Ninawezaje kuifungulia mashtaka Benki ya NMB kwa dhuluma hii ya fedha zangu?

Kuna watu wakiona mtu anafanya kazi bank basi wanamuona wa maana na kumuogopa
Kuna majizi humu ukijichanganya lazima uumie
Haki yako unashindwa kuipigania
Anawezaje kukuambia eti ntakushtaki kwa mkurugenzi ufukuzwe kazi na wewe unaogopa badala ya kwenda kwa mkurugenzi
Nyie ndio mnazabwa kofi mnaondoka
Pigania haki yako na uhame bank hiyo
 
Mabenki yanaiba sana kwenye Topup
 
Sikuogopa Ila nilimheshimu tu.

Na tena nilimjibu kuwa sidhani Kama lengo la majadiliano Yale Ni kutishana.
 
Au ulifoji nyaraka za kuombea huo mkopo kwa mwajiri wako na huyo meneja na loan officer wake wanajua kuwa ulifoji hizo nyaraka hadi kufanikisha huo mkopo ndiyo maana kakutishia kukushitaki kwa mwajiri wako?
 
...Ni Vizuri ukatuleza Wazi kilichopo ili tuweze kusaidia.
Wamuambia Kwa Nini hasa Account imefingwa ? Bila shaka watakuwa na Sababu. Tuanzie Hapo...
 
Kwanza naomba kuuliza wakati unapewa mkopo wa top up, ulipewa hela yote uliyoomba au ulipewa balance baada ya kufuta mkopo wa awali.
(i) Kama ulipewa hela zote ulizoomba kwenye mkopo wa pili maana yake mkopo wa kwanza haukufutwa hivyo benki wako sahihi kukukata mikopo yote 2 unless urudishe hela zilizotakiwa kufuta mkopo wa kwanza

(ii) Kama ulipewa balance baada ya kukata hela za kufuta mkopo wa kwanza then benki wamekosea kuendelea kukukata mkopo wa kwanza ambao ulishakatwa hela kuulipa na hivyo wewe una haki
 
Sikuogopa Ila nilimheshimu tu.

Na tena nilimjibu kuwa sidhani Kama lengo la majadiliano Yale Ni kutishana.
Pambania haki yako, asikutishe au yeye ndio anaiba
Hawa jamaa wananiudhi sana
Nilishatukana benk kwa wizi wao wa kutupa elfu 10 chini halafu wanasema zimepungua
Usiwape heshima kama wao wameshindwa kujiheshimu
Kwani sio halali hizo pesa?
 
Ilikuwaje kwanza hadi unafungiwa akaunti?
Hayo mambo hayo wanafanyiwa wafanyabiashara wenye mzozo na Tra
 
Ndugu yangu mkopo wa bank una walakini, hakuna aliyekopa akabaki salama
Jirani zangu hapa wengi na Watanzania wengi wameuzishwa nyumba zao kila mtu mtaani analaani
 
Unamkumbuka kuna mfanyabiashara fulani pale kariakoo alikuwa na kesi na TRA? Alitumia media mwisho wa siku hamna alichokipata.
Hoja sio kutumia Media tu, lazima mengine yazingatiwe tu. Ni lazima ukae na wanasheria wabobevu ili kuona kama madai yako yana mashiko na kuna mianya ya kupita, kisha uelekee kwenye media ili kuondoa uwezekano wa kesi yako kuishia gizani.

Kwenye kesi za madai dhidi ya makampuni makubwa, ukiwa na hoja zenye mashiko na ushahidi wa kutosha then ukatembea na media, hiyo unashinda mchana kweupe.

Huyo wa TRA alianzisha kesi bila kuwa na msingi, media haikufanyi ushinde kesi zaidi ya kuileta kwenye mwanga.
 
Kwani huyo wa TRA aliwahi kwenda mahakamani kufungua kesi kweli? Nakumbuka huyu bwana viongozi wa serikali na TRA waliishia tu kumpiga dana dana hadi alipoamua kujiua kwa kujipiga risasi.
 
...Ni Vizuri ukatuleza Wazi kilichopo ili tuweze kusaidia.
Wamuambia Kwa Nini hasa Account imefingwa ? Bila shaka watakuwa na Sababu. Tuanzie Hapo...
Mwanzoni waliniambia mfumo wa ESS una matatizo ukitulia watafuta Deni langu la awali (maana nimeisha lilipa) Ila kadri muda unavyosogea sababu zinakua nyingi Hadi hivi Sasa nikiwapigia simu wanasema niendelee kukaa hivyo hivyo Hadi Mambo yatakavyo kuwa sawa.

Na Mimi kwa vile nimepewa vitisho na Branch manager siwezi kumfuatilia kwa karibu na bakia ku-deal na loan officer tu, nayeye haelewi awhile wapi aache wapi.

Nitaweka picha ya majibu kutoka NMB
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…