Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 7,899
- 10,415
Ningekuwa ndio mkuu wa wilaya ningetatua tatizo la ajira kwa watu wote wanaoishi wilayani kwangu.
Hizi ni hatua ambazo ningechukua.
Kwanza ningetambua idadi ya wahitimu wote wanaotokea wilayani kwangu.
Ningehakikisha kama hawana kazi za kufanya nawatafutia kampuni, taasisi na viwanda vya kufanyia mazoezi ya vitendo (internship) kipindi wanasubiria ajira zao.
Nisingekubali wahitimu wanaotokea wilayani kwangu kukaa bila kitu cha kufanya huku wakipoteza maarifa yao waliojifunza vyuoni bila kuyafanyia chochote.
Pili ningehakikisha natambua idadi ya wanafunzi wanaoendelea na masomo vyuoni. Hawa wangekuwa wanajiunga kufanya field moja kwa moja kwenye kampuni, taasisi na viwanda vilivyopo wilani kwangu.
Ningeanzisha wakala wa kuajiri kwa kazi zote zinazotangazwa na kampuni za binafsi katika wilaya yangu. Hivyo ningetambua nafasi zote zilizowazi katika kampuni, taasisi na viwanda binafsi kisha zingetangazwa kupitia wakala hiyo wilayani kwangu.
Tatu ningeanzisha vikundi mbalimbali kwaajili ya ujasiriamali ambavyo ningevidhamini mikopo ya riba nafuu. Vikundi hivi vingefanya ujasiriamali mbalimbali mfano ufugaji, kilimo, biashara za bidhaa, usafirishaji n.k. Haya yote yangekua chini ya uangalizi wa wilaya yangu.
Kwakweli mambo yangekua ni moto kwenye wilaya yangu.
Kwenye wilaya kuna matatizo mengi lakini nadhani tatizo la ajira ndio kubwa kuliko matatizo yote Tanzania. Ni tatizo gumu linalohitaji ushirikiano na akili ya ziada ili kuweza kulitatua.
Wewe kama mkuu wa wilaya unatumia mbinu zipi kutakua tatizo hilo.
Karibuni kwa maoni.