Ninawaogopa sana viumbe wa kuitwa binadamu

Una uwezo wa kuishi na kila binadamu, ila uwe makini na yule unayemsogeza kwenye maisha yako.

Wengine wanastaili uishi nao kwa mbali na wachache sana wanapaswa uwe nao karibu.
Kosa ni kufanya vise versa ama kuwakataa watu.

Kumbuka hata huyo unayemuona mbaya kuna namna moja ama nyingine anamsaada na wewe.

Kumkataa mtu ni sawa na kujikataa mwenyewe, cha msingi tumia akili kuishi na watu.
 
Ni kweli lakini ikifikia hatua ya kuwaogopa watu hadi utamani kuishi kipweke ni hatari kwako.
Jichanganye nao hivyohivyo sababu ukishindwa utaishia kuyachukia maisha yako pia... Wao ni watu, na wewe ni mtu.
Ukituona sisi sote ni wabaya lazima ufikie kujiua sababu wewe na mimi tunafanana. Ukiona watu wote hawafai hata wewe utajiona hufai na utaanza kutafuta maisha ya kipekeepekee ambayo hawezi kuyapata ukiwa hai.

Kwa kifupi wewe unahitaji daktari wa akili au unaweza kupona mwenyewe kwa kuanza kuyatazama maisha tofauti kadogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ