Ninawezaje kuifungulia mashtaka Benki ya NMB kwa dhuluma hii ya fedha zangu?

Ndugu yangu mkopo wa bank una walakini, hakuna aliyekopa akabaki salama
Jirani zangu hapa wengi na Watanzania wengi wameuzishwa nyumba zao kila mtu mtaani analaani
Nashukuru Mimi dhamana yangu kuwa ajira yangu la sivyo sijui tungefikishana wapi.
 
Pambania haki yako, asikutishe au yeye ndio anaiba
Hawa jamaa wananiudhi sana
Nilishatukana benk kwa wizi wao wa kutupa elfu 10 chini halafu wanasema zimepungua
Usiwape heshima kama wao wameshindwa kujiheshimu
Kwani sio halali hizo pesa?
Huwezi Amin kwa muda uliobakia nawaza kuchukua maamuzi magumu itakapofika January
 
Kuna bank za kiswahili kuweni nazo makini,bank za maana si zipo,kila siku tu bank inapewa lawama bado mnaing'angnia tu,aisee poleni
 
Fata huu ushauri mkuu,washtaki hao !
 
Ipo hivyi

Walikuwa wananidai Milioni mbili na nikaongeza Deni la Milioni Saba jumla Milioni Tisa.

Hivyo Basi kwenye Deni jipya nikaandikiwa Milioni 9 na nikapewa Milioni 7 cash Ila wakati pesa zinaingia akaunti ikafungiwa na pesa sikuzipokea mkononi na salio lilokuwepo kwenye akaunti pia likajumlishwa na mkopo huo kufungiwa.

2:- Mkopo wa awali kwenye ESS haujatolewa na huku kwenye makato mapya ya mkopo wa Milioni Tisa wanakata pia......Aiseeeeh
 
Wakati wa top up ilitakiwa deni liwekwe pamoja.

Kufikia kufungiwa account ni kuwa hakuna kitu unachoweka kwenye account yako, hivyo wanai hold kiknachoingia kinamezwa.

NMB walitakiwa wakuite kupitia mwajiri wako ili mrekebishe hilo.

Sasa hilo la kumfungulia mke wangu biashara ujiweke sawa, hakuna mia atakayolipia deni.
 
Yaan pesa zako wao wanajichukulia tu, alafu ukienda kuomba waache kuzichukua wanakutishia kukufukuza kazi, na wewe hujui ufanye nini?
Umeona jinsi nchi hii ilipotufikisha?, Na huyu Ni mtumishi wa umma, vipi kwa mwananchi wa kawaida?

Hebu unaweza amini ata Mimi ninazo hasira?
 
Afisa utumishi aliishasema wamuone awasaidie Nini Cha kufanya Ila wao wakajifanya Ukuaji, maana Hadi alirejea Benki ya CRDB napo walikutana na changamoto Kama yangu ikatatuliwa Ila wao wakajifanya wajuaji.

Tena ulitaka Benki nyingine wanakua wakali mno, kwamba nawafundisha kazi.
 
NMB wengi hawana customer care language.
 
Yani wewe hueleweki,hata kusiidiwa ni ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ