Ningekuwa Mkuu wa Wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu

Ningekuwa Mkuu wa Wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Ningekuwa ndio mkuu wa wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu.

Hizi ni hatua ambazo ningechukua.

Kwanza ningetambua idadi ya wahitimu wote wanaotokea wilayani kwangu.

Ningehakikisha kama hawana kazi za kufanya nawatafutia kampuni, taasisi na viwanda vya kufanyia mazoezi ya vitendo (internship) kipindi wanasubiria ajira zao.

Nisingekubali wahitimu wanaotokea wilayani kwangu kukaa bila kitu cha kufanya huku wakipoteza maarifa yao waliojifunza vyuoni bila kuyafanyia chochote.

Pili ningehakikisha natambua idadi ya wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuoni. Hawa wangekuwa wanajiunga kufanya field moja kwa moja kwenye kampuni, taasisi na viwanda vilivyopo wilani kwangu.

Ningeanzisha wakala wa kuajiri kwa kazi zote zinazotangazwa na kampuni za binafsi katika wilaya yangu. Hivyo ningetambua nafasi zote zilizowazi katika kampuni, taasisi na viwanda binafsi kisha zingetangazwa kupitia wakala hiyo wilayani kwangu.

Tatu ningeanzisha vikundi mbalimbali kwaajili ya ujasiriamali ambavyo ningevidhamini mikopo ya riba nafuu. Vikundi hivi vingefanya ujasiriamali mbalimbali mfano ufugaji, kilimo, biashara za bidhaa, usafirishaji n.k. Haya yote yangekua chini ya uangalizi wa wilaya yangu.

Kwakweli mambo yangekua ni moto kwenye wilaya yangu.

Kwenye wilaya kuna matatizo mengi lakini nadhani tatizo la ajira ndio kubwa kuliko matatizo yote Tanzania. Ni tatizo gumu linalohitaji ushirikiano na akili ya ziada ili kuweza kulitatua.

Wewe kama mkuu wa wilaya unatumia mbinu zipi kutakua tatizo hilo.

Karibuni kwa maoni.
 
Kwa muundo wa Utawala wa nchi hii hilo haliwezekani milele na ndo Maana tunataka Katiba ibadilishwe.

Mambo yako centralized na maamuzi yote na sera zote zinatungwa juu huko.

Kwa Mfumo wa Utawala wa Majimbo hilo linawezekana, Mfano Kenya hawana Mikoa kwa sasa wana County zinaitwa na kila County ina Gavana wake na Yule Gavana anapigiwa kura na wananchi na kila county ina Bajeti yake ina jenga Barabara yenyewe, Inalipa mishahara watumishi wa afya na kada zingine yenyewe, inaajiri yenyewe. Haiingiliwi na Serikali kuu.

Sasa Mkuu wa wilaya hana Bajeti anaajiri vipi? Sana sana labda kwenda kuitwa kufungua.
 
Kwa muundo wa Utawala wa nchi hii si Mkuu wa wilaya wala Mbunge wala Mkuu wa Mkoa anaye weza tatua changamoto za ajira wailayani kwakwe au mkoani kwake.
 
Suppose wewe ni mkuu wa wilaya ya Liwale au Namtumbo ambapo hakuna kiwanda wala kampuni yoyote ile ungefanyaje?
 
Ningekuwa ndio mkuu wa wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu.

Hizi ni hatua ambazo ningechukua...
Kuwa na mawazo kama hayo ni vyema na siyo dhambi mkuu, lakini umejaribu kujiuliza kwanza Tanzania yako unayoishi mawazo haya yanawezekana? Siyo rahisi kwa mfumo wetu na katiba yetu iliyopo. Fight for your own kwanza, achana na ndoto za ukuu wa Wilaya.
 
Safi sana, ni muhimu kuwa na watu wenye uthubutu.

Je, Mkuu utayakumbuka haya ukishaanza kukaa kwenye VIETEEE 🤣
 
Mkuu sio rahisi hivyo. Ukichukua tu wilaya moja wasio na kazi wanaweza kujaza viwanda vyote Bongo 😀😀
 
Back
Top Bottom