Eyce,Kama kawaida, rejea zinatumika pale unapoona zinaendana na nia zako ila pale unapoona zinakinzana au kukupa ushahidi usiokutosheleza bhasi inakuja simulizi ya yaliyofanyika au uliyopata kuyasikia ukiwa mtoto au kijana mdogo NYUMBANI, SEBULENI, KIBARAZANI au POPOTE PALE kwa wahusika. Hujawahi kwenda kinyume na hapo
Nyerere angekuwa muislamu na kwa hicho kichwa cha habari, bhasi ungeandika kurasa tatu bila kuchoka na kwa ushahidi ila kwa kuwa ni mkristo bhasi imekuja simulizi ambayo hatuna hata hakika nayo ikifuatiwa na malalamiko tupu.
Dr. Simba,Wazee wetu walikengeuka kumuamini kafiri.....nyerere aliwauza wazee wetu
Double R,Heko maalim.
Hiki nadhani ni kile waelezacho kuishi kwa sababu.(sina hakika kama ni maneno sahihi)
Waislam wa nchi hii na wazee wako umewasemea.
Mimi leo nimejifunza tu, persistence.
Sijui nini kati ya 'maumivu' au 'malengo' yanakusukuma kukomaa.
Najua dunia wakati mwingine hutupatia tusivyoviomba wala kuvitaka.
Kama ni maumivu mwenyezi Mungu akujalie faraja.
Kama ni malengo ikiwa ya heri ikawe hivyo uone majibu kabla ya kaburi.
Inshaallah