Watu ndiyo maisha.
Ukikata uepukane na watu, basi unahitaji pumziko la milele. Kufa.
Na huko huna hakika kama hawapo. Unaweza kuwakimbia huku, alafu unaelekezwa Jehanamu.
Huko ni vilio, vijambo, machozi, ukunga, harufu ya kuungua, aaagh kubabake.
Au ukimbilie Paradiso huko ni kelele za kusifu, shangwe, kuabudu, kugigida mito ya pombe, kufanyana, eee bhanah weee.
Bakia tu humu ulipotuzoea Mkuu.
Wakikuumiza wapo watakaokufariji. Wakikuzomea wapo watakushangilia. Wakikuchukia wapo watakaokupenda.
Hakunaga upande mmoja tu.