Nini hasa kinaendelea ndani ya CWT (iwafikie walimu wote na jamii ya Watanzania)

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
3,417
Reaction score
6,149
NINI HASA KINAENDELEA NDANI YA CWT (IWAFIKIE WALIMU WOTE NA JAMII YA WATANZANIA)

Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii huenda umekutana na taarifa za uteuzi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) kuwa wakuu wa wilaya mnamo tarehe 25 Januari 2023; mwalimu Leah Ulaya rais wa CWT kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, mwalimu Japhet Maganga Katibu Mkuu wa CWT kuwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mwingine ni Mwalimu Dina Mathamani aliyekuwa makamu wa rais wa CWT hadi disemba 2022 aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Uvinza.

Baada ya Uteuzi huo mengi yamezungumzwa na kuandikwa na wadau mbalimbali na kama ilivyo kawaida yetu walimwengu kumekua na taarifa nyingi zilizoibua hisia mchanganyiko hasa ukizingatia kuwa hivi karibuni kumekua na sintofahamu nyingi ndani ya chama cha walimu Tanzania ambazo zilimalizwa kwenye mkutano mkuu wa CWT uliofanyika Disemba 2022 mjini Dodoma ukumbi wa Venance Mabeyo ambapo kwa mujibu wa katiba ya CWT rais wa Chama ambaye alisimamishwa kimizengwe mwaka mmoja na nusu uliopita na baraza la taifa.

Mkutano mkuu wa chama ulimrejesha Leah Ulaya kwenye nafasi yake kama rais wa CWT na kwa mujibu wa katiba ya CWT Japhet Maganga aliyekuwa naibu katibu mkuu alipewa ukatibu mkuu baada ya aliyekuwa katibu mkuu Deus Seif kutiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kosa la wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka hivyo kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani tarehe 28 Juni 2022.

Ni busara kwa kila Muungwana kutokushabikia upande wowote na kujaribu kulifuatilia jambo hili kwa undani na kujihoji maswali ya msingi ambayo yatapelekea kuelewa ni nini hasa kinachoendelea ndani ya chama cha walimu Tanzania (CWT).

Swali la kwanza la msingi ambalo kila mwenye akili na busara anatakiwa kujiuliza ni kuwa je uteuzi wa viongozi waandamizi wa CWT kwa nafasi za uDc na Mheshimiwa Rais una maana gani? Inapokuja taarifa ya uteuzi wa kiongozi hasa kwenye jukumu nyeti kama la kumsaida Mheshimiwa Rais katika nafasi kama ya mkuu wa wilaya ni wazi kuwa ni taarifa ya kufurahisha ambayo kila mzalendo na mwenye mapenzi mema na nchi yake si tu angependa kutimiza jukumu hilo bali pia asingekubali kufanya jukumu hilo chini ya kiwango na matarajio ya Mheshimiwa Rais. Lakini swali la msingi ni kuwa je, uteuzi wa viongozi wote waandamizi wa chama cha walimu Tanzania unakiacha chama katika hali gani?

Baada ya kufatilia taarifa ya uteuzi wa viongozi hao vyanzo vilibaini kuwa uteuzi huo ulimaanisha kuwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa chama hicho tarehe 1 novemba 1993 chama kingeelekea kwenye mikutano ya kikatiba ya chama ambayo ni kamati ya utendaji ya taifa na baadae baraza la taifa vinavyoendelea kufanyika jijini Tanga bila ya uwepo wa kiongozi yeyote mwandamizi wa chama madarakani kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha Walimu Tanzania.

Hakingekuwa na rais wala makamu wake, katibu mkuu wala naibu wake, na kingekuwa tu na mwekahazina wa muda ambaye aliteuliwa na baraza la taifa baada ya aliyekuwepo Abubakari Salum Alawi kuhukumiwa kifungo yeye na aliyekuwa katibu mkuu Deus Seif kama ilivyobainishwa hapo juu; rais na katibu mkuu ndio walioandaa na kuitisha vikao hivi ambavyo vimeanza tarehe 30 Januari hadi tarehe 7 februari 2023 ikiwa ni Siku tano tu tangu viongozi hao wateuliwe kwa nafasi ya uDc.

Ni kiongozi asiye na busara pekee ambaye baada ya Uteuzi huo angekimbilia kituo kipya cha kazi bila kuhakikisha kuwa kuna makabidhiano ya majukumu yake ya kiofisi na ni yupi hasa anayepokea majukumu yake kwa kufuata utaratibu na katiba ya CWT ukizingatia historia ya miaka 4 iliyopita ya ubadhirifu uliokuwa ukitendeka wa mali na fedha za chama.

Swali la pili la kuhoji ni je ni kweli kuwa viongozi wa CWT walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya walikataa teuzi? Na kama ni kweli je taarifa za kukataa uteuzi nani anapaswa kuzitoa? Ni wao wenyewe, mamlaka iliyowateua, au mitandao ya kijamii na vyombo vya habari? Na kama ni wao wenyewe wanapaswa kuzitoa kwa nani? Kwa taaluma yao, uzoefu wao wa uongozi na busara zao zilizoufanya mkutano mkuu wa CWT kuwateua Disemba 2022 hawawezi wakakacha uteuzi wao kihuni.

Wanawajibika kwa mamlaka iliyowateua. Baada ya taarifa ya uteuzi kukaibuka taarifa za kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na vyama vya siasa walianza kuwashinikiza na hata kuwatishia kuwa ni lazima wakaripoti na kuapishwa ili wasije kuchukuliwa hatua za kinidhamu japo hawasemi zingechukuliwa na nani. Kilichojificha hapa ni kwamba washinikizaji na watishiaji hawa walitaka viongozi wa CWT waende kuapishwa na wakiache chama kikiwa yatima ili watumie ushawishi wao kuwaleta madarakani kwa namna na gharama yoyote viongozi wanaowataka wao ili wafaidike na fedha na rasilimali za chama.

Hii sio speculation kwani kama leo hii serikali au mamlaka zake zingeamua kufanya forensic audit za fedha mali za chama tangu Deus Seif aingie madarakani 2018 itabainika namna CWT ilivyofanyiwa ufujaji wa kutisha wa fedha na rasilimali wafaidika wakiwa ni viongozi waandamizi wa serikali na vyama vya siasa, hata moja ya timu ya mpira wa miguu ligi kuu Tanzania bara imekua ikifaidika na fedha hizi.

TAKUKURU wana taarifa na vielelezo vyote kwa miaka miwili sasa juu ya ufisadi wa Bilioni 5 za Tisheti za CWT, pamoja na kuwasainisha watuhumiwa document za kwenda mahakamani, kesi hiyo halijaanza hadi leo. Kuna tuzo za walimu bora zilizotolewa 2022 zikihusisha TAMISEMI na CWT mjini Dodoma bajeti ilikua ni zaidi ya milioni 300 lakini fedha iliyotoka CWT kwa hafla hiyo ni Bilioni 1, Katibu Mkuu na mwekahazina wa chama wakihusika kikamilifu, hili TAKUKURU pia wanalijua.

Pale ambapo mteuliwa kwa busara zake anabaini kuwa hatoshi kwenye nafasi fulani au kwamba kazi hiyo hataifanya kwa ufanisi ni jambo la busara kuiambia mamlaka ya uteuzi na jambo hilo linategemewa kufanyika kabla ya kuutangazia umma juu ya uteuzi huo. Je wateuliwa walipewa taarifa ya kuteuliwa kwao kabla ya kutangaziwa umma?

Taarifa ya kuteuliwa na kisha wateuliwa kutokwenda kuripoti kwa wakati inaashiria kwamba kuna kundi la watu wanaoaminiwa na Mheshimiwa Rais ambao wanashindwa kumsaidia kwa kutengeneza utaratibu wa teuzi hizo hali inayopelekea kuzua taharuki na kuchonganisha mamlaka ya Rais na wateuliwa.

Jambo la Tatu la kujihoji ni taarifa za kuwepo kwa makundi ndani ya Chama Cha Walimu. Vyanzo vya uhakika ndani ya CWT vinabainisha kuwa wakati wa mkutano mkuu disemba 2022 kumekuwepo na makundi 2 ndani ya Chama tofauti na uvumi unaotembea kuwa kumekuwa na makundi mengi.

Kundi Moja dogo likiwa ni kundi la viongozi wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT Bw. Deus Seif ambaye yeye pamoja na aliyekuwa Mwekahazina Bw. Abubakari Alawi walihukumiwa kwenda jela kwa ubadhirifu wa fedha za Chama.

Kundi lingine kubwa likiwa la Katibu Mkuu wa Sasa Bw. Japhet Maganga na rais Leah Ulaya ambao walipitishwa na Mkutano mkuu wa CWT mwezi Disemba 2022 kwa kauli moja kwa nafasi zao; viongozi hawa waliapa kurejesha utulivu na mshikamano ndani ya chama na kupambana na ufisadi, utulivu na mshikamano huo ulionekana kwenye mkutano mkuu wa CWT disemba 2022 hadi kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya taifa na baraza la taifa uliofanyika tarehe 30 januari hadi 7 februari 2023 jijini Tanga huku vikao hivyo pamoja na mambo mengine vikishughulika na maandalizi ya mkutano mkuu wa dharura wa CWT machi 2023 ili pamoja na mambo mengine kujaza nafasi za makamu wa rais, naibu katibu mkuu na mweka hazina wa taifa.

Uteuzi wa viongozi hawa umezaa tafsiri kinzani kwa walimu. Wapo baadhi wanaoamini uteuzi huo ni faida kwao kwani uchapakazi wao umeonekana na mamlaka ya uteuzi na wapo walimu wengi wanaoamini viongozi hao wameteuliwa kama njia ya kupisha baadhi ya wahuni waliokuwa wakitolea macho fedha za CWT ambapo uwepo wao ungekua kikwazo cha kukamilisha uhuni huo.

Kilichoshangaza zaidi ni wakati wa kikao cha kamati ya utendaji ya taifa ya CWT kilichofanyika ukumbi wa Naivera Tanga ambapo, idadi ya waandishi wa habari na polisi waliokuwa nje ya ukumbi ilizidi ile ya wajumbe wa kikao. Kwa nini walifurika kwa kiasi kile? Ilipobainika hali ya usalama ni shwari, makundi yaliyokuwa nje ya ukumbi yaliondoka, kongole kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga ikiongozwa na mkuu wa mkoa Komredi Omary Mgumba aliyeingia kwenye mkutano huo na kuwathibitishia wajumbe kwamba uvumi wa kutokuwepo kwa usalama ulikuwa ni wa kipuuzi na wajumbe waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Kwa taarifa za Kuaminika ni kuwa kuna kundi la wanasiasa ambalo kwa nafasi zao wamekua wakimhujumu Mheshimiwa Rais kwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama cha walimu, mgawanyiko huo ni wa kimaslahi na sio wa ufanisi. Kwa wakati sahihi wahusika watadhihirishwa mbele ya umma wa Watanzania.

Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya Leah Ulaya na Japhet Maganga kuteuliwa kwenye nafasi za uDc shinikizo lilianza kutoka kwa baadhi ya wanasiasa waandamizi serikalini kwamba wateuliwa waende wakaripoti haraka iwezekanavyo; tarehe 31 Januari kwa mfano, mmoja wa mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema kwamba viongozi hao wasipokwenda kuripoti kwa kuwa wameazimwa kutoka serikalini na kwa kuwa wanawajibika kwenye mamlaka nyingi za serikali na hasa wakifika mezani kwake watawajibishwa.

Leah Ulaya rais wa chama ni mwalimu wa sekondari huko Tabora na ana vipindi darasani ameazimwa na nani? Aliyelengwa hapa ni Japhet Maganga ambaye ameazimwa kutoka serikalini kwa mkataba wa miaka 3 unaoishia 2025. Upotoshaji mwingine kwenye vyombo vya habari ni ule wa Dkt. Avemaria Semakafu wa tarehe 31 Januari 2022 na kati ya mengi aliyopotosha umma alisema kwamba wanachama wa CWT wanakatwa asilimia 2 ya mshahara wao na wanapostaafu wanaishia kupata bati 20 kama mkono wa kwaheri.

Asichokijua Semakafu ni kwamba vyama vyote 13 vya wafanyakazi Tanzania chini ya TUCTA na 18 vya wafanyakazi visivyo chini ya TUCTA wanachama wao wanakatwa asilimia 2 ya mishahara yao kama CWT lakini kwa vyama vyote hivyo hakuna kinachotoa mabati wala golden handshake ya aina yoyote kwa wanachama wake isipokuwa CWT. Eti badala ya kupongeza anaponda, huu ni umbumbumbu wa hali ya juu usiolingana na elimu yake . Kingine asichokijua ni kwamba asilimia 15 ya marejesho ya michango ya wanachama kila wilaya yanarejeshwa sehemu za kazi ambazo ni shule na vyuo ambapo wanachama wanapata pesa wanazoziamulia matumizi yake kila mwezi. Ni vizuri wanasiasa wanapoamua kusema mambo wajue undani wa mambo hayo badala ya kukurupuka na kuupotosha umma. Ukweli kuhusu mgawanyo wa fedha za CWT rejea kanuni za chama toleo la 4 la 2014.

Kwenye Sakata la Leah Ulaya na Japhet Maganga tunajiuliza ni kwa nini baadhi ya viongozi wa serikali na baadhi ya wanasiasa waandamizi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanalishadadia jambo hili, wateuliwa wanajua mamlaka iliyowateua na mustakabali wao utatoka kwenye mamlaka hiyo hiyo. Tarehe 31 Januari 2023 Mkuu wa Mkoa wa Tanga mhe Omary Mgumba aliingia kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya taifa ya CWT akasema kwamba viongozi wa CWT ni halali, aliyewateua anajua wako wapi; kuteuliwa na kutoa udhuru sio jambo la ajabu na wao sio wa kwanza kufanya hivyo hapa nchini, mustakabali wa viongozi hao uko mikononi mwa aliyewateua, alisema anawatambua viongozi hao halali na waendelee na vikao vyao. Ukweli ni kwamba Mastermind anayechanganya chama cha walimu na serikali ni huyu pichani Bw. Deus Seif aliyehukumiwa kifungo cha miezi 6 na Hakimu Mkazi Kisutu mhe. Richard Kabate kwa kosa la wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka.

Huyu ndiye anayeratibu kila kitu kwenye kuwayumbisha walimu, chama chao, na kuwachonganisha na serikali. Ni mtu hatari sana, ikifanyika forensic audit kwa usimamizi wa serikali na mamlaka zake kwa muda aliokuwa katibu mkuu wa CWT watabainika majambazi wote waliokula fedha za walimu, walioko serikalini na kwenye sekta binafsi.

Baada ya Deus Seif na Abubakari Alawi kumaliza kifungo chao cha miezi sita gereza la ukonga, ambapo kwa uhalisia walikaa juma moja na wakatoka kinyemela, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikata rufaa mahakama kuu na mafisadi hao pia walikata rufaa, mvutano wa awali ulikua kwamba, kesi ni moja kwa nini iwe na majaji wawili? Wao walisisitiza kuwa wanae Jaji wao na kwa maisha yao yote ndani ya CWT wamekua na falsafa ya kwamba (hakuna mkate mgumu mbele ya chai), rufaa imekwishasikilizwa na hukumu inayosubiriwa na walimu wa nchi hii na jamii imepangwa kutoka tarehe 17 februari 2023 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam chumba namba 4 na itatolewa na Mhe. Jaji Ephery Kisanya.

Kuna taarifa inayokaribia kuaminika kwamba Deus Seif na Abubakari Alawi wamesaidiwa na baadhi ya wanasiasa waandamizi na baadhi ya watu mashuhuri wachache kuwaandikia document na kuwashika mkono hadi mamlaka za juu kuelezea namna chama kilivyotoa misaada kwenye jamii wakati wakiwa madarakani ili ikiwezekana wafutiwe kesi yao na warudi kuwa watumishi wa umma. Hilo likitokea kama ni kwa figisu zitaidhalilisha TAKUKURU/JAMHURI na kesi zilizoko mbele yao hazitaendelea na mbaya zaidi walimu watakata tamaa na kuthibitisha uthabiti wa usemi kwamba hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
 
Aliyeandika ni kati ya wale wateule wawili wa Rais aliyekataa uteuzi. Nahisi huyu ni Maganga
Ukiisoma vizuri utagundua haya ni mapambano dhidi ya wahuni, Maganga hana nguvu ya haya mapambano. huu ni mwandiko wa kizalendo. Turudi kwenye hoja
 
Sawa ndugu Maganga ila nyie munalipi la kujivunia ambalo mumeweza kuwatetea walimu likafanikiwa? CWT ni tawi la CCM na ccm inaitumia CWT kuwakandamiza walimu na kuwanyanyasa. CWT na walimu wake wanapeana kazi za kwenda kusimamia uchaguzi wanaisaidia CCM kuiba Kura. Kwahiyo CWT na serikali ni kitu Kimoja kabisa. Hapo kinachogambaniwa ni maslahi tu kati ya yule mwizi aliyefungwa ukonga seif na mwenzake na wezi wengine wapya ambao ni viongozi wapya wa CWT
 
Rudi kwenye hoja, usiseme kila kitu kinachoujaza moyo wako
 
NINI HASA KINAENDELEA NDANI YA CWT (IWAFIKIE WALIMU WOTE NA JAMII YA WATANZANIA)

Kama umekuwa mfuatiliaji mzuri wa mitandao ya kijamii huenda umekutana na taarifa za uteuzi wa baadhi ya viongozi waandamizi wa chama cha walimu Tanzania (CWT) kuwa wakuu wa wilaya mnamo tarehe 25 Januari 2023; mwalimu Leah Ulaya rais wa CWT kuwa mkuu wa Wilaya ya Mbogwe, mwalimu Japhet Maganga Katibu Mkuu wa CWT kuwa mkuu wa Wilaya ya Kyerwa mwingine ni Mwalimu Dina Mathamani aliyekuwa makamu wa rasi wa CWT hadi disemba 2022 aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Uvinza.

Baada ya Uteuzi huo mengi yamezungumzwa na kuandikwa na wadau mbalimbali na kama ilivyo kawaida yetu walimwengu kumekua na taarifa nyingi zilizoibua hisia mchanganyiko hasa ukizingatia kuwa hivi karibuni kumekua na sintofahamu nyingi ndani ya chama cha walimu Tanzania ambazo zilimalizwa kwenye mkutano mkuu wa CWT uliofanyika Disemba 2022 mjini Dodoma ukumbi wa Venance Mabeyo ambapo kwa mujibu wa katiba ya CWT rais wa Chama ambaye alisimamishwa kimizengwe mwaka mmoja na nusu uliopita na baraza la taifa, mkutano mkuu wa chama ulimrejesha Leah Ulaya kwenye nafasi yake kama rais wa CWT na kwa mujibu wa katiba ya CWT Japhet Maganga aliyekuwa naibu katibu mkuu alipewa ukatibu mkuu baada ya aliyekuwa katibu mkuu Deus Seif kutiwa hatiani na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kwa kosa la wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka hivyo kuhukumiwa kifungo cha miezi 6 gerezani tarehe 28 Juni 2022.

Ni busara kwa kila Muungwana kutokushabikia upande wowote na kujaribu kulifuatilia jambo hili kwa undani na kujihoji maswali ya msingi ambayo yatapelekea kuelewa ni nini hasa kinachoendelea ndani ya chama cha walimu Tanzania (CWT).

Swali la kwanza la msingi ambalo kila mwenye akili na busara anatakiwa kujiuliza ni kuwa je uteuzi wa viongozi waandamizi wa CWT kwa nafasi za uDc na Mheshimiwa Rais una maana gani? Inapokuja taarifa ya uteuzi wa kiongozi hasa kwenye jukumu nyeti kama la kumsaida Mheshimiwa Rais katika nafasi kama ya mkuu wa wilaya ni wazi kuwa ni taarifa ya kufurahisha ambayo kila mzalendo na mwenye mapenzi mema na nchi yake si tu angependa kutimiza jukumu hilo bali pia asingekubali kufanya jukumu hilo chini ya kiwango na matarajio ya Mheshimiwa Rais. Lakini swali la msingi ni kuwa je, uteuzi wa viongozi wote waandamizi wa chama cha walimu Tanzania unakiacha chama katika hali gani?

Baada ya kufatilia taarifa ya uteuzi wa viongozi hao vyanzo vilibaini kuwa uteuzi huo ulimaanisha kuwa kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa chama hicho tarehe 1 novemba 1993 chama kingeelekea kwenye mikutano ya kikatiba ya chama ambayo ni kamati ya utendaji ya taifa na baadae baraza la taifa vinavyoendelea kufanyika jijini Tanga bila ya uwepo wa kiongozi yeyote mwandamizi wa chama madarakani kwa mujibu wa Katiba ya Chama cha walimu Tanzania, hakingekuwa na rais wala makamu wake, katibu mkuu wala naibu wake, na kingekuwa tu na mwekahazina wa muda ambaye aliteuliwa na baraza la taifa baada ya aliyekuwepo Abubakari Salum Alawi kuhukumiwa kifungo yeye na aliyekuwa katibu mkuu Deus Seif kama ilivyobainishwa hapo juu; rais na katibu mkuu ndio walioandaa na kuitisha vikao hivi ambavyo vimeanza tarehe 30 Januari hadi tarehe 7 februari 2023 ikiwa ni Siku tano tu tangu viongozi hao wateuliwe kwa nafasi ya uDc.

Ni kiongozi asiye na busara pekee ambaye baada ya Uteuzi huo angekimbilia kituo kipya cha kazi bila kuhakikisha kuwa kuna makabidhiano ya majukumu yake ya kiofisi na ni yupi hasa anayepokea majukumu yake kwa kufuata utaratibu na katiba ya CWT ukizingatia historia ya miaka 4 iliyopita ya ubadhirifu uliokuwa ukitendeka wa mali na fedha za chama.

Swali la pili la kuhoji ni je ni kweli kuwa viongozi wa CWT walioteuliwa kuwa wakuu wa wilaya walikataa teuzi? Na kama ni kweli je taarifa za kukataa uteuzi nani anapaswa kuzitoa? Ni wao wenyewe, mamlaka iliyowateua, au mitandao ya kijamii na vyombo vya habari? Na kama ni wao wenyewe wanapaswa kuzitoa kwa nani? Kwa taaluma yao, uzoefu wao wa uongozi na busara zao zilizoufanya mkutano mkuu wa CWT kuwateua Disemba 2022 hawawezi wakakacha uteuzi wao kihuni.

Wanawajibika kwa mamlaka iliyowateua. Baada ya taarifa ya uteuzi kukaibuka taarifa za kuwa baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na vyama vya siasa walianza kuwashinikiza na hata kuwatishia kuwa ni lazima wakaripoti na kuapishwa ili wasije kuchukuliwa hatua za kinidhamu japo hawasemi zingechukuliwa na nani. Kilichojificha hapa ni kwamba washinikizaji na watishiaji hawa walitaka viongozi wa CWT waende kuapishwa na wakiache chama kikiwa yatima ili watumie ushawishi wao kuwaleta madarakani kwa namna na gharama yoyote viongozi wanaowataka wao ili wafaidike na fedha na rasilimali za chama.

Hii sio speculation kwani kama leo hii serikali au mamlaka zake zingeamua kufanya forensic audit za fedha mali za chama tangu Deus Seif aingie madarakani 2018 itabainika namna CWT ilivyofanyiwa ufujaji wa kutisha wa fedha na rasilimali wafaidika wakiwa ni viongozi waandamizi wa serikali na vyama vya siasa, hata moja ya timu ya mpira wa miguu ligi kuu Tanzania bara imekua ikifaidika na fedha hizi. TAKUKURU wana taarifa na vielelezo vyote kwa miaka miwili sasa juu ya ufisadi wa Bilioni 5 za Tisheti za CWT, pamoja na kuwasainisha watuhumiwa document za kwenda mahakamani, kesi hiyo halijaanza hadi leo. Kuna tuzo za walimu bora zilizotolewa 2022 zikihusisha TAMISEMI na CWT mjini Dodoma bajeti ilikua ni zaidi ya milioni 300 lakini fedha iliyotoka CWT kwa hafla hiyo ni Bilioni 1, Katibu Mkuu na mwekahazina wa chama wakihusika kikamilifu, hili TAKUKURU pia wanalijua.

Pale ambapo mteuliwa kwa busara zake anabaini kuwa hatoshi kwenye nafasi fulani au kwamba kazi hiyo hataifanya kwa ufanisi ni jambo la busara kuiambia mamlaka ya uteuzi na jambo hilo linategemewa kufanyika kabla ya kuutangazia umma juu ya uteuzi huo. Je wateuliwa walipewa taarifa ya kuteuliwa kwao kabla ya kutangaziwa umma?

Taarifa ya kuteuliwa na kisha wateuliwa kutokwenda kuripoti kwa wakati inaashiria kwamba kuna kundi la watu wanaoaminiwa na Mheshimiwa Rais ambao wanashindwa kumsaidia kwa kutengeneza utaratibu wa teuzi hizo hali inayopelekea kuzua taharuki na kuchonganisha mamlaka ya Rais na wateuliwa.

Jambo la Tatu la kujihoji ni taarifa za kuwepo kwa makundi ndani ya Chama Cha Walimu. Vyanzo vya uhakika ndani ya CWT vinabainisha kuwa wakati wa mkutano mkuu disemba 2022 kumekuwepo na makundi 2 ndani ya Chama tofauti na uvumi unaotembea kuwa kumekuwa na makundi mengi.

Kundi Moja dogo likiwa ni kundi la viongozi wanaomuunga mkono aliyekuwa Katibu Mkuu wa CWT Bw. Deus Seif ambaye yeye pamoja na aliyekuwa Mwekahazina Bw. Abubakari Alawi walihukumiwa kwenda jela kwa ubadhirifu wa fedha za Chama.

Kundi lingine kubwa likiwa la Katibu Mkuu wa Sasa Bw. Japhet Maganga na rais Leah Ulaya ambao walipitishwa na Mkutano mkuu wa CWT mwezi Disemba 2022 kwa kauli moja kwa nafasi zao; viongozi hawa waliapa kurejesha utulivu na mshikamano ndani ya chama na kupambana na ufisadi, utulivu na mshikamano huo ulionekana kwenye mkutano mkuu wa CWT disemba 2022 hadi kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya taifa na baraza la taifa uliofanyika tarehe 30 januari hadi 7 februari 2023 jijini Tanga huku vikao hivyo pamoja na mambo mengine vikishughulika na maandalizi ya mkutano mkuu wa dharura wa CWT machi 2023 ili pamoja na mambo mengine kujaza nafasi za makamu wa rais, naibu katibu mkuu na mweka hazina wa taifa.

Uteuzi wa viongozi hawa umezaa tafsiri kinzani kwa walimu. Wapo baadhi wanaoamini uteuzi huo ni faida kwao kwani uchapakazi wao umeonekana na mamlaka ya uteuzi na wapo walimu wengi wanaoamini viongozi hao wameteuliwa kama njia ya kupisha baadhi ya wahuni waliokuwa wakitolea macho fedha za CWT ambapo uwepo wao ungekua kikwazo cha kukamilisha uhuni huo.

Kilichoshangaza zaidi ni wakati wa kikao cha kamati ya utendaji ya taifa ya CWT kilichofanyika ukumbi wa Naivera Tanga ambapo, idadi ya waandishi wa habari na polisi waliokuwa nje ya ukumbi ilizidi ile ya wajumbe wa kikao. Kwa nini walifurika kwa kiasi kile? Ilipobainika hali ya usalama ni shwari, makundi yaliyokuwa nje ya ukumbi yaliondoka, kongole kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Tanga ikiongozwa na mkuu wa mkoa Komredi Omary Mgumba aliyeingia kwenye mkutano huo na kuwathibitishia wajumbe kwamba uvumi wa kutokuwepo kwa usalama ulikuwa ni wa kipuuzi na wajumbe waendelee na shughuli zao kama kawaida.

Kwa taarifa za Kuaminika ni kuwa kuna kundi la wanasiasa ambalo kwa nafasi zao wamekua wakimhujumu Mheshimiwa Rais kwa kuchochea mgawanyiko ndani ya chama cha walimu, mgawanyiko huo ni wa kimaslahi na sio wa ufanisi. Kwa wakati sahihi wahusika watadhihirishwa mbele ya umma wa Watanzania.

Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya Leah Ulaya na Japhet Maganga kuteuliwa kwenye nafasi za uDc shinikizo lilianza kutoka kwa baadhi ya wanasiasa waandamizi serikalini kwamba wateuliwa waende wakaripoti haraka iwezekanavyo; tarehe 31 Januari kwa mfano, mmoja wa mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alijitokeza kwenye vyombo vya habari na kusema kwamba viongozi hao wasipokwenda kuripoti kwa kuwa wameazimwa kutoka serikalini na kwa kuwa wanawajibika kwenye mamlaka nyingi za serikali na hasa wakifika mezani kwake watawajibishwa.

Leah Ulaya rais wa chama ni mwalimu wa sekondari huko Tabora na ana vipindi darasani ameazimwa na nani? Aliyelengwa hapa ni Japhet Maganga ambaye ameazimwa kutoka serikalini kwa mkataba wa miaka 3 unaoishia 2025. Upotoshaji mwingine kwenye vyombo vya habari ni ule wa Dkt. Avemaria Semakafu wa tarehe 31 Januari 2022 na kati ya mengi aliyopotosha umma alisema kwamba wanachama wa CWT wanakatwa asilimia 2 ya mshahara wao na wanapostaafu wanaishia kupata bati 20 kama mkono wa kwaheri.

Asichokijua Semakafu ni kwamba vyama vyote 13 vya wafanyakazi Tanzania chini ya TUCTA na 18 vya wafanyakazi visivyo chini ya TUCTA wanachama wao wanakatwa asilimia 2 ya mishahara yao kama CWT lakini kwa vyama vyote hivyo hakuna kinachotoa mabati wala golden handshake ya aina yoyote kwa wanachama wake isipokuwa CWT. Eti badala ya kupongeza anaponda, huu ni umbumbumbu wa hali ya juu usiolingana na elimu yake . Kingine asichokijua ni kwamba asilimia 15 ya marejesho ya michango ya wanachama kila wilaya yanarejeshwa sehemu za kazi ambazo ni shule na vyuo ambapo wanachama wanapata pesa wanazoziamulia matumizi yake kila mwezi. Ni vizuri wanasiasa wanapoamua kusema mambo wajue undani wa mambo hayo badala ya kukurupuka na kuupotosha umma. Ukweli kuhusu mgawanyo wa fedha za CWT rejea kanuni za chama toleo la 4 la 2014.

Kwenye Sakata la Leah Ulaya na Japhet Maganga tunajiuliza ni kwa nini baadhi ya viongozi wa serikali na baadhi ya wanasiasa waandamizi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanalishadadia jambo hili, wateuliwa wanajua mamlaka iliyowateua na mustakabali wao utatoka kwenye mamlaka hiyo hiyo. Tarehe 31 Januari 2023 Mkuu wa Mkoa wa Tanga mhe Omary Mgumba aliingia kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya taifa ya CWT akasema kwamba viongozi wa CWT ni halali, aliyewateua anajua wako wapi; kuteuliwa na kutoa udhuru sio jambo la ajabu na wao sio wa kwanza kufanya hivyo hapa nchini, mustakabali wa viongozi hao uko mikononi mwa aliyewateua, alisema anawatambua viongozi hao halali na waendelee na vikao vyao. Ukweli ni kwamba Mastermind anayechanganya chama cha walimu na serikali ni huyu pichani Bw. Deus Seif aliyehukumiwa kifungo cha miezi 6 na Hakimu Mkazi Kisutu mhe. Richard Kabate kwa kosa la wizi wa fedha za walimu na matumizi mabaya ya madaraka.

Huyu ndiye anayeratibu kila kitu kwenye kuwayumbisha walimu, chama chao, na kuwachonganisha na serikali. Ni mtu hatari sana, ikifanyika forensic audit kwa usimamizi wa serikali na mamlaka zake kwa muda aliokuwa katibu mkuu wa CWT watabainika majambazi wote waliokula fedha za walimu, walioko serikalini na kwenye sekta binafsi.

Baada ya Deus Seif na Abubakari Alawi kumaliza kifungo chao cha miezi sita gereza la ukonga, ambapo kwa uhalisia walikaa juma moja na wakatoka kinyemela, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilikata rufaa mahakama kuu na mafisadi hao pia walikata rufaa, mvutano wa awali ulikua kwamba, kesi ni moja kwa nini iwe na majaji wawili? Wao walisisitiza kuwa wanae Jaji wao na kwa maisha yao yote ndani ya CWT wamekua na falsafa ya kwamba (hakuna mkate mgumu mbele ya chai), rufaa imekwishasikilizwa na hukumu inayosubiriwa na walimu wa nchi hii na jamii imepangwa kutoka tarehe 17 februari 2023 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam chumba namba 4 na itatolewa na Mhe. Jaji Ephery Kisanya.

Kuna taarifa inayokaribia kuaminika kwamba Deus Seif na Abubakari Alawi wamesaidiwa na baadhi ya wanasiasa waandamizi na baadhi ya watu mashuhuri wachache kuwaandikia document na kuwashika mkono hadi mamlaka za juu kuelezea namna chama kilivyotoa misaada kwenye jamii wakati wakiwa madarakani ili ikiwezekana wafutiwe kesi yao na warudi kuwa watumishi wa umma. Hilo likitokea kama ni kwa figisu zitaidhalilisha TAKUKURU/JAMHURI na kesi zilizoko mbele yao hazitaendelea na mbaya zaidi walimu watakata tamaa na kuthibitisha uthabiti wa usemi kwamba hakuna mkate mgumu mbele ya chai.
Serikali iliporuhusu makato makubwa ya asilimia 2!

Yaliua uwajibikaji wa chama Hicho kwa walimu na kuwa pango la unyang'anyi!

Tunavuna tulichopanda!

Tumekuza wizi na kutowajibika kwa viongozi Hao!
 
Usituhumu serikali, soma Employment and Labor Relations Act No. 6 yani sheria ya ajira na mahusiano kazini ya 2004. Tubaki kwenye hoja
Serikali iliporuhusu makato makubwa ya asilimia 2!

Yaliua uwajibikaji wa chama Hicho kwa walimu na kuwa pango la unyang'anyi!

Tunavuna tulichopanda!

Tumekuza wizi na kutowajibika kwa viongozi Hao!
 
hicho ni chama cha watu wa Kigoma tu, hakina national credibility. Usiyumbishe hoja mwalimu
Kimeanzia Kigoma ,nakuhakikishia kitasambaa pamoja na hujuma ambazo CWT inafanya kukiangusha. CWT na CCM ni kopo na mfuniko.Yaliyomo humo ni wizi, ufisadi, udanganyifu, fitina na na aina zote za uovu. Sisi watu wa Kigoma tumekataa utumwa wa CWT. Natumaini mikoa mingine itaiga. Kulikuwa na mgogoro hapa Kigoma manispaa wa kuwakata wanachama wa CHAKUHAWATA agency fee, CWT mmeumbuka. Nasema hivi, walimu wote nchini wapaswa kukataa huu utumwa wa CWT.
 
Back
Top Bottom