Kuna jamaa yangu mmachane alipata demu mkibosho wote ni wazaliwa wa dar, ila Mikasa ilianza demu alipopata ujauzito familia ya mshkaji iligoma kabisa kumtambua demu kama mkwe, ikafika kipindi demu kajifungua wanataka kubatiza mtoto familia ya jamaa iligoma kabisa kutoa ushirikiano demu akawa analia tu, sisi tunakula bia tunamwambia Shem kausha yataisha, Sasa ikafika point jamaa anataka kufunga ndoa hapo ndo familia yake ikaona mshenzi huyu wakaamua kumfukuza kwenye nyumba aliyojenga kwenye uwanja wa familia, tulienda Moshi kwenye send-off ya demu masela tupu hakuna ndugu hata mmoja wa mwanaume, ila baada ya send-off tulikaa kama kamati tukamshauri mwana asitishe masuala ya harusi maana maneno na vikao vya ndugu kumlaani vilikua vingi sana, hadi leo jamaa anaishi na demu wanalea mtoto wao bila kufunga ndoa, niliongea na baadhi ya ndugu was jamaa wanasema ni bora angeoa demu wa kigoma au shinyanga kuliko kuoa mmachame