Ninavyowafahamu wateule wapya wa Rais Samia kwa historia yao ya nyuma na uhusiano wao na viongozi wa leo

Ninavyowafahamu wateule wapya wa Rais Samia kwa historia yao ya nyuma na uhusiano wao na viongozi wa leo

Wote walioteuliwa wanafahamika kwa sura na kwa tabia. Sababu za kuteuliwa kwao ndo vigumu kuzitambua. Hapa nitajaribu kuzitaja kadri ninavyowafahamu.

Tuanze na Stergomena Tax
Huyu ni mtu mwenye elimu nzuri, mwanamke ambaye ktk wengi walioko baraza, hatuna wanawake wenye uwezo. Ana matatizo yake ya elimu ya u-daktari lakini haina shida. Tutegemee atumie Masters yake na siyo Ph.D uonayo kwenye jina. Kwa tamaa ya kuwa na akina mama, ameweza kuuzika kiurahisi kwa wizara ambayo kazi yake ni kusoma bajeti tu!

Ashantu Kijaji
Ni msomi, aliyeanzia kwenye akademia. Akiwa naibu waziri hakufanya vibaya na ana tabia ya kupenda maendeleo ktk jimbo lake sana, kwa kuwasikitikia viongozi wa serikali wasiojali maisha ya walio chini. Ni kiongozi mzuri ambaye haijulikani ni kwa nini hakupanda baada ya kuwa Naibu wa wizara ya fedha. Akiwa mwanamama, anastahili kujaribiwa.

Januari Makamba
Ana uwezo mdogo ambao hufichwa na ushujaa wake wa ku-pozi kama mwerevu. Hakustahili kuingia tena ktk baraza, lakini kuna nguvu kubwa ya urafiki. Ni misheni tauni sana na nasaha za internet kwa wingi ili aonekane ni msomi. wapo akina Rostam, wanufaika wa wizara yake na bado wanapenda kunufaika. Yupo na mstaafu JK anayemkumbuka kwa kuamini atapanda kulinda maslahi yake. Nishati ni wizara ambayo inawanufaisha watu kupitia umeme migodini, mafuta, na vituo vya hovyo hovyo na ukwepaji kodi ktk sekta hii. Ameingizwa ili kazi iendelee. Tutalizwa tu!

Makame Mbarawa
Ni waziri wa kuteuliwa miaka mingi, akitokea Pemba ambako CCM kwao ni ndoto kushinda kihalali. Amekuwa akiteuliwa ili kulinda nafasi ya Pemba. Alikuwa waziri mzuri kwa misingi yake ya kutokea akademia. Tatizo lake alijiingiza kwenye rushwa za wizara ya maji na akaanza kutafuta pesa alizoziita za uchaguzi, akifahamu Pemba hawezi pita. Naamini ameingizwa kwa msimamo wa rais kuinua kuonekana kwa Z’bar pamoja na kwamba uaminifu wake ulishaingia doa.

Eliezer Feleshi na Adelardus Kilangi
Hawa wamekuwa ktk mkanganyiko sana lakini Kilangi tangu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye ni kama alibebwa saana bila kujali uwezo wake. Badala yake tukaambiwa sijui anaaminika wapi na wapi lakini msingi wake ktk sheria na hata sifa ya profesa haina msingi wa kuaminika.

Feleshi simfahamu sana ktk mambo yake ya kiofisi. Je ni uzoefu wake wa kunyamazia maovu ktk awamu ya 4? Kama ni hivyo basi naye kaingizwa kwa mtindo wa kazi iendelee. Tutapigwa hadi nchi ichakae.
Umeandika
 
January Makamba miongoni mwa wanasiasa wenye IQ kubwa ndo maana sikushangaa kuwa na urafiki mkubwa na Ruge RIP kwani ndege wafananao huruka pamoja sitoshangaa akija kuwa rais wetu hapo badae
Akili yako ya mwisho bure kama alivyo mtupu Makamba
 
Magufuli[emoji15]???hakukuwa na rais mule,ule ulikuwa mzigo ambao taifa hili lisingeuweza kuubeba,usiombe uwe na raisi fisadikteta utaimba haleluya.
Aidha unaumwa au ni hater tu
 
Watu mna chuki sana na January Makamba.

Hivi ndani ya CCM nani aliye msafi?
 
Sehemu kubwa na ufahamu wako ni sahihi, ila sijui kwa nini unasema Ph.D ya Stergomena ina matatizo. Niliwahi kumwona zamani sana akiwa mwanafunzi wa UDSM, na sababu kubwa ni kwa vile alikuwa anasemekena ni msukuma lakini alikuwa anaonekana tofauti na wasukuma, hivyo hiyo sifa ya kuwa msukuma asiyeonekana kama msukuma ikafanya awe anajulikana campus yote. Alipatia Ph.D yake Japan, je huko nako alinunua?

Makamba na Mbarawa wameingia pale nadhani zaidi ni kwa nguvu ya Kikwete tu, ni watu waliojaribiwa wakashindwa. Insurbodination aliyofanya makamba ni disqualification katika uongozi wowote wa kuteuliwa, na kwa failure ya Mbarawa kutimiza majukumu yake wizara ya ujenzi wakati huo, hakutakiwa kurudi pale tena.
Mimi nilikuwa najua hii PhD ni ya Bukoba
 
Uchambuzi wako

Uchambuzi wako hupo deep sana.Umenifanya nitoe machozi.Na nione kuwa ,Tanzania hatuwezi kusonga mbele.Mama ameishiwa tayari.Ambao walishawahi kuwa mawaziri na kufeli ,wanarudishwa.Je, nn kiliwaondoa na nn kimewarudisha?Je, katika watanzania million 60 hakuna wengine?Je,January Makamba ana kitu gani cha maana mpaka arudishwe kuwa waziri?Je,Prof Makame ana nn cha maana mpaka arudishwe kuwa waziri?Tanzania tupo kwenye break even point .CCM imechoka kabisa .Wapinzani pia wamechoka kabisa.Tutafute watu tofauti waunde vyama ili tuwaondoe CCM .Mama alitupa matumaini mwanzoni kuwa mtanzania yeyote anaweza kupata nafasi serikalini.Lakini naona ,mama amechoka.Hana jipya.
Nafikiri una ndoto za mchana aisee! Eti tutafute wapinzani wengine!! Wanasiasa wa kweli uzaliwa....! Wewe umeshindwa nini mpaka uwatafute wengine? Kuwa miongoni mwa waleta mabadiliko unayotaka yatokee!
 
Mimi nawaonea huruma wakina mabeyo wanawapigia saluti wakina mama tu!

Halafu karibu wizara zote muhimu zipo chini ya wakina mama!
Tatizo sio kuwapigia saluti akina Mama, bali ni mwanamke gani aliye ndani ya ile gauni/sketi/suruali/ n.k
Hayo ndio Maneno ya Robert Gabriel Mugabe kuhusu hiyo 50/50 au kwa kiswahili rahisi usawa wa kijinsia
 
JANUARY MAKAMBA alishaingizwa kwenye system na kuonekana ni Mpiga dili, bado anarudishwa tena.

Ataenda kuiba pesa nyingi ili aje kugombea Urais kama ilivyo ndoto yake
 
JPM alijaribu kuharibu hizi circle za madaraka kwa kuleta walau akili mpya lakini sasa tunarudishwa mule mule tena kwa lazima.

Ina maana hii nchi hakuna brain nyingine za kuongoza hadi turudie makosa haya haya kila mwaka?
Uongo mtupu
 
Uchambuzi wako kwa kiasi kikubwa nakubaliana nao. Tunarudi pale pale. Hata tubadilishe marais namna gani kila mmoja anayeingia akifanya uteuzi, ni lazima uegee kwenye mapenzi yake kwa wateuliwa zaidi kuliko uwezo wao. Tunarudi kule kule. Bila kufumua system na kuhakikisha rais hafanyi uteuzi kwa kutumia ''mahaba'' badala ya ''uwezo'' hakuna kipya.
Katiba mpya
 
Magufuli[emoji15]???hakukuwa na rais mule,ule ulikuwa mzigo ambao taifa hili lisingeuweza kuubeba,usiombe uwe na raisi fisadikteta utaimba haleluya.
Utakuwa ulitumbuliwa au ni fisadi mwizi mlarushwa ukakomeshwa. Magufuli ni kipenzi cha wanyonge majority na si ww. Historia itamkumbuka mwana mwema wa afrika. Watoto wako watamsoma hatua kwa hatua. Kipi alichofanya na si propaganda. Mwisho umati uliomzika na ideology iliyokaa ndani ya mioyo ya wengi
 
Back
Top Bottom