Ninawaogopa sana viumbe wa kuitwa binadamu

Asante sana. Nimezingatia maneno haya🙏🏾
 
Watu ndiyo maisha.

Ukikata uepukane na watu, basi unahitaji pumziko la milele. Kufa.

Na huko huna hakika kama hawapo. Unaweza kuwakimbia huku, alafu unaelekezwa Jehanamu.
Huko ni vilio, vijambo, machozi, ukunga, harufu ya kuungua, aaagh kubabake.

Au ukimbilie Paradiso huko ni kelele za kusifu, shangwe, kuabudu, kugigida mito ya pombe, kufanyana, eee bhanah weee.

Bakia tu humu ulipotuzoea Mkuu.
Wakikuumiza wapo watakaokufariji. Wakikuzomea wapo watakushangilia. Wakikuchukia wapo watakaokupenda.

Hakunaga upande mmoja tu.
 
Wakati nasoma heading, nikadhani aliyeandika post hii labda ni mamba au kiboko au mbwa..!! Kumbe naye ni binadamu lakini hajiogopi yeye..!!

Embu mamdogo Amehlo njoo nisaidie kuelewa hii makitu. Dada To yeye na wewe unajiogopa? Shemela Evelyn Salt kwani huyu kapigapigaje hapo?
 
Asante, sijawahi kufikiria kujitoa uhai.
Nipo sawa kwa sasa.
 
Upo sahihi.
 
Binadamu katika level tofauti tofauti za wanyama😂
 
Mimi nadhani wewe tutaendana. Mimi pia nipo hivo hivo..natamani ningeenda kuishi kwenye kisiwa changu peke yangu.Binadamu ni hatari sana sio wa kuwachukulia poa kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…