Nini dhumuni la Serikali kuanzisha tahasusi hii ya biashara ikiwa na somo la 'Islamic Knowledge'?

Comb zote za biashara hujaziona ? Ikiwemo EGM?


Mbona hapa hamuongei?
 

Attachments

  • Screenshot_20240321-200843.png
    131.6 KB · Views: 2
Comment na hapo kwenye divinity
 

Attachments

  • Screenshot_20240321-200843.png
    131.6 KB · Views: 1
Sawa tu, hata waweke na Budhisim knowledge kwangu poa tu, zote ni elimu.
 
Wanataka wapate wachumi wa kiislamu waende kufundisha uchumi uarabuni
 
Ficha ujinga wako, yaani watu mna chuki na uislamu kupitiliza


Mbona divinity ipo? Yaani Mtu anaangalia mwisho 26 anakuja kuanzisha uzi na kuleta lawama
 

Attachments

  • Screenshot_20240321-200843.png
    131.6 KB · Views: 3
Comb zote za biashara hujaziona ? Ikiwemo EGM?


Mbona hapa hamuongei?
Hizo zimewekwa Chambo. Zilipaswa ziwekwe Kwenye Shule za Kidini na Mitaala Ya Kidini.

Serikali yetu isiyo na Dini haikupaswa kuingiza mambo ya Dini Kwenye Shule za Serikali.

Nakumbuka huko Nyuma Shule za Seminari za Kikristo zilikuwa na Mitaala yake binafsi ikijumuisha na ya serikali

Haikutakiwa Mitaala ya Shule za Serikali Ijumuishe Mitaala ya Kidini.

Tena Nadhani Divinity lingekuwa somo Jumuishi Kwa Dini Zote. Yani Mtu ukiamua kusoma Divinity uweze kuwasoma Miungu Yote ya Dini Zote na maarifa yake bila kujali Imani Yako.

Lete Mtaala Wenye "Christianity Religion" ndani yake.
 
Hili lisheitwan linaloitwa TAMISEMI,limepoka madaraka ya Wizara nyingi kama afya&elimu.
Na kuwatupilia mbali wanataaluma wa Wizara husika.
Hivi kazi ya Wizara ya Elimu ni nini vile kwa sasa?
 
Mbona kama anataka kuvurugs East Africa.waarabu watu wenye roho mbaya.
 
Tumesema mambo ya dini ziachiwe dini zenyewe. Sasa combination yenye islamic knowledge ni ya kazi gani. Halafu binafsi nimestaajabu kuona wameongeza utitiri wa combinations. Nilitarajia wapunguze au kuboresha zilizopo.
 
1.Msmbo ya tahasusi si uchaguzi wa lazima ni hiari. Hivyo hiyo tahasusi ambayo inaleta mtafaruku hakuna kijana ataelazimishwa kuisioma
Kuendelea kuipigia kelele ni dalili ya uoga ambao ni zao la ubaguzi

2.Tahasusi imelenga kuanda vijana ambao watakidhi matakwa ya kisoko ktk Islamic finance/banking/insurance
Wenzetu ktk 1st World wame recognise matakwa hayo muda mrefu na wame advance sana bila kujali mfumo huo unatolewa na imani gani
Wakati wa Kenya wanapigana kuwa champions kwenye Islamic Finance in East Africa bado sisi tunanyoosheana vidole

Wakati ule wa World Economic Crisis/Credit Crunch Pope wa wakati ule aliwahi kushauri nchi za Ulaya ziangalie Islamic Finance kama alternative solution
Kanisa Katoliki South Africa zaidi ya 1/3 ya deposit zao Wana deposit kwa Islamic Bank of South Africa

3. Kabla hata ya haya mabadiliko Divinity Ina tofauti sana na Islamic Knowledge
Divinity Iko ktk masuala ya mahusiano ya Moja kwa Moja kati ya binaadam na Muumba
Wakati Islamic Knowledge ukiacha masuala ya mahusiano ya binaadam na Muumba inazungumzia masuala yenye vionjo vya Kisheria, Kiuchumi na Kibiashara kama Zaka, Mirathi na Miamala ya Kibiashara. Hivyo basi kuoanisha masomo ya biashara/uchumi na Islamic Knowledge si kitu kibaya au kigumu

Islamic Knowledge kama lilivyo ukiacha mabadiliko ambayo yanatarajiwa kufanywa na Bakwata limekuwa somo ambalo lina mawanda mapana kiasi kwamba kijana ambaye anaweza kupata C ya Islamic anaweza akasoma somo lolote la social science akafaulu vzuri sana

Watu wanaosomea Sheria watakuwa mashahidi. Kuna Sheria 3 ==>
1 Canon Law ambazo tumerithi toka kwa Muingereza
2. Custom Law ambazo ni Sheria za Kimila
3. Islamic Law ambazo ni Sheria za Kiislam

Kwanini waweke Islamic Law tu, wasiweke na Christian Law. ??

Asilimia 90 ya Ma Sheikh tulionao ukiwapa.Mtihani wa Islamic Knowledge hata wa 0 level wanapata F. Ni somo linalohitaji arguements na logic


4. Bado wa Tanzania wengi hatuamini ktk professionalism
Kulingana na experience yangu (17+ yrs) nimeshuhudia vijana wa Kiislam ambao wamekosa position ktk Islamic windows ktk taasisi mbalimbali ambazo zinazotoa huduma za Islamic banking kwa sababu tu ya kukosa weledi ktk mawanda hayo
Nimeshuhudia vijana wasio Waislam wakinyakuwa position mbalimbali ktk Islamic windows wakiwa na weledi mpana ktk sector hiyo bila kujali dini zao
Kuna vyuo ambavyo vinatoa Certificate/Diploma/Degree etc za Islamic Finance na ktk facilitators wao hakuna hata mmoja ambaye ni Muislam na wanatoa madini si ya kawaida
 
Pelekeni hiyo kitu kwenye madrasa au misikiti yenu. Kama shuleni ifundishwe kama option. Umeshajiuliza hawa waliimmu wa masomo ya dini watakwa wameajiriwa na nani? Unajua katiba inasemaje kuhusu serikali kuendesha shughulli za dini? Yaani kodi ya wataanzania itumike kulipa walimu wa dini? Si ni kuvunja katiba huko? Kwnani nchi yetu ni ya kidini? Huoni kwa lazima kutakuwa na upendeleo kwenye ufaulu kwenye haya masomo ya dini? Tanzania siyo nchi ya kidini na itabaki hivyo.
 
Hivi huko mashuleni huwa mnaenda kufanya nini ?
Wapi umekuta Divinity au Islamic Knowledge ni Compulsory ?
 
Duuh.... Tafsiri ya wapi hiyo ndugu?
Kwani Islamic knowledge haiwezekani kuwa ndani ya divinity?
O-level ilikuwa inaitwa Bible knowledge. Advance ilikuwa inaitwaje?
 
Mnaenda hijja kidini au kiserikali? Kama ni kidini serikali inahusikaje hapo?Hizo bank kama zinahitaji watu wa hiyo fani zitajua zinawapatia wapi. Haitakiwi kutumia rasilimali za umma kufundisha watu kuhusu dini moja au nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…