Mtoa hoja ama ni mnafiki, au ana uelewa mdogo.
Labda kwakumpa faida, tuamini kuwa ana uelewa mdogo, na hivyo tumpe shule kidogo ili aanze kuuendea weledi taratibu.
1) Baada yaminong'ono mingi kuwa Mbowe ameikalia hiyo nafasi kwa muda mrefu sana, na kuifanya CHADEMA kusemwa vibaya na wapinzani wake, Mbowe mwenyewe kwa kinywa chake, alitamka kuwa kipindi chake cha uongozi kikiisha, hatagombea tena. Uamuzi wake wa kugomvea tena, huku tayari ameishikilia nafasi hiyo kwa miaka 21, ni jambo linalomshamgaza kila mwenye akili. Maana anatengeneza mazingira ya CHADEMA kusemwa kwa ubaya na washindani wake.
2) Mwakajana ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi wa ndani ya chama, kikatiba, lakini haukumalizika, na hivyo kusogezwa mbele kidogo. Kama akili inacheza kidogo, utakuwa umepata jibu la swali lako kwa nini siyo juzi au jana. Haya siyo mapinduzi bali uchaguzi. Hivyo kudai kuwa kuna watu wanataka kumwondoa Mbowe kwenye nafasi ya umwenyekiti, ni uwongo mkubwa, na inadhihirisha kuwa wewe kwenye haya mambo ni mtupu kabisa. Mbowe anamaliza kipindi chake cha uongozi, na kisha atakabidhi kwa atakayekuwa amechaguliwa, kumpokea.