Ninayoyaona KKKT nimegundua Kanisa Katoliki ndilo kanisa la Kweli

Kwani malasusa na tuhuma zake? Wachungaji wangapi wanalawiti na kugonga wake za watu? Mti mwema ndio unaopigwa mawe. Ni binadamu na wana mapungufu ila sio mapungufu ya kanisa
 
Ngoja nichukue popcorn kuangalia vita vya Wagalatia .Sijui kwa nini hawakumpa usukani Maghayo amalize utata wote.
 
Uislam pekee.

Hakuna mfumo kama wa kanisa kwenye Uislam. Uislam ndiyo dini pekee kwa Mwenyezi Mungu. Kila kitu ni wewe na Muumba wako tu.

Naheshimu Mtazamo wako Dada yangu, hapo ume address akili yangu, na mambo ya Imani inabidi uje ushawishi wa moyoni baada ya kupitia aya za imani na kupata badiliko la ndani (Biblia pekee ndo ime cover hii topic vizuri), vipi napataje maelezo yatakayobadilisha moyo wangu kuamini unachokisema?
 
Nimesikitika sana kwa Wewe Kuchelewa kujua kuwa Kanisa Katoliki ukiahilia mbali kuwa ndilo Kongwe duniani na limezaa hayo Madhehebu mengine pia ndiyo Kanisa linaoongoza kwa kuwa na Watu ( Waumini ) wenye Akili Kubwa, Wasioogopa, Wasomi wa Kweli na hawatishwi na ama Mpumbavu yoyote au Mamlaka yoyote ile ya Kikatiba katika nchi waliyoko.

Halafu Wakatoliki na TEC yao ( yetu GENTAMYCINE nikiwemo ) huwa Wakitoa Tamko au Msimamo wao mara nyingi hawathubutu kupoteza muda wa Majibizano na Wapumbavu bali hukaa Kimya ( Hunyamaza ) ili Akili na Ujinga vipambane / viumane.

Ninajivunia kuwa Mromani Katoliki!!!
 
Kwani malasusa na tuhuma zake? Wachungaji wangapi wanalawiti na kugonga wake za watu? Mti mwema ndio unaopigwa mawe. Ni binadamu na wana mapungufu ila sio mapungufu ya kanisa
Sasa kijana Kanisa makasii, na mapadri wawe zaidi ya 90% mashoga halafu useme siyo tatizo la kanisa?

Tuwe wa kweli kwenye nafsi zetu, tusidanganyane kutetea maovu, kwa kuwa tumeaminishwa ujinga tu.

Wazungu wameshastuka huko, wanayafunga makanisa na kuyafanya misikiti:

 
Nilisoma andiko moja la Ellen G white alisema kanisa katoliki limejengwa katika misingi imara halitakaa litetereke mpaka mwisho wa dunia.kuna muda itafika utatokea mpasuko ndani ya sabato na wengi watajitenga halafu haya madhehebu mengine yatasambaratika kabla ya mwisho wa dunia!!!
Ukiangalia kwa jicho la tatu andiko lake kama lina ka ukweli hivi,kanisa katoliki linapingwa vikali na madhehebu kibao lakini halijawahi kutetereka miaka na miaka!!
 
Mashekhe wanavyowala watoto? Huko madrasa? Mfano juzi shekhe zuberi kapigwa miaka 30 jumlisha kifungo cha maisha....halafu michezo ya kulawiti ipo kwenu sana waislamu na watu wa pwani sio siri..
....
 
Kwanza nakushauri isome Qur'an, majibu yote ambayo huyapati kwneye biblia au kanisanai yanajibiwa na Qur'an: Qur'ani Tukufu

Cha pili, ingia msikiti wowote utaposikia aadhana ufate Waislam wanavyosali, utaiona tofauti na raha yake. Wewe mfate imam, hata kama hujuwi kwa mwanzo mwanzo, inama na inuka nao tu. Ustaiona raha yake na utajiuliza niloikuwa wapi siku zote.

Uislam ni mwema sana. Hakuna longolongo. Fata Uislam usifate Waislam, wapo wengine ni Waislam jina tu.
 
Mleta mada hujui historia, na umechanganya mambo.
Ngoja upate elimu kidogo.

1. Petro hakuanzisha Kanisa Katoliki. Petro alizaliwa Israeli, akaishi Israeli, akahubiri Israel na mwisho akauwawa Israel, tena akiuwawa na utawala wa kikoloni wa kirumi (Roma). Kanisa Katoliki (Roma) lilianzishwa karne kadhaa baada ya Petro kufa, na lilianzishwa huko Roma. Yote kwa yote, Biblia inasema Petro alikuwa na mke na familia!

2. Yesu aliposema atalijenga kanisa lake juu ya mwamba huu, hakumaanisha atajenga jengo la kanisa juu ya Kabuli la Petro, bali atajenga imani ya ufuasi juu ya kile ambacho Petro alikisema saa ile (Petro alisema, wewe Yesu ndio kristo (akimaanisha Yesu ndio alipakwa mafuta (aliyeandaliwa rasmi kutoka mbinguni) kuja kuwaokoa watu na dhambi zao)

3. Kanisa Katoliki la sasa kimuundo, kimwenendo na kimsimamo sio sawa na katoliki lililokuwepo zama zingine zote za nyuma. (Kuna vitu vingi vipya (vizuri au vibaya) vipo sasa tofauti na hapo kale.)

4. Kanisa Katoliki halifanani kila kitu dunia nzima. Ndio maana usishangae kuna mapadri huko Brazil wanaruhusiwa kuoa, huko Marekani kuna majimbo ya kanisa Katoliki yanatambua ushoga na kubariki ndoa za jinsia moja nk). Hivyo usikariri sana.

5. Mifumo mingine ya ndani ya siri ya kanisa katoliki sio safi au kuishabikia kidini, ni mifumo ya kisiasa na umafia ndani yake. Hivyo utazame ukatoliki kiimani na kisiasa pia.
 
Lingekuwa halitetereki makanisa yasingegeuzwa misikiti.
 
Mashekhe wanavyowala watoto? Huko madrasa? Mfano juzi shekhe zuberi kapigwa miaka 30 jumlisha kifungo cha maisha....halafu michezo ya kulawiti ipo kwenu sana waislamu na watu wa pwani sio siri..
....
Huo ni ubishani wa kijinga tu. Shekhe siyo Uislam, kama unamfata Shekhe unaufananisha Uislam na Ukristo. Hilo ni kosa.

Uislam ni dini ya kila mtu siyo ya "Shekhe". Shekhe unaesema kalawiti watoto huyo ndiyo ukisikia "kafiri" katika Uislam.
 
Haya yapo hata Kwa Maustadh na Mashehe ni tabia ya mtu.Kuna mtu ana wanawake wanne lakini Bado ana michepuko hapo utasema Waislamu Malaya?Bali ni tabia ya mtu.Nyakati zitakuja ambalo Waafrika tutarudi kwenye Dini zetu tukiachana na hizi futuhi za Waarabu na Wazungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…