Kadhi Mkuu 1
JF-Expert Member
- Feb 4, 2015
- 19,687
- 23,689
Hata mimi nakuogopa sana wewe binadamu ungejua hata usinge karibia watu.Nimejikuta ninawaogopa sana binadamu kutokana na visa mbalimbali nilivyowahi kupitia kwenye maisha yangu.
Asili yangu ni ukimya na utaratibu lakini kuna wakati maisha yanahitaji ujichanganye na watu mbalimbali kutokana na mifumo yetu.
Na ndicho kipindi nilichojifunza kuwa binadamu ni kiumbe hatari mno.
Ninaogopa watu, ninaogopa miunganisho mipya, hata katika mahusiano ya kimapenzi inachukua muda mno kujiunganisha na mtu kihisia.
Sina imani na kiumbe binadamu kwenye nyanja zote za kimaisha! Japokuwa haiwezekani, lakini ninatamani niishi mahali nisiyoweza kukutana na binadamu.😔😔😔