Labda Baba alikuwa kikazi tu huko . Hii Kichugu wanatakiwa atueleweshe.Kazaliwa mage eti
Naona Liberata naye ana influence haya mambo au Chalinze
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Labda Baba alikuwa kikazi tu huko . Hii Kichugu wanatakiwa atueleweshe.Kazaliwa mage eti
Naamini mama anaambiwa amchague nani na amtumbue yupi. Kwa ufupi kuna nguvu kubwa inayohakikisha mama anatimiza matakwa ya hiyo nguvu. Kumrudisha fisadi na msanii Makamba? Angalia mkuu wa mkoa Dar? Nani asiyejua ngivu hiyo? Tunasubiri naye Membe aletwe kundiniJPM alijaribu kuharibu hizi circle za madaraka kwa kuleta walau akili mpya lakini sasa tunarudishwa mule mule tena kwa lazima.
Ina maana hii nchi hakuna brain nyingine za kuongoza hadi turudie makosa haya haya kila mwaka?
Hivi ile route ya ndege kwenda chato bado ipo?
Naiona historia ya mobutu mpya wa Tanzania ikidhihiri Chato.
Dai katiba acha majungu, na mpgiwe mchakae tu . Tukiwamahasisha kudai katiba mnatuita magaidiWote walioteuliwa wanafahamika kwa sura na kwa tabia. Sababu za kuteuliwa kwao ndo vigumu kuzitambua. Hapa nitajaribu kuzitaja kadri ninavyowafahamu.
Tuanze na Stergomena Tax
Huyu ni mtu mwenye elimu nzuri, mwanamke ambaye ktk wengi walioko baraza, hatuna wanawake wenye uwezo. Ana matatizo yake ya elimu ya u-daktari lakini haina shida. Tutegemee atumie Masters yake na siyo Ph.D uonayo kwenye jina. Kwa tamaa ya kuwa na akina mama, ameweza kuuzika kiurahisi kwa wizara ambayo kazi yake ni kusoma bajeti tu!
Ashantu Kijaji
Ni msomi, aliyeanzia kwenye akademia. Akiwa naibu waziri hakufanya vibaya na ana tabia ya kupenda maendeleo ktk jimbo lake sana, kwa kuwasikitikia viongozi wa serikali wasiojali maisha ya walio chini. Ni kiongozi mzuri ambaye haijulikani ni kwa nini hakupanda baada ya kuwa Naibu wa wizara ya fedha. Akiwa mwanamama, anastahili kujaribiwa.
Januari Makamba
Ana uwezo mdogo ambao hufichwa na ushujaa wake wa ku-pozi kama mwerevu. Hakustahili kuingia tena ktk baraza, lakini kuna nguvu kubwa ya urafiki. Ni misheni tauni sana na nasaha za internet kwa wingi ili aonekane ni msomi. wapo akina Rostam, wanufaika wa wizara yake na bado wanapenda kunufaika. Yupo na mstaafu JK anayemkumbuka kwa kuamini atapanda kulinda maslahi yake. Nishati ni wizara ambayo inawanufaisha watu kupitia umeme migodini, mafuta, na vituo vya hovyo hovyo na ukwepaji kodi ktk sekta hii. Ameingizwa ili kazi iendelee. Tutalizwa tu!
Makame Mbarawa
Ni waziri wa kuteuliwa miaka mingi, akitokea Pemba ambako CCM kwao ni ndoto kushinda kihalali. Amekuwa akiteuliwa ili kulinda nafasi ya Pemba. Alikuwa waziri mzuri kwa misingi yake ya kutokea akademia. Tatizo lake alijiingiza kwenye rushwa za wizara ya maji na akaanza kutafuta pesa alizoziita za uchaguzi, akifahamu Pemba hawezi pita. Naamini ameingizwa kwa msimamo wa rais kuinua kuonekana kwa Z’bar pamoja na kwamba uaminifu wake ulishaingia doa.
Eliezer Feleshi na Adelardus Kilangi
Hawa wamekuwa ktk mkanganyiko sana lakini Kilangi tangu alipoingia alikuwa ni mtu ambaye ni kama alibebwa saana bila kujali uwezo wake. Badala yake tukaambiwa sijui anaaminika wapi na wapi lakini msingi wake ktk sheria na hata sifa ya profesa haina msingi wa kuaminika.
Feleshi simfahamu sana ktk mambo yake ya kiofisi. Je ni uzoefu wake wa kunyamazia maovu ktk awamu ya 4? Kama ni hivyo basi naye kaingizwa kwa mtindo wa kazi iendelee. Tutapigwa hadi nchi ichakae.
Nchi ina mtindio wa ubongoKwa makamba nchi inarudi kwenye dili.
Hiyo inaonakana ndo kawaida ya viongozi wetu. Maana hata JPM alikuwa anaweza mtumbua mtu na baadae akamrudisha tena. Ona kwa Simbachawene, Nchemba n.k.Hivi ni sharti kila rais akiingia madarakani Mawaziri, RCs na DCs lazima wawe ni watu wale wale wa miaka yote? Kwamba uteuzi lazima uteue watu waliowahi kuwa mawaziri hata kama walitoka baadae kwa ufisadi, ni sharti uchague kutoa hao ama kuwa badirisha tu hao hao. Maana miaka yote majina ni yale yale tu
Mkuu ni lipi baya la Makamba linalomfanya awe hafai kurudi katika nafasi ya uwaziri ?System imeshakufa mtu anampangia njama Rais kipindi u makamu leo unamrudisha unataka tuseme ulikua kwenye NJAMA ... vetting gani mtu kama MAKAMBA ANAWEZA PITA KAMA sio Tz na UGANDA tu dunia nzima.
Kutaka kugombea urais hapo baadae (kwa mwanasiasa) haliwezi kuwa ni kosa.JANUARY MAKAMBA alishaingizwa kwenye system na kuonekana ni Mpiga dili, bado anarudishwa tena.
Ataenda kuiba pesa nyingi ili aje kugombea Urais kama ilivyo ndoto yake
Kuna mambo mawili,Kukopa 1b ktk mifuko ya jamii
Kwani wewe unaweza kukopeshwa na mifuko ya jamii pamoja na kuwa unaweza kuwa mwanachamaKuna mambo mawili,
1. Ni lazima iwe ni kosa kukopa kwenye mifuko ya jamii.
2. Ni lazima iwe ni kweli unayemtaja alifanya hicho ulichokisema kafanya.
Je, una hakika hayo mawili hapo juu ni kweli kwa Mh. Makamba au ni tuhuma za jumla zisizo na uthibitisho ?
Unaposema WIZARA ISIYO YA MUUNGANO unamaanisha nini ?Japokuwa Rais hapangiwi nani wa kuwateua katika nafasi mbalimbali, lakini ni sahihi wizara isiyo ya Muungano kupangiwa watu kutoka upande wa pili wa Muungano.Pili ni sahihi mkoa mmoja kuwa na mawaziri watatu, kutoka kwenye majimbo, wakati mikoa mingine haijatoa mawaziri kabisa.
Ningependa sana unijibu mkuu. Ila kama umeamua mjadala uwe ni "swali kwa swali" basi sawa. Naishia hapo.Kwani wewe unaweza kukopeshwa na mifuko ya jamii pamoja na kuwa unaweza kuwa mwanachama
Na wengine wanatuhumiana tuWatu wanateteana tu...
Kuhusu January umesema kweli kweliiii kweliiiii 1000%.
Uwezo wa January ni mdogo mdogo sanaaa, he has no potential kabisa, as you said, nguvu kubwa imetumika kumweka January katika baraza la Mawaziri, ili alinde maslahi ya akina JK ya mafuta, Lake Oil and Lake Gas, pia Maslahi ya Rostam katika Gas, Taifa Gas and Mihan.
Sitegemei kama atadumu muda mrefu katika hii wizara ya Nishati, sbb kashfa ya rushwa au mikataba mibovu atakayoingia baadae au sera mbovu atakazopendekeza baadae kwa kulazimisha au upendeleo wa walimweka utadhihirika mapema na itamuondoa haraka, huwa sikoseagi kubashiri, hasa pia kikubwa kitakacho muondoa ni kutaka kugombea nafasi ya Urais hapo mbeleni, sbb ataanza makundi na mikakati mapema ili agombee, hapo CCM itamkata haraka.