MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,011
- 2,185
Wote walioteuliwa wanafahamika kwa sura na kwa tabia. Sababu za kuteuliwa kwao ndo vigumu kuzitambua. Hapa nitajaribu kuzitaja kadri ninavyowafahamu.
Tuanze na Stergomena Tax
Huyu ni mtu mwenye elimu nzuri, mwanamke ambaye ktk wengi walioko baraza, hatuna wanawake wenye uwezo. Ana matatizo yake ya elimu ya u-daktari lakini haina shida. Tutegemee atumie Masters yake na siyo Ph.D uonayo kwenye jina. Kwa tamaa ya kuwa na akina mama, ameweza kuuzika kiurahisi kwa wizara ambayo kazi yake ni kusoma bajeti tu!
Ashantu Kijaji
Ni msomi, aliyeanzia kwenye akademia. Akiwa naibu waziri hakufanya vibaya na ana tabia ya kupenda maendeleo ktk jimbo lake sana, kwa kuwasikitikia viongozi wa serikali wasiojali maisha ya walio chini. Ni kiongozi mzuri ambaye haijulikani ni kwa nini hakupanda baada ya kuwa Naibu wa wizara ya fedha. Akiwa mwanamama, anastahili kujaribiwa.
Januari Makamba
Ana uwezo mdogo ambao hufichwa na ushujaa wake wa ku-pozi kama mwelevu. Hakustahili kuingia tena ktk baraza, lakini kuna nguvu kubwa ya urafiki. Ni misheni tauni sana na nasaha za internet kwa wingi ili aonekane ni msomi. wapo akina Rostam, wanufaika wa wizara yake na bado wanapenda kunufaika. Yupo na mstaafu JK anayemkumbuka kwa kuamini atapanda kulinda maslahi yake. Nishati ni wizara ambayo inawanufaisha watu kupitia umeme migodini, mafuta, na vituo vya hovyo hovyo na ukwepaji kodi ktk sekta hii. Ameingizwa ili kazi iendelee. Tutalizwa tu!
Makame Mbarawa
Ni waziri wa kuteuliwa miaka mingi, akitokea Pemba ambako CCM kwao ni ndoto kushinda kihalali. Amekuwa akiteuliwa ili kulinda nafasi ya Pemba. Alikuwa waziri mzuri kwa misingi yake ya kutokea akademia. Tatizo lake alijiingiza kwenye rushwa za wizara ya maji na akaanza kutafuta pesa alizoziita za uchaguzi, akifahamu Pemba hawezi pita. Naamini ameingizwa kwa msimamo wa rais kuinua kuonekana kwa Z’bar pamoja na kwamba uaminifu wake ulishaingia doa.
Eliezer Feleshi na Adelardus Kilangi
Hawa wamekuwa ktk mkanganyiko sana lakini Kilangi tangu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye ni kama alibebwa saana bila kujali uwezo wake. Badala yake tukaambiwa sijui anaaminika wapi na wapi lakini msingi wake ktk sheria na hata sifa ya profesa haina msingi wa kuaminika.
Feleshi simfahamu sana ktk mambo yake ya kiofisi. Je ni uzoefu wake wa kunyamazia maovu ktk awamu ya 4? Kama ni hivyo basi naye kaingizwa kwa mtindo wa kazi iendelee. Tutapigwa hadi nchi ichakae.