Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Nini hasa kinafanya gharama za kuchimba kisima kuwa mil 8, 10, 12? What is so special?

Kuna muda nilihitaji wanichimbie kisima, sema hiyo gharama maana pia nilitaka maji niuze. Ila hiyo gharama ikanishinda na Cha kushangaza wakati wa kiangazi maji yanakata.

Maji ya kisima huwa hayakauki kiangazi

Labda kama mchimbaji ni muhuni

Kwetu kwa wazazi ni temeke tuna kisima kimechimbwa miaka 30 iliyopita mpaka leo hakujawai kauka hata mara moja
 
Kuna baadhi ya maeneo hapa Dar kama ukanda wa Kimara na Mbezi usipoteze hela yako kuchimba kisima

Water table ya hayo maeneo maji yake yana magadi maana ile sio chumvi imagine hata wanyama wanayasusa

Ni kweli..

Nilichimba kisima ubungo external nikala hasara ya milioni 5 sababu ya magadi

Maji ya kisima tunayatumia kuflash vyoo tu
 
Pole sana

Mwanangu mmoja anaishi Kimara alipoteza milioni 8 kuchimba kisima

Sasa hivi kakitelekeza nafikiri naye anatumia kuflush tu

Kisima bwana ni risk sana.

Mimi nilichimba awamu ya kikwete. Ubungo maji yalikuwa shida sana..

Kipindi hicho Dumu moja linauzwa 1000. Ikabidi nichimbe kisima ili nami niuze maji.. ndio nikala hasara ya kupata maji yenye magadi kibaooo
 
Kisima bwana ni risk sana.

Mimi nilichimba awamu ya kikwete. Ubungo maji yalikuwa shida sana..

Kipindi hicho Dumu moja linauzwa 1000. Ikabidi nichimbe kisima ili nami niuze maji.. ndio nikala hasara ya kupata maji yenye magadi kibaooo
Vipimo Vyao Vinaonyesha Maji Ila Havibainishi Ladha Yake
 
Nitakachokifanya siku za usoni nikuchimba kisima changu mwenyewe using my home made tools DIY.. YouTube ni msaada tosha mpaka sasa nachohitaji now ni kununua motor yaku drive hiyo shaft wakati wa uchimbaji the rest ni tool ambazo ziko available katika mazingira ya kawaida
Kikubwa kua na maji ya kuyeyusha njia unayoichimba utaokoa nguvu nyingi sn pili unaweza tumia wale wazibuavyoo watakusaidia kwakua wanaujuzi wakuchimbamaeneo km hayo gharama inaweza isifike hata 3mil
 
Vipimo Vyao Vinaonyesha Maji Ila Havibainishi Ladha Yake

Vipimo vina ujinga mmoja kuweka exemption ili usiwashtaki.

Mimi nilipimiwa na chuo cha maji udsm.. wataalam wa wizara ya maji ndio walikuja kunipimia.

Na kwenye report yao ya upimaji wakaandika kwamba uhalisia wa maji yalivyo utapatikana baada ya uchimbaji kufanyika.. hivyo tangu kwenye prediction walijilinda kwamba hawana uhakika mpaka wachimbe kwanza
 
Back
Top Bottom