Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Kisima bwana ni risk sana.

Mimi nilichimba awamu ya kikwete. Ubungo maji yalikuwa shida sana..

Kipindi hicho Dumu moja linauzwa 1000. Ikabidi nichimbe kisima ili nami niuze maji.. ndio nikala hasara ya kupata maji yenye magadi kibaooo
Hasara kubwa sana uliingia
 
Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer(mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.

Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya
wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

[emoji115][emoji115][emoji115]

Ukibadili mita hizo kwenda kilomita utapata kilomita ngapi?

Hizo tarakimu vipi? Au wanzuki ipo pembeni yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NImejifunza kitu kwenye huu uzi.

1. kuchimba kisima wakati wa kiangazi..

2. Lazima ujiridhishe kwenye mtaa wako kama kuna watu walichimba na wakapata maji safi yasiyo na magadi,vinginevyo utakuwa wa mfano.

3. Kuepuka udalali mwingi ni bora kuwaendea moja kwa moja watu wa makampuni ya uchimbaji.

4. Bora kushare na mtu(jirani) katika kuchimba ili kwma ni hasara basi mgawane isiwe peke yako.😃😃
 
Katika vitu ambavyo Kila nikifikiria nakosa majibu ni gharama ya kuchimba kisima na Ile mitambo yao kiujumla, Sote tunajua kuwa katika mitambo inayouzwa bei ghali ni mitambo ya kutengeneza Barabara na ya migodini, ikiwemo Wheel loader, Excavator, Bull dozer(mashine ya kipekee ambayo ukiwa Dar unaweza kuiwasha kuweka mafuta na kuweka gia na kuielekezea Mwanza Kisha ukapanda ndege na baada ya muda litafika tu Mwanza lenyewe maana Kila mahali linapita). Sasa hii mitambo gharama ya kukodisha Kwa siku ni kati ya laki 8 Hadi milioni.

Sasa twende huku kwenye visima vya maji, wao wanakuambia Kwa MITA 50,000 Hadi 85,000 hivyo mpaka kisima unamaliza ni milioni 10+.

Sasa je ni Nini hasa kinachokuwa gharama kwao mpaka kupelekea gharama ishoot milioni 10 Kwa kisima, maana haiingii akilini, Nilielewa hii nitakaa kimya
Uku kwetu nanjilinji,ukitaka kuchimba kisima unaenda dawasco wanakupa gari bure wewe ni kujaza wese tu
 
NImejifunza kitu kwenye huu uzi.

1. kuchimba kisima wakati wa kiangazi..

2. Lazima ujiridhishe kwenye mtaa wako kama kuna watu walichimba na wakapata maji safi yasiyo na magadi,vinginevyo utakuwa wa mfano.

3. Kuepuka udalali mwingi ni bora kuwaendea moja kwa moja watu wa makampuni ya uchimbaji.

4. Bora kushare na mtu(jirani) katika kuchimba ili kwma ni hasara basi mgawane isiwe peke yako.😃😃
Ni Nawazo Mazuri Sana
Mimi Eneo Nililochimba Kuna Majirani 2 Walichimba Kwa Kutumia Watu Maji Yakapatikana Ingawa Muda Huu Kiangazi Kikali Hiki Yanasuasua

Japo Mimi Bado Yanatoka Ingawa Nilichimba December 2022 Kiangazi Kikiwa Juu Sana Na Hakuna Mvua
 
Nishapitia changamoto Kama iyo,
Nilichogundua hizo Bei Ni upigaji TU.

Tatzo la dar,Udalali mwing Sana
Kampuni nyng za visima hapa dar Zina mawinga wengi Sana, inayopelekea Bei kua juu mno, kila winga ana shea Yake.

Tumia kampuni za visima zinazofanya kazi zao mikoani, Bei zao huwa chini Sana na kazi zao huwa Ni uhakika Sana.

Nmechimba visima 2 Hapa hapa dar (mita 35,kingine mita 48).
Hakuna Hata kimoja kilichozidi mil 5 kwa kila kitu, na vyote vinatoa maji mwaka mzima uhakika bila kukauka isipokua kimoja maji yake Yana chumvi.

Na wanatoa warranty ya miaka 2 Kisha kuna bima ya matengenezo, service zote unawapigia wanakuja kufanya kazi endapo kisima kikisumbua.

Option ambazo kwa kampuni nyng za dar, kuzipata Ni ndoto mno
Umeongea kina cha kawaida sana 35m-40m kwa 5m ni kawaida tu au naweza kusema ni ghali. Kuna maeneo hapa mjini watu wanachimba hadi 120m-150m kwa around 8m-10m
 
Kuna baadhi ya maeneo hapa Dar kama ukanda wa Kimara, Mbezi, Kibamba, Ubungo usipoteze hela yako kuchimba kisima

Water table ya hayo maeneo maji yake yana magadi maana ile sio chumvi imagine hata wanyama wanayasusa
Watu wanachimba tu mbona, sema unakuwa na machine za filter ili kuchuja maji. Kuna jamaa alichimba maeneo ya mageti kuelekea goba, 120m akayakuta ni chumvi balaa, ila amefunga machine ya filter na sasa hivi anasema chumvi inaelekea kwisha.
 
Zile mashine za filter nimeona hata baadhi ya taasi hasa shule za private ukanda wa maji ya chumvi. Ila kwa yale magadi ya Kimara sijui kama zinaweza kutoboa
 
Back
Top Bottom