mbele na kwa nini wenzao hawakujitokeza kwa nguvu.

Katika watafiti wa historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika nimeeleza changamoto zilizojitokeza baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961.
 
 

Kama kuongea haya mambo sharti uwe

1. Mpigania uhuru ....TAA na TANU

2. Ulikuwepo kwenye harakati za uhuru

3. Kuwepo ndani ya TAA na TANU

4. Kufaham historia.....sijuwi ufaulu ni upi?

Basi wewe na Mzee Mohamed pia kaeni kimya.
 
naomba kujua hilo kwa nini mnaonekana hamjasoma??
Tajiri...
Hebu soma hayo hapo chini:

Wajerumani walipofika Tanganyika waliwakuta Waislam wanafahamu kuandika, kusoma na walikuwa wameelimika katika hesabu.

Mmishionari Ludwig Krapf alipofika kwa Chifu Kimweri wa Usambaa mwaka 1848 alimkuta yeye na wanae wote wanajua kusoma.

Herufi walizokuwa wakitumia zilikuwa za Kiarabu.

Wajerumani kwa ajili hii basi waliwaajiri Waislam kama walimu, wakalimani na makarani serikalini.

Wamisionari na wakoloni waliona wivu kwa maendeleo haya waliyoyakuta kwa Waislam.

Kubwa zaidi ni kuwa walikuwa wamekuja kustaarabisha watu ''washenzi'' badala yake wamewakuta watu walistaaarabika na wanye utamaduni wa kupendeza.

Elimu hii yote na utamaduni huu wa hali ya juu ulikuwa unatokana na Uislam na shule zake ni madras. Hapo ndipo zilipoaanza mbinu ya kuvunja maendeleo haya yote.

Herufi za Kiarabu zikapigwa marufuku kutumika na badala yake watu wakalazimishwa kujifunza herufi za Kirumi.

Muislam ambae jana alipoingia kulala alikuwa anaitwa ameelimika akaamka asubuhi yake mjinga, hana elimu, hajui kusoma wala kuandika. Njama hizi zote dhidi ya Uislam ilikuwa sehemu ya makubaliano kama ilivyoandikwa katika kifungu IV cha Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884.

Kifungu hicho kilikuwa kinasema kuwa Ukristo ni lazima ulindwe dhidi ya Uislam.

Kati ya mwaka 1888-1892 katika kutekeleza kifungu hicho kama ilivyokubalika katia Mkutano wa Berlin, Imperial British East Africa Company ilitumia nguvu za kisiasa na kijeshi kuulinda Ukristo katika Afrika ya Mashariki.

Ombwe lililoachwa na elimu ya Kiislam ikajazwa na elimu ya Kanisa chini ya usimamizi wa Waingereza.

Hivi sasa kuna propaganda kuwa Kanisa ndilo lililoweka msingi wa kwanza wa elimu Tanganyika.

Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

Kwa kipindi cha zaidi ya miaka mia moja Kanisa likaelekeza nguvu zake katika katika kuwatayarisha raia ambao wengi wao walikuwa Wakristo, watakaokuwa watiifu kwa Kanisa na serikali.

Ni katika mtandao huu ndiyo hii leo unaona Waislam wako nyuma na wamekuwa wakilalamika kuwa kuna hujma dhidi yao.

Bahati mbaya hili ni tatizo ambalo linatisha sana serikali na hivyo kuogopa kuliweka katika agenda ya matatizo ya jamii yetu.
 
Maustadhi mna vituko sana, fanyeni kazi, nendeni shuleni, madrasa siyo chuo.
Jeki,
Huwa naona tabu kutimia neno hili ''ujinga.''
Hofu yangu ni kuwa huenda kuna baadhi yetu wataona nimewatukana.

Lakini ukweli ni kuwa kuna watu wengi sana ni wajinga katika historia ya Tanganyika.
Hawajui mambo mengi sana.

Ndugu yangu jeki anawahimiza ''maustadhi,'' kujielimisha na anaandika kwa kejeli akidhani kuwa wajinga ni Waislam.

Waislam wengelikuwa wajinga wasingeweza kupambana na ukoloni kwa kiwango kile cha kuunda TANU na kuwaunganisha Watanganyika wote chini ya Mwalimu Nyerere kudai uhuru.

Soma historia ya Waislam wa Tanganyika uifahamu ndipo uzungumze na kuwa muungwana kwa kuonyesha adabu.

Katika mgogoro mkubwa uliokumba Waislam mara tu baada ya uhuru ni mgogoro wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) pale serkali ilipojitokeza kuivunja ili kuzuia Waislam wasijenge shule zao na Chuo Kikuu.

Sasa jitulize ondoa huko ''kujua'' ingia mitandaoni soma historia hii.

Ukioenda ingia hapa fanya search: mohamedsaidsalum.blogspot.com
 
Siongelei malaika. Naongelea jina Angel (given name) ambalo kwa hapo Tanzania ninawafahamu wanawake wengi tu wanaitwa hivyo, sijawahi muona mwanamme wa Kitanzania akiitwa Angel labda Angelo.
Pole sana.
kumbe hujawahi kuona,pole sana
 
Ukweli ni kuwa Wamisionari walifuata nyayo za madras na walimu wa kwanza katika shule za misheni walikuwa Waislam ambao hawakusoma katika shule za kanisa bali katika madras.

ilikuaje wakafundisha shule za kikristo na walikuwa wanajua kuandika kiarabu tu
 
Kama kuongea haya mambo sharti uwe

1. Mpigania uhuru ....TAA na TANU

2. Ulikuwepo kwenye harakati za uhuru

3. Kuwepo ndani ya TAA na TANU

4. Kufaham historia.....sijuwi ufaulu ni upi?

Basi wewe na Mzee Mohamed pia kaeni kimya.
Adolay,
Hapana haja ya hasira sote tujadiliane faida kubwa itapatikana.
Si lazima uwe ulishiriki katika harakati za kudai uhuru.

Mimi nimeijua historia hii zaidi ya watu wengine kwa kuwa ni historia ya maisha ya wazee wanga kwa hiyo nimeisikia na kidogo mengine kuona kwa macho yangu.

Nanyi katika mazungumzo mmesikia na kujifunza mengi kutoka kwangu.
Miaka yote nyie mkiamini kuwa TANU kajanayo Mwalimu Nyerere.

Mimi nkakurudisheni nyuma hadi 1924 kwa Kleist Sykes na Dr. Kwegyr Aggrey.
Sasa haya mngeyajuaje ikiwa tusingekuwa tunazungumza?
 
Tajiri,
Herufi za Kirumi zilikuja kutumika baada ya Wajerumani kuingia Tanganyika.

Kabla ya hapo watu wakiandika kwa herufi za Kiarabu na hizi zimetumika hadi
1950s mimi nimeshuhudia babu zetu wakiandikiana barua kwa herufi za Kiarabu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…