Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Nishapitia changamoto Kama iyo,
Nilichogundua hizo Bei Ni upigaji TU.

Tatzo la dar,Udalali mwing Sana
Kampuni nyng za visima hapa dar Zina mawinga wengi Sana, inayopelekea Bei kua juu mno, kila winga ana shea Yake.

Tumia kampuni za visima zinazofanya kazi zao mikoani, Bei zao huwa chini Sana na kazi zao huwa Ni uhakika Sana.

Nmechimba visima 2 Hapa hapa dar (mita 35,kingine mita 48).
Hakuna Hata kimoja kilichozidi mil 5 kwa kila kitu, na vyote vinatoa maji mwaka mzima uhakika bila kukauka isipokua kimoja maji yake Yana chumvi.

Na wanatoa warranty ya miaka 2 Kisha kuna bima ya matengenezo, service zote unawapigia wanakuja kufanya kazi endapo kisima kikisumbua.

Option ambazo kwa kampuni nyng za dar, kuzipata Ni ndoto mno
hiyo mil5 ni uchimbaji tu au na mitambo ni juu yao ww unakabidhiwa kisima chako kimekamilika
 
Bei za wapi izo njoo tabata kuna kampuni ya kichina million 4 tu unachimbiwa mpaka mita 60..wanakuja na wataalamu wao wanapima kabisa..usifanye mchezo na wachina..wanachimba mpaka kwa mkopo unatoa 2million inayobaki mnaandikishinana unaimalizia lini..Watu mambo ya dawasco tulishayasahau.
Mkuu inategemea na water table ya maji, kuna mahsli maji yanapatikana 200m huwezi kamwe kuchimba hata kwa 5m
 
Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer(mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.

Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya
Wanakadiria kuokota dhahabu hivyo wakachaji extra.
 
Uchimbaji wa maji wakati flani ni bahati nasibu.
Wanaweza kupima maji na wakaona kuna maji.

Lakini wakati wa kuchimba wanaeeza kuyafikia lakini wasiweze kuyapandisha juu...wanadai yamekimbilia kwenye miamba.

Kazi kwetu tulipoteza 20m, maji yalichimbwa vizuri, wakayafikia, wakati wa kuyasafisha na wafitishe mabomba, hayakuweza kupanda juu.

Hasara hii tuliibeba kwasababu tulitumia wapimaji tofauti na wachimbaji.

PIli...wanadai mafuta mengi yanatumika kwa siku katika kuchimba wastani wa 500k/siku.

Tatu...gharama za mabomba kununuana ..kufitisha
Dah! So sad.
 
Bei za wapi izo njoo tabata kuna kampuni ya kichina million 4 tu unachimbiwa mpaka mita 60..wanakuja na wataalamu wao wanapima kabisa..usifanye mchezo na wachina..wanachimba mpaka kwa mkopo unatoa 2million inayobaki mnaandikishinana unaimalizia lini..Watu mambo ya dawasco tulishayasahau.
Safi sana aisee!!!.Hao jamaa wanaweza kuja Mikoani?.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Bei za wapi izo njoo tabata kuna kampuni ya kichina million 4 tu unachimbiwa mpaka mita 60..wanakuja na wataalamu wao wanapima kabisa..usifanye mchezo na wachina..wanachimba mpaka kwa mkopo unatoa 2million inayobaki mnaandikishinana unaimalizia lini..Watu mambo ya dawasco tulishayasahau.
Weka anuani mzee! Au huoni maombi yetu, au mawinga wamekupata PM wakakipiga mkwara, au ....
 
Back
Top Bottom